Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w23 Novemba uku. 32
  • Dokezo la Kujifunza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Dokezo la Kujifunza
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jifunze Kukariri “Nyimbo za Kiroho”
  • Msifu Yehova kwa Shangwe Kupitia Nyimbo
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Je, Uko Tayari Kumwimbia Yehova Kwenye Mikutano Yetu?
    Huduma ya Ufalme—2009
  • Nyimbo Mpya za Ibada!
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Nyimbo Zinazotusaidia Kumkaribia Mungu Zaidi
    Jinsi Michango Yako Inavyotumiwa
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
w23 Novemba uku. 32

Dokezo la Kujifunza

Jifunze Kukariri “Nyimbo za Kiroho”

“Nilipopambana na hisia za kujiona sifai, Yehova alinitia moyo kwa kutumia nyimbo zilizo kwenye JW Broadcasting®.”—Lorraine, Marekani.

Sikuzote “nyimbo za kiroho” zimekuwa sehemu ya ibada ya Kikristo. (Kol. 3:16) Ukikariri nyimbo hizo, zinaweza kukusaidia hata usipokuwa na kitabu cha nyimbo au kifaa cha kielektroni. Madokezo yafuatayo yatakusaidia kukariri baadhi ya nyimbo.

  • Soma maneno ya wimbo kwa makini ili uelewe maana yake. Ukielewa maana ya jambo fulani, utalikumbuka kwa urahisi. Maneno ya nyimbo zetu zote, kutia ndani nyimbo zilizotungwa na nyimbo kwa ajili ya watoto, yanapatikana katika jw.org. Kwenye sehemu ya Maktaba, nenda kwenye Muziki.

  • Andika kwa mkono maneno ya wimbo. Kufanya hivyo kutakusaidia kukumbuka vizuri zaidi nyimbo hizo.—Kum. 17:18.

  • Fanya mazoezi kwa sauti. Soma au imba wimbo huo mara kwa mara.

  • Pima kumbukumbu yako. Jaribu kukumbuka maneno ya wimbo bila kuyatazama, na kisha uangalie kama umefanikiwa kukumbuka maneno yote.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki