Sababu 12 za Kuhubiri
Kwa nini sisi huhubiri na kuongoza mafunzo ya Biblia? Je, sababu ya msingi ni kuwasaidia watu wenye mioyo minyoofu waingie katika barabara inayoongoza kwenye uzima? (Mt. 7:14) Hiyo ndiyo sababu ya kwanza iliyoorodheshwa hapa chini, lakini si sababu kuu. Kati ya sababu 12 zifuatazo za kuhubiri, unafikiri ni ipi iliyo muhimu zaidi?
1. Kuhubiri husaidia kuokoa uhai.—Yoh. 17:3.
2. Husaidia kuonya waovu.—Eze. 3:18, 19.
3. Huchangia kutimia kwa unabii wa Biblia.—Mt. 24:14.
4. Huonyesha uadilifu wa Mungu. Hakuna mtu anayeweza kudai kwamba Yehova aliangamiza waovu bila kuwapa nafasi ya kutubu.—Mdo. 17:30, 31; 1 Tim. 2:3, 4.
5. Hutuwezesha kutimiza wajibu wetu wa kuandaa msaada wa kiroho kwa watu walionunuliwa kwa damu ya Yesu.—Rom. 1:14, 15.
6. Hutusaidia kuepuka hatia ya damu.—Mdo. 20:26, 27.
7. Ni takwa ili sisi wenyewe tuokolewe.—Eze. 3:19; Rom. 10:9, 10.
8. Huonyesha upendo kwa jirani.—Mt. 22:39.
9. Huonyesha utii wetu kwa Yehova na kwa Mwana wake.—Mt. 28:19, 20.
10. Ni sehemu ya ibada yetu.—Ebr. 13:15.
11. Huonyesha kwamba tunampenda Mungu.—1 Yoh. 5:3.
12. Huchangia kulitakasa jina la Yehova.—Isa. 43:10-12; Mt. 6:9.
Bila shaka, kuna sababu nyingine zaidi za kuhubiri. Kwa mfano, kuhubiri huimarisha imani yetu na pia tunapata pendeleo la kuwa wafanyakazi wenzi wa Mungu. (1 Kor. 3:9) Hata hivyo, sababu muhimu zaidi ya kuhubiri ni namba 12. Hata itikio liweje, kuhubiri huchangia kulitakasa jina la Mungu ili Yehova amjibu yule anayemdhihaki. (Met. 27:11) Kwa kweli, tuna sababu nzuri sana za ‘kuendelea bila kuacha kufundisha na kutangaza habari njema.’—Mdo. 5:42.