Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 11
  • Je, Wasomi Wanaamini Kuwa Yesu Aliwahi Kuishi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wasomi Wanaamini Kuwa Yesu Aliwahi Kuishi?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Habari Zinazolingana
  • 3 Jifunze Ukweli Kumhusu Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Uthibitisho wa Kwamba Yesu Kristo Aliishi Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Yesu Yeye Ni Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 11
Yesu akiwa na taji la miiba

Je, Wasomi Wanaamini Kuwa Yesu Aliwahi Kuishi?

Wasomi wana msingi imara wa kuamini kwamba Yesu aliwahi kuishi. Kuhusu marejeo ya Yesu na Wakristo wa mapema yaliyofanywa na wanahistoria wa karne ya kwanza na ya pili, kitabu Encyclopædia Britannica, Toleo la 2002, kinasema hivi: “Masimulizi hayo mbalimbali yanathibitisha kwamba zamani za kale hata wapinzani wa Ukristo hawakutilia shaka kwamba Yesu alikuwa mtu halisi. Jambo hilo lilibishaniwa kwa mara ya kwanza na bila sababu nzuri mwishoni mwa karne ya 18, katika karne ya 19, na mwanzoni mwa karne ya 20.”

Mwaka wa 2006, kitabu Jesus and Archaeology kilisema: “Hakuna msomi anayejulikana leo anayetilia shaka kwamba Myahudi aliyeitwa Yesu mwana wa Yosefu aliwahi kuishi; wengi sasa wanakubali wenyewe kwamba tunajua mambo mengi kuhusu matendo na mafundisho yake ya msingi.”

Biblia inamtaja Yesu kuwa mtu halisi. Inatoa majina ya mababu zake na watu wake wa ukoo wa karibu. (Mathayo 1:1; 13:55) Pia, inatoa majina ya watawala maarufu walioishi wakati wa Yesu. (Luka 3:1, 2) Mambo hayo yote yanawapa nafasi watafiti wachunguze usahihi wa masimulizi ya Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki