The Bible—Its Power in Your Life
Biblia imesaidia mamilioni ya watu kuboresha maisha yao. Ni zipi baadhi ya kanuni za Biblia, ambazo tukizitumia, zitatusaidia kukabiliana na matatizo leo? Bila shaka utafurahia kupata jibu la swali hilo kwa kutazama video, The Bible—Its Power in Your Life, ambayo ni sehemu ya pili kati ya sehemu tatu za DVD inayoitwa The Bible—A Book of Fact and Prophecy. Baada ya kutazama sehemu hiyo ya pili, je, unaweza kujibu maswali yafuatayo?
(1) Kwa nini tunaweza kusema kwamba Biblia si kitabu bora tu? (Ebr. 4:12) (2) Ikiwa Biblia inaweza kuwasaidia watu kuboresha maisha yao, kwa nini basi wanadamu wana matatizo mengi sana? (3) Kichwa kikuu cha Biblia ni nini? (4) Ni Maandiko gani ambayo yametajwa yanayoweza kuwasaidia wenzi wa ndoa (a) kuboresha mawasiliano yao, na (b) kudhibiti hasira yao? (5) Maoni ya Mkristo kuhusu ndoa huboreshaje maisha ya familia? (Efe. 5:28, 29) (6) Yehova amewawekeaje wazazi mfano bora? (Marko 1:9-11) (7) Ni kwa njia gani wazazi wanaweza kufanya funzo la familia lifurahishe? (8) Kando na funzo la Biblia, nini kingine ambacho Neno la Mungu linawahimiza wazazi wawaandalie watoto wao? (9) Shauri la Biblia linaweza kusaidiaje familia zifanikiwe kiuchumi? (10) Ni kanuni zipi za Biblia kuhusu usafi, matumizi mabaya ya dawa na pombe, na mfadhaiko, ambazo zikitumiwa zitapunguza matatizo ya afya? (11) Ni ahadi gani za Biblia zinazoweza kututegemeza? (Ayu. 33:25; Zab. 145:16) (12) Mafundisho ya Neno la Mungu yamekusaidiaje kuboresha maisha yako? (13) Unaweza kutumiaje video hii kuwasaidia wengine?