13 Nanyi mmesema, ‘Tazama! Jambo hili linachosha kama nini!’+ nanyi mmeitolea pumzi puani kwa dharau,” Yehova wa majeshi amesema. “Nanyi mmeleta kitu ambacho kimenyakuliwa, na chenye kilema, na kilicho kigonjwa;+ ndiyo, mmekileta kama zawadi. Je, naweza kukifurahia mkononi mwenu?”+ Yehova amesema.