HAZINA ZA NENO LA MUNGU
Mwanamke Mwovu, Aliyejitakia Makuu Aadhibiwa
Athalia aliua uzao wote wa kifalme ili atawale Yuda (2Fa 11:1; it-1 209; ona chati “‘Nyumba Yote ya Ahabu Itaangamia’—2Fa 9:8”)
Yehosheba alimficha Yehoashi, mrithi wa ufalme (2Fa 11:2, 3)
Kuhani Mkuu Yehoyada alimweka rasmi Yehoashi kuwa mfalme na kumuua Athalia mwovu, ambaye huenda ndiye mtu pekee aliyekuwa hai katika nyumba ya Ahabu (2Fa 11:12-16; it-1 209)
JAMBO LA KUTAFAKARI: Simulizi hili linaonyeshaje ukweli wa Methali 11:21 na Mhubiri 8:12, 13?