Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matangazo
    Huduma ya Ufalme—1996 | Novemba
    • Matangazo

      ◼ Toleo la fasihi la Novemba: Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Jitihada ya pekee itafanywa kufuatia maangusho yote, tukiwa na kusudi la kuanzisha mafunzo ya Biblia nyumbani. Desemba: New World Translation pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? Januari: Kitabu chochote chenye kurasa 192 kilichotangazwa kabla ya 1984 ambacho kutaniko laweza kuwa nacho akibani kitatolewa kwa nusu bei. Vichapo ambavyo vimechapishwa kwenye karatasi isiyochakaa au kugeuka rangi havipaswi kutiwa ndani ya toleo hili lililopunguzwa bei. Makutaniko ambayo hayana ugavi wa vitabu hivyo yaweza kutoa Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya au Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani.” Februari: Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Tumia kitabu chochote cha zamani chenye kurasa 192 ulicho nacho akibani, kiwe badala.

      ◼ Makutaniko ambayo bado yana ugavi wa Habari za Ufalme trakti Na. 34 yanaweza kutia moyo watangazaji wazitoe kwa namna sawa na zile trakti nyingine, iwe ni mlango hadi mlango au mahali penginepo. Ikiruhusiwa, watangazaji wanaweza kuacha moja kwa wasiokuweko nyumbani, wakihakikisha imewekwa vizuri mahali isipoweza kuonekana na mpita-njia. Jitihada zapaswa kufanywa ili kuangusha nakala zote za ujumbe huu wenye thamani.

      ◼ Makutaniko yapaswa kuanza kuagiza 1997 Yearbook of Jehovah’s Witnesses pamoja na agizo lao la fasihi la Novemba. Kitabu-Mwaka hicho kitapatikana katika Kiarabu, Kichina, Kifaransa na Kiingereza. Hadi wakati Kitabu-Mwaka hicho kitakapopatikana na upakizi ufanywe, kitaonekana kuwa “Vinavyokuja” katika orodha ya upakizi ya kutaniko. Vitabu-Mwaka ni vifaa vya kuombwa kipekee.

      ◼ Vichapo Vinavyopatikana:

      Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1997 —Kiingereza

      Lasting Peace and Happiness—How Can You Find Them? —Kichina (Sahili)

      ◼ Vidio Kaseti Zinazopatikana:

      Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele (Buku la nne)

      —Lugha ya Ishara ya Kimarekani

      Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele—(Buku la tano)

      —Lugha ya Ishara ya Kimarekani

  • Sanduku La Swali
    Huduma ya Ufalme—1996 | Novemba
    • Sanduku La Swali

      ◼ Tunapaswa kukumbuka nini tunapoandikia barua wenye nyumba ambao hatukuweza kuwapata nyumbani?

      Kwa sababu tofauti-tofauti, tunaona ikizidi kuwa vigumu kupata watu tunapozuru nyumba zao. Watangazaji kadhaa wameona uandikaji wa barua kuwa njia yenye kutumika ya kuwafikia. Ingawa jambo hili linaweza kutokeza matokeo mazuri, kuna uhitaji wa kufikiria baadhi ya vikumbusha vinavyoweza kutusaidia kuepuka magumu fulani:

      Usitumie anwani ya Sosaiti. Kufanya hivyo kutaonyesha isivyofaa kwamba barua ilitumwa kutoka ofisi zetu, kukisababisha matatizo yasiyo ya lazima na nyakati nyingine gharama za ziada.

      Hakikisha kwamba una anwani sahihi na stampu za kutosha.

      Usiandike barua kwa “Mkazi”; tumia jina hususa.

      Usiache barua mlangoni wakati ambapo hakuna mtu nyumbani.

      Barua fupi ndizo bora zaidi. Weka ndani trakti au gazeti badala ya kujaribu kuandika ujumbe mrefu.

      Barua zilizoandikwa kwa chapa ni zenye kusomeka kwa urahisi sana nazo hupendeza.

      Barua hazihesabiwi kuwa ziara za kurudia isipokuwa umemtolea ushahidi kibinafsi mtu huyo mbeleni.

      Ikiwa unamwandikia mtu ambaye hapo kwanza alionyesha kupendezwa, unapaswa kutoa anwani au namba ya simu ili aweze kuwasiliana nawe. Eleza juu ya programu yetu ya funzo la Biblia.

      Toa mwaliko wa mikutano ya kutaniko la kwenu. Onyesha anwani na saa za mikutano.

      Usiendelee kutuma barua kwa wasiokuwako nyumbani baada ya kurudisha eneo; mtangazaji aliye na eneo hilo wakati huu ana daraka la kulihubiri.

  • Funzo la Kitabu la Kutaniko
    Huduma ya Ufalme—1996 | Novemba
    • Funzo la Kitabu la Kutaniko

      Ratiba ya mafunzo ya kutaniko katika kitabu Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!

      Kutoka: Hadi:

      Novemba 4: uku. 186, ¶1 uku. 189, ¶ 12

      Novemba 11: uku. 190, ¶13 uku. 192, ¶ 24

      Novemba 18: uku. 193, ¶25 uku. 198, ¶ 38

      Novemba 25: uku. 198, ¶1 uku. 201, ¶ 11

  • Ripoti Ya Utumishi Ya Julai
    Huduma ya Ufalme—1996 | Novemba
    • Ripoti Ya Utumishi Ya Julai

      Wast. Wast. Wast. Wast.

      Idadi ya: Saa Mag. Z. K. Maf. Bi.

      K

      Pai. Pekee 217 140.5 28.2 46.6 7.8

      Mapai. 947 82.3 13.3 23.5 4.1

      Pai. Msai. 469 62.0 10.0 13.9 2.3

      Wata. 9,097 15.4 3.3 4.7 0.9

      JUMLA 10,730 Kilele Kipya: 10,563

      _

      R

      Pai. Pekee 50 141.3 8.5 77.9 11.4

      Mapai. 497 89.8 1.8 41.8 6.1

      Pai. Msai. 504 61.0 1.0 36.5 4.7

      Wata. 2,849 27.2 0.7 15.7 2.6

      JUMLA 3,900

      _

      S

      Pai. Msai. 43 65.8 5.0 39.1 4.4

      Wata. — 17.8 2.0 11.3 1.9

      _

      T

      Pai. Pekee 112 139.4 31.3 61.3 7.8

      Mapai. 667 73.5 9.7 24.3 3.3

      Pai. Msai. 318 60.2 9.2 19.0 2.3

      Wata. 5,007 13.7 2.2 4.4 0.6

      JUMLA 6,104 Kilele Kipya

      _

      U

      Pai. Pekee 48 118.6 22.0 47.1 5.9

      Mapai. 105 75.5 12.8 28.3 4.2

      Pai. Msai. 50 63.5 8.8 24.0 4.0

      Wata. 1,379 14.3 2.6 6.0 1.2

      JUMLA 1,582

  • Mahali pa Kulala pa Mwangalizi wa Mzunguko
    Huduma ya Ufalme—1996 | Novemba
    • Mahali pa Kulala pa Mwangalizi wa Mzunguko

      Twathamini sana kazi za ndugu zetu wanaotumika katika utumishi wa wakati wote wakiwa waangalizi wasafirio, sivyo? Kadiri hali zetu zinavyoruhusu, twaweza kuwapa moja kwa moja msaada wa kimwili. Kwa mfano, mwangalizi wa mzunguko azurupo kutaniko lako, huenda ukaweza kumwandalia makao yanayofaa, milo, au msaada kwa gharama zake za usafiri. Ukarimu kama huo haukosi kuonwa na Baba yetu wa kimbingu, anayetaka watumishi wake watunzwe. (Zab. 37:25) Miaka kadhaa iliyopita ndugu mmoja aliyeweza kuandaa vyakula vyepesi pekee alialika mwangalizi asafiriye pamoja na mkeye nyumbani mwake. Wenzi hao walipotoka waende katika huduma ya utumishi ya jioni, ndugu huyo akawapa wageni wake bahasha. Ndani mlikuwa na noti (iliyotoshana na dola moja ya Marekani) iliyokuwa pamoja na taarifa hii iliyoandikwa kwa mkono: ‘Kwa kikombe cha chai, au galani ya petroli.’ Ni uthamini mzuri kama nini ulioonyeshwa katika njia hii sahili! Tungependa kuwaandalia mahali pa kulala waangalizi wetu wasafirio. Inaonekana haijawa rahisi katika maeneo mengine na hii ni sehemu tunayotaka kuangalia.—Ona Mnara wa Mlinzi, Desemba 1, 1994, kurasa 17-18, fungu la 19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki