Kutazama Historia ya The New World Society in Action
Unapoitazama video hii ya filamu ya 1954, fikiria majibu ya maswali yafuatayo: (1) Kwa nini filamu hiyo ilitengenezwa, nayo ilitimiza jambo gani? (2) Mashahidi wa Yehova huchapisha vichapo gani, navyo huchapwa kwa ajili ya nani na kwa nini? (3) Kiwango cha sasa cha ugawaji wa gazeti la Mnara wa Mlinzi chalinganaje na kile cha 1954? (4) Katika miaka ya karibuni, utaratibu wa uchapaji umefanywaje kuwa wa kisasa? (5) Ni nini kinachokuvutia kuhusu mkusanyiko wa kimataifa wa 1953 uliofanywa huko Yankee Stadium? (6) Trailer City ilikuwa nini na ni mambo gani yenye kutokeza uliyoona kuihusu? (7) Ni nini kinachoonyesha kwamba kazi yetu si ya taifa moja tu, au watu wa aina moja tu? (8) Ni kwa njia zipi umeona upendo ulio ndani ya tengenezo la Yehova? (Zab. 133:1) (9) Wafikiri ni nani atafurahia kuona video hii inayoonyesha historia ya utendaji wa jamii ya ulimwengu mpya katika miaka ya 1950?