Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb20 Machi uku. 7
  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kuwahubiria Vipofu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kuwahubiria Vipofu
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
  • Habari Zinazolingana
  • Wasaidie Vipofu Wajifunze Kumhusu Yehova
    Huduma Yetu ya Ufalme—2015
  • Maandishi ya Vipofu Yanabadili Maisha
    Jinsi Michango Yako Inavyotumiwa
  • Kuishi Bila Kuona
    Amkeni!—2015
  • Louis Braille—Kuwaangazia Nuru Wafungwa wa Giza
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2020
mwb20 Machi uku. 7
Dada ambaye ni kipofu akitumia mikono yake kusoma chapisho la maandishi ya vipofu.

MAISHA YA MKRISTO

Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kuwahubiria Vipofu

KWA NINI NI MUHIMU: Vipofu wengi hawajihisi huru kuzungumza na mtu mgeni. Kwa hiyo, unahitaji kuwa na ustadi ili kuwatolea ushahidi. Yehova anawapenda na kuwajali vipofu. (Law 19:14) Tunaweza kuiga mfano wake kwa kuchukua hatua ya kwanza kuwasaidia vipofu kiroho.

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • “Watafute” vipofu. (Mt 10:11) Je, unamfahamu mtu aliye na mtu wa ukoo ambaye ni kipofu? Je, eneo lenu lina shule au mashirika mengine ambayo yangependa machapisho yaliyotayarishwa kwa ajili ya vipofu?

  • Onyesha upendezi wa kibinafsi. Kuonyesha urafiki na upendezi wa kweli kutamfanya mtu ambaye ni kipofu ajihisi huru. Jaribu kuanzisha mazungumzo yanayotegemea habari inayofaa eneo lenu

  • Andaa msaada wa kiroho. Ili kuwasaidia vipofu na wale wenye uwezo mdogo wa kuona, tengenezo letu limetokeza machapisho ya aina mbalimbali. Muulize mwenye-nyumba angependa kutumia njia gani kujifunza. Mwangalizi wa utumishi anapaswa kuhakikisha kwamba mtumishi wa machapisho anatoa ombi la aina ya chapisho ambalo kipofu angependa zaidi

Machapisho ya aina zifuatazo yanapatikana katika lugha kadhaa kwa ajili ya vipofu na wenye matatizo makubwa ya kuona:

  • Rekodi za kusikiliza kutoka kwenye JW Library na jw.org

  • Chapa kubwa

  • Maandishi ya vipofu (braille)

  • Faili za kielektroni kwa ajili ya vifaa vya kuandikia maandishi (vifaa vya kielektroni vilivyo na uwezo wa kutokeza sauti na kuandika maandishi ya vipofu)

  • Faili za kielektroni za kusoma skrini (programu za kompyuta ambazo husoma kwa sauti chochote kilichoandikwa kwenye skrini)

Picha: 1. Dada akisoma chapisho la maandishi ya vipofu. 2. Dada akitumia kifaa kilicho na uwezo wa kutokeza sauti na kuandika maandishi ya vipofu.

Kutumia machapisho ya maandishi ya vipofu na kifaa cha kielektroni cha kuandika maandishi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki