Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb20 Februari uku. 3
  • Unajifunza Nini Kutokana na Nyimbo Zilizotungwa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unajifunza Nini Kutokana na Nyimbo Zilizotungwa?
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
  • Habari Zinazolingana
  • Nyimbo Zinazotusaidia Kumkaribia Mungu Zaidi
    Jinsi Michango Yako Inavyotumiwa
  • Msifu Yehova kwa Shangwe Kupitia Nyimbo
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Nyimbo za Ufalme Zinatutia Moyo Tuwe na Ujasiri
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
  • Dokezo la Kujifunza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
mwb20 Februari uku. 3
Ndugu na dada wakifurahia kucheza gitaa na kuimba wakiwa nje.

MAISHA YA MKRISTO

Unajifunza Nini Kutokana na Nyimbo Zilizotungwa?

Ni nyimbo gani unazopenda zaidi kati ya nyimbo zilizotungwa? Kwa nini? Je, video za nyimbo hizo zinaonyesha mambo yanayotokea katika maisha ya kila siku? Nyimbo hizo zinawavutia watu wote kwa sababu zina vichwa mbalimbali na aina tofauti-tofauti za muziki. Isitoshe, lengo la nyimbo zilizotungwa si kutuburudisha tu.

Kila wimbo uliotungwa unatufundisha masomo muhimu tunayoweza kutumia katika maisha na huduma yetu ya Kikristo. Baadhi ya nyimbo huzungumzia ukarimu, umoja, urafiki, ujasiri, upendo, au imani. Nyingine zinazungumza kuhusu kumrudia Yehova, kusamehe, kudumisha utimilifu kila siku, na kufuatia miradi ya kiroho. Hata kuna wimbo uliotungwa kuhusu kuwa na usawaziko katika kutumia simu za mkononi. Ni masomo gani mengine muhimu ambayo umepata katika nyimbo zilizotungwa?

TAZAMA VIDEO YA WIMBO ULIOTUNGWA WENYE KICHWA PARADISO IKO KARIBU SANA, KISHA UJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Wenzi hao wa ndoa wenye umri mkubwa wanafikiria kuhusu baraka gani za wakati ujao?—Mwa 12:3

  • Tunaweza kuimarishaje imani yetu katika uwezo wa Yehova wa kutimiza ahadi zake?

  • Hivi karibuni tutafurahia kukutana tena na nani?

  • Tumaini la Ufalme linatusadiaje kuvumilia majaribu tunayopata sasa?—Ro 8:25

DOKEZO KWA AJILI YA IBADA YA FAMILIA

Tazama video za nyimbo zifuatazo zilizotungwa, kisha ujibu maswali haya mawili: Video hii inanifundisha masomo gani muhimu? Ninaweza kutumiaje masomo hayo maishani mwangu?

  • Usiogope

  • Tusameheane

  • “Fuateni Mwendo wa Ukaribishaji-Wageni”

  • Keep the Pace

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki