Mambo ya Kusema Kuhusu Magazeti
Mnara wa Mlinzi Mac. 15
“Je, wafikiri mafundisho ya Yesu yanafaa siku zetu? [Ngoja jibu.] Bila shaka utakubaliana na amri hii ambayo Yesu alitoa siku ya mwisho ya maisha yake duniani. [Soma Yohana 15:12.] Vilevile, Yesu alifundisha mambo mengine muhimu siku hiyo. Toleo hili la Mnara wa Mlinzi linaonyesha jinsi tunavyoweza kufaidika na mambo hayo.”
Amkeni! Mac. 22
“Je, umegundua kwamba siku hizi watu wengi hushindwa kulala vya kutosha? [Ngoja jibu.] Mahangaiko au wasiwasi unaweza kuchangia hali hiyo. [Soma Mhubiri 5:12.] Gazeti hili lazungumzia baadhi ya visababishi vya ugonjwa wa kukosa usingizi, na lina madokezo yanayofaa ya jinsi tunavyoweza kuboresha usingizi wetu.”
Mnara wa Mlinzi Apr. 1
“Hii ni picha ya kile kinachoitwa kwa kawaida Chakula cha Mwisho. [Onyesha jalada la mbele na nyuma ya gazeti.] Je, wajua kwamba hii ndiyo sherehe pekee ambayo Wakristo wanaamriwa kuadhimisha? [Ngoja jibu. Kisha soma Luka 22:19.] Gazeti hili laeleza kwa nini mwadhimisho huo ni muhimu na jinsi unavyokuhusu.”
Amkeni! Apr. 8
“Je, haisikitishi kwamba vijana wengi wameathiriwa na dawa za kulevya? [Ngoja jibu.] Mara nyingi matatizo huanza vijana wanaposhirikiana na marafiki wasiofaa. [Soma 1 Wakorintho 15:33.] Toleo hili la Amkeni! lazungumzia mambo yanayowafanya vijana waanze kutumia dawa za kulevya na kile ambacho wazazi wanaweza kufanya ili kuwalinda.”