Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/09 uku. 3
  • Je, Uko Tayari Kumwimbia Yehova Kwenye Mikutano Yetu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Uko Tayari Kumwimbia Yehova Kwenye Mikutano Yetu?
  • Huduma ya Ufalme—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Nyimbo Mpya za Ibada!
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Dokezo la Kujifunza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Imba kwa Shangwe na Sauti Kubwa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Mwimbieni Yehova!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Huduma ya Ufalme—2009
km 12/09 uku. 3

Je, Uko Tayari Kumwimbia Yehova Kwenye Mikutano Yetu?

1 Kujitayarisha ili kushiriki katika mikutano yetu kunatia ndani kujitayarisha kuimba nyimbo za sifa. Fikiria madokezo yafuatayo.

2 Kuelewa Maneno ya Nyimbo: Andiko la msingi na maandiko mengine yaliyoorodheshwa mwishoni mwa kila wimbo yanaonyesha msingi wa Kimaandiko wa maneno ya wimbo huo.

3 Fanyeni Mazoezi: Mnaweza kutumia muda fulani wakati wa Ibada ya Familia ili kujizoeza kuimba nyimbo zetu mpya. Imbeni nyimbo zilizoteuliwa kwa ajili ya kila mkutano, kwa kufuatana na muziki wa piano uliorekodiwa. Unaweza kujifunza maneno ya baadhi ya nyimbo hizo mpya na kujizoeza kuziimba kwa kusikiliza CD Mwimbieni Yehova—Muziki wa Kuimbwa, Diski ya 1.

4 Je, utakuwa tayari mwisho wa juma hili tutakapoanza kutumia kitabu cha nyimbo Mwimbieni Yehova katika Funzo la Mnara wa Mlinzi? Ndiyo, utakuwa tayari ukichukua wakati kuelewa maana ya maneno ya nyimbo zetu mpya na pia kujizoeza kuziimba.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki