-
“Nisikilizeni Ninapojitetea”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
SURA YA 23
“Nisikilizeni Ninapojitetea”
Paulo anaitetea kweli mbele ya umati wenye vurugu na mbele ya Sanhedrini
1, 2. Kwa nini Paulo amerudi Yerusalemu, na atakabili hali gani ngumu?
YERUSALEMU! Kwa mara nyingine tena Paulo anatembea katika barabara za jiji hilo zenye watu wengi. Jiji hilo ni la pekee katika historia ya watu wa Yehova. Wakazi wengi wa jiji hilo hujivunia historia hiyo ya pekee. Paulo anajua kwamba Wakristo wengi katika jiji hilo wanazingatia kupita kiasi historia hiyo, na si rahisi kwao kukubali njia mpya ya kumwabudu Yehova. Paulo aliamua kutembelea jiji hilo si tu kwa sababu ya uhitaji wa kimwili waliokuwa nao, bali pia uhitaji wa kiroho wa ndugu katika jiji hilo. (Mdo. 19:21) Ameazimia kabisa kulitembelea jiji hilo licha ya hatari zilizopo.
2 Paulo atakabili hali gani katika jiji la Yerusalemu? Kwanza, kuna uvumi usio wa kweli kumhusu miongoni mwa wafuasi wa Kristo. Hata hivyo, atakabili changamoto kubwa zaidi kutoka kwa adui za Kristo. Watatoa mashtaka ya uwongo dhidi ya Paulo, watampiga, na kujaribu kumuua. Yote hayo yatampa Paulo nafasi ya kujitetea. Unyenyekevu, ujasiri na imani yake katika kushughulikia hali hizo ngumu ni mfano mzuri kwa Wakristo leo. Jinsi gani? Acheni tuone.
“Wakaanza Kumtukuza Mungu” (Mdo. 21:18-20a)
3-5. (a) Paulo alihudhuria mkutano gani jijini Yerusalemu, na ni mambo gani yaliyozungumziwa? (b) Tunajifunza nini kutokana na mkutano huo wa Paulo na wazee jijini Yerusalemu?
3 Siku ya pili baada ya kufika Yerusalemu, Paulo na wenzake walienda kuwaona wazee wenye madaraka kutanikoni. Hakuna yeyote kati ya mitume anayetajwa; huenda kufikia wakati huo walienda kutumikia katika maeneo mengine. Hata hivyo, Yakobo ndugu ya Yesu bado alikuwa huko. (Gal. 2:9) Inawezekana kwamba Yakobo alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo, ambapo “wazee wote walikuwapo,” pamoja na Paulo.—Mdo. 21:18.
4 Paulo aliwasalimu wazee “na kuanza kusimulia kirefu mambo ambayo Mungu alifanya miongoni mwa mataifa kupitia huduma yake.” (Mdo. 21:19) Wazia jinsi habari hizo zilivyowatia moyo! Leo, sisi pia hufurahia ripoti za maendeleo ya kazi katika nchi nyingine.—Met. 25:25.
5 Katika mazungumzo hayo, haikosi Paulo alitaja michango aliyoleta kutoka Ulaya. Lazima ndugu hao waliokuwa wakimsikiliza Paulo waliguswa moyo sana kuona jinsi ndugu zao katika sehemu nyingine wanavyowahangaikia. Baada ya kuisikiliza ripoti ya Paulo, masimulizi yanasema: “[Wazee hao] wakaanza kumtukuza Mungu”! (Mdo. 21:20a) Leo pia, wengi ambao wamekumbwa na majanga au magonjwa huchochewa sana wakati ambapo waabudu wenzao wanatoa misaada na kuwafariji.
Bado Wengi “Wanafuata Sheria kwa Bidii” (Mdo. 21:20b, 21)
6. Paulo alijulishwa tatizo gani?
6 Kisha wazee wakamweleza Paulo kwamba kuna tatizo Yudea ambalo linamhusu. Walisema: “Ndugu, unaona jinsi ambavyo maelfu ya Wayahudi wamekuwa waamini, na wote wanafuata Sheria kwa bidii. Lakini wamesikia uvumi kukuhusu kwamba umekuwa ukiwafundisha Wayahudi wote kati ya mataifa kuiasi sheria ya Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao wala kufuata desturi zilizowekwa.”a—Mdo. 21:20b, 21.
7, 8. (a) Wakristo wengi wa Yudea walikuwa na maoni gani? (b) Kwa nini maoni yao hayakuwafanya waasi imani?
7 Miaka 20 baada ya Sheria ya Musa kuondolewa, kwa nini bado Wakristo wengi walikuwa wakiishikilia kwa bidii? (Kol. 2:14) Mwaka wa 49 W.K., mitume na wazee jijini Yerusalemu waliyatumia makutaniko barua wakieleza kwamba waamini kutoka kwa mataifa hawahitaji kutahiriwa wala kuwa chini ya Sheria ya Musa. (Mdo. 15:23-29) Hata hivyo, barua hiyo haikutaja waamini Wayahudi, ambao wengi kati yao hawakuelewa kwamba Sheria ya Musa haitumiki tena.
8 Je, kutoelewa kwa waabudu hao Wayahudi kulimaanisha kwamba hawakustahili kuendelea kuwa Wakristo? Hapana. Si kwamba walikuwa waabudu wa miungu ya kipagani awali, na sasa walikuwa wakiendeleza mapokeo ya dini zao za zamani. Sheria hiyo ambayo ilikuwa muhimu sana kwa waamini hao Wayahudi, ilitoka kwa Yehova. Sheria yenyewe haikuwa na ubaya wowote, wala haikuwa ya kikatili. Tofauti ni kwamba Sheria hiyo ilikuwa sehemu ya agano la kale, nao Wakristo walikuwa chini ya agano jipya. Kwa hiyo, ibada safi haikutegemea tena kuendelea kulishikilia agano la Sheria. Wakristo Waebrania waliokuwa wakishikilia Sheria kwa bidii hawakuelewa vizuri utendaji wa kutaniko la Kikristo. Walihitaji kupatanisha maoni yao na kweli iliyokuwa ikifunuliwa hatua kwa hatua.b—Yer. 31:31-34; Luka 22:20.
“Uvumi Walioambiwa Kukuhusu si wa Kweli” (Mdo. 21:22-26)
9. Paulo alifundisha nini kuhusu Sheria ya Musa?
9 Namna gani ule uvumi wa kwamba Paulo alikuwa akiwafundisha Wayahudi kati ya mataifa “wasiwatahiri watoto wao wala kufuata desturi zilizowekwa”? Paulo alikuwa mtume kwa Watu wa Mataifa, naye aliposhughulika nao, aliunga mkono uamuzi uliopitishwa wa kwamba Watu wa Mataifa hawahitaji kufuata matakwa ya Sheria. Pia, alifafanua kwa nini ni kosa kwa mtu yeyote kujaribu kuwalazimisha waabudu wa Mataifa watahiriwe ili tu kuonyesha kwamba wanaiheshimu Sheria ya Musa. (Gal. 5:1-7) Katika majiji aliyotembelea, Paulo aliwahubiria habari njema Wayahudi pia. Bila shaka, aliwaeleza waliokuwa tayari kumsikiliza kwamba kifo cha Yesu kiliondolea mbali Sheria na kwamba uadilifu ungepatikana kwa imani, bali si kwa kushika Sheria.—Rom. 2:28, 29; 3:21-26.
10. Paulo alionyesha usawaziko jinsi gani kuhusu Sheria na tohara?
10 Hata hivyo, Paulo alielewa hisia za wale waliokuwa wakiendelea kufuata baadhi ya desturi za Kiyahudi, kama vile kutofanya kazi siku ya Sabato au kutokula vyakula fulani. (Rom. 14:1-6) Naye hakuweka sheria kuhusu tohara. Paulo alimtahiri Timotheo ili Wayahudi wasiwe na shaka kumhusu Timotheo, ambaye baba yake alikuwa Mgiriki. (Mdo. 16:3) Suala la tohara lilikuwa la kibinafsi. Paulo aliwaambia Wagalatia: “Kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna faida yoyote, bali imani inayotenda kupitia upendo ina faida.” (Gal. 5:6) Hata hivyo, kutahiriwa ili tu kutimiza Sheria au kudai kwamba lazima mtu atahiriwe ili apate kibali cha Yehova ni kukosa imani.
11. Wazee walimwagiza Paulo afanye nini, na huenda ni nini kilichohusika? (Ona pia maelezo ya chini.)
11 Ijapokuwa uvumi uliokuwa umeenea haukuwa wa kweli, bado uliwasumbua waamini Wayahudi. Ndiyo sababu wazee walimwagiza Paulo: “Tuna wanaume wanne waliojiwekea nadhiri. Nenda pamoja na watu hawa ukajitakase kisherehe pamoja nao na kuwagharimia, ili wanyolewe vichwa vyao. Ndipo kila mtu atajua kwamba uvumi walioambiwa kukuhusu si wa kweli, bali unatembea kwa utaratibu, na pia unashika Sheria.”c—Mdo. 21:23, 24.
12. Paulo alionyeshaje kwamba alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali na kufuata maagizo ya wazee wa Yerusalemu?
12 Paulo angeweza kushikilia msimamo wake na kudai kwamba tatizo si uvumi ulioenea kumhusu, bali ni maoni ya waamini hao Wayahudi kuhusu Sheria ya Musa. Badala ya kufanya hivyo, alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali maadamu kufanya hivyo hakungevunja viwango vya Mungu. Mapema alikuwa ameandika hivi: “Kwa wale walio chini ya sheria nilikuwa kama aliye chini ya sheria, ingawa mimi mwenyewe siko chini ya sheria, ili niwapate wale walio chini ya sheria.” (1 Kor. 9:20) Katika kisa hiki, Paulo aliamua kufuata maagizo ya wazee wa Yerusalemu na kuwa “kama aliye chini ya sheria.” Kwa kufanya hivyo, alituwekea kielelezo kizuri cha kufuata maagizo ya wazee badala ya kuamua kufanya mambo kwa njia yetu.—Ebr. 13:17.
Ikiwa hakuna kanuni za Kimaandiko zilizohusika, Paulo alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali. Je, wewe hufanya hivyo?
“Hafai Kuishi!” (Mdo. 21:27–22:30)
13. (a) Kwa nini baadhi ya Wayahudi walisababisha mvurugo hekaluni? (b) Paulo aliokolewaje?
13 Mambo hayakwenda vizuri hekaluni. Kadiri siku za nadhiri zilivyokuwa zinakaribia kwisha, Wayahudi kutoka Asia walimwona Paulo, wakamshtaki kwa uwongo kwamba amewaingiza Watu wa Mataifa hekaluni, na kusababisha mvurugo. Kama kiongozi wa jeshi la Roma hangeingilia kati, Paulo angepigwa na kuuawa. Hata hivyo, kiongozi huyo akamfunga. Tangu siku hiyo, Paulo alikaa gerezani kwa zaidi ya miaka minne kabla ya kufunguliwa. Nazo hatari zilizomkabili hazikuwa zimeisha. Kiongozi alipowauliza Wayahudi kwa nini walimshambulia Paulo, umati huo ulitoa mashtaka mbalimbali. Kwa sababu kulikuwa na vurugu, kiongozi huyo hangeweza kusikia chochote. Ilibidi Paulo aondolewe hapo. Paulo na askari jeshi wa Roma walipokaribia kuingia katika makao ya askari jeshi, Paulo alimwambia kiongozi huyo: “Nakuomba uniruhusu nizungumze na watu hawa.” (Mdo. 21:39) Kiongozi alikubali, naye Paulo akaitetea imani yake kwa ujasiri.
14, 15. (a) Paulo aliwaeleza Wayahudi nini? (b) Kiongozi wa jeshi la Roma alichukua hatua gani ili kujua kwa nini Wayahudi wana hasira kali hivyo?
14 Paulo alianza kwa kusema: “Nisikilizeni ninapojitetea.” (Mdo. 22:1) Paulo alihutubia umati huo kwa Kiebrania, jambo lililowatuliza. Aliwaeleza kwa unyoofu kwa nini yeye ni mfuasi wa Kristo. Kwa ustadi, Paulo alitoa hoja ambazo Wayahudi hao wangeweza kuthibitisha ikiwa wangetaka. Paulo alikuwa amesomea miguuni pa Gamalieli, aliyejulikana sana, naye alikuwa amewanyanyasa wafuasi wa Kristo, kama vile baadhi ya watu katika umati huo wanavyojua. Hata hivyo, alipokuwa njiani kuelekea Damasko aliona maono. Katika maono hayo, Kristo aliyekuwa amefufuliwa alizungumza naye. Watu waliokuwa wakisafiri na Paulo waliona nuru nyangavu na kusikia sauti, lakini hawakuelewa maana ya maneno yaliyosemwa. (Mdo. 9:7; 22:9) Kisha, Paulo aliyekuwa amepofushwa na maono hayo, aliongozwa na wenzake hadi Damasko. Akiwa huko Anania, aliyejulikana na Wayahudi wa eneo hilo, alimponya Paulo kimuujiza.
15 Paulo alisema kwamba baada ya kurudi Yerusalemu, Yesu alimtokea tena akiwa hekaluni. Waliposikia hilo, Wayahudi wakakasirika sana na kuanza kupiga kelele wakisema: “Mwondoeni duniani mtu kama huyu, hafai kuishi!” (Mdo. 22:22) Ili kumwokoa Paulo, kiongozi wa jeshi akaagiza apelekwe ndani ya kambi ya askari jeshi. Akitaka kujua ni kwa nini Wayahudi hao wana hasira kali hivyo kumwelekea Paulo, kiongozi huyo akaamuru ahojiwe huku akipigwa mijeledi. Paulo aliamua kutumia ulinzi wa kisheria na kusema kwamba yeye ni raia wa Roma. Leo pia, waabudu wa Yehova hutumia ulinzi wa kisheria kutetea imani yao. (Ona sanduku lenye kichwa “Sheria ya Waroma na Raia wa Roma,” na “Kesi za Kisheria Katika Siku Zetu.”) Baada ya kusikia kwamba Paulo ni raia wa Roma, kiongozi huyo alihitaji kutafuta njia nyingine ya kupata habari. Siku iliyofuata, alimleta Paulo mbele ya mkutano wa pekee wa mahakama kuu ya Wayahudi inayoitwa Sanhedrini.
“Mimi Ni Farisayo” (Mdo. 23:1-10)
16, 17. (a) Eleza kilichotokea Paulo alipokuwa akijitetea mbele ya Sanhedrini. (b) Alipopigwa, Paulo alionyeshaje unyenyekevu?
16 Paulo alianza kujitetea mbele ya mahakama hiyo kwa kusema: “Wanaume, akina ndugu, nimetenda kwa dhamiri safi kabisa mbele za Mungu mpaka leo hii.” (Mdo. 23:1) Kabla hajasema zaidi, “kuhani mkuu Anania akawaagiza wale waliosimama kando yake wampige kofi mdomoni.” (Mdo. 23:2) Alimdharau sana! Tendo hilo lilionyesha chuki aliyokuwa nayo. Ni kana kwamba alisema Paulo ni mwongo hata kabla ya kumsikiliza! Si ajabu Paulo alisema: “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa. Je, unaketi kunihukumu kulingana na Sheria na wakati uleule unaivunja Sheria hiyo kwa kuamuru nipigwe?”—Mdo. 23:3.
17 Baadhi ya wale waliokuwa wamesimama hapo wakashangazwa—si na yule aliyempiga Paulo, bali na jibu la Paulo! Wakamuuliza: “Je, unamtukana kuhani mkuu wa Mungu?” Jibu la Paulo lilionyesha kwamba yeye ni mnyenyekevu na pia anaiheshimu Sheria. Alisema: “Akina ndugu, sikujua yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana imeandikwa, ‘Usiseme vibaya juu ya mtawala wa watu wako.’”d (Mdo. 23:4, 5; Kut. 22:28) Paulo akabadili njia yake. Akijua kwamba washiriki wa mahakama hiyo ni Mafarisayo na Masadukayo, akasema: “Wanaume, akina ndugu, mimi ni Farisayo, mwana wa Mafarisayo. Ninahukumiwa kwa sababu ya tumaini la ufufuo wa wafu.”—Mdo. 23:6.
Kama Paulo alivyofanya, sisi hujaribu kuweka msingi mzuri wa mazungumzo tunapozungumza na watu wenye imani tofauti
18. Kwa nini Paulo alijiita Farisayo, nasi tunaweza kufuata mfano wake jinsi gani?
18 Kwa nini Paulo anajiita Farisayo? Kwa sababu alikuwa “mwana wa Mafarisayo” kutoka katika familia ya Kifarisayo. Kwa hiyo, machoni pa wengi alionwa kuwa Farisayo.e Hata hivyo, je, imani ya Paulo kuhusu ufufuo ilikuwa sawa na ya Mafarisayo? Mafarisayo waliamini nafsi haifi, na kwamba nafsi ya waadilifu huishi tena katika miili ya binadamu. Bila shaka, Paulo hakuamini hivyo bali aliamini ufufuo uliofundishwa na Yesu. (Yoh. 5:25-29) Hata hivyo, sawa na Mafarisayo, Paulo aliamini kwamba kuna tumaini la ufufuo. Kwa upande mwingine, Masadukayo hawakuamini kuna ufufuo. Tunaweza kufuata mfano wake tunapowahubiria Wakatoliki au Waprotestanti. Tunaweza kuwaambia sisi pia tunaamini kuna Mungu. Ingawa wanaamini Utatu, sisi tunamwamini Mungu anayetajwa katika Biblia. Hivyo, sote tunaamini kwamba kuna Mungu.
19. Kwa nini kulikuwa na vurugu mahakamani?
19 Maneno ya Paulo yalitokeza mgawanyiko. Simulizi hilo linasema: “Kukawa na vurugu, na baadhi ya waandishi wa chama cha Mafarisayo wakasimama na kuanza kubishana kwa ukali, wakisema: “Hatuoni kosa lolote katika mtu huyu, lakini ikiwa roho au malaika alizungumza naye—.’” (Mdo. 23:9) Wazo la kwamba huenda Paulo alikuwa ameongea na malaika, liliwachukiza sana Masadukayo ambao hawakuamini malaika! (Ona sanduku lenye kichwa “Masadukayo na Mafarisayo.”) Vurugu hizo zilikuwa kubwa sana hivi kwamba yule kiongozi akalazimika kumwokoa tena mtume huyo. (Mdo. 23:10) Hata hivyo, bado Paulo alikuwa hatarini. Ni nini kitakachompata mtume huyo? Tutaona katika sura inayofuata.
a Ili kushughulikia mahitaji ya kiroho ya idadi kubwa ya Wakristo Wayahudi, lazima kulikuwa na makutaniko mengi yaliyokuwa yakikutana katika nyumba za watu binafsi.
b Miaka michache baadaye, mtume Paulo aliandika barua yake kwa Waebrania, ambamo alithibitisha ubora wa agano jipya. Katika barua hiyo, alionyesha wazi kwamba kuanzishwa kwa agano jipya kuliondolea mbali agano la kale. Mbali na kutoa hoja zenye kusadikisha ambazo Wakristo Wayahudi wangeweza kutumia kuwajibu Wayahudi waliowapinga, hoja za Paulo ziliimarisha imani ya baadhi ya Wakristo waliokuwa wakishikilia kupita kiasi Sheria ya Musa.—Ebr. 8:7-13.
c Wasomi fulani wanadokeza kwamba watu hao walikuwa wameweka Nadhiri. (Hes. 6:1-21) Ni kweli kwamba Sheria ya Musa, iliyotumika kuweka nadhiri hizo, haikuwa ikitumika tena. Hata hivyo, huenda Paulo aliona kwamba hakuna ubaya kwa watu hao kutimiza nadhiri waliyoweka kwa Yehova. Kwa hiyo, haingekuwa vibaya kulipa gharama zao na kuandamana nao. Hatujui ni nadhiri ya aina gani iliyowekwa, hata hivyo, haielekei kwamba Paulo angeshiriki kutoa dhabihu ya mnyama (kama Wanadhiri walivyofanya), akiamini kwamba ingesafisha dhambi za mtu. Dhabihu kamilifu ya Kristo ilikuwa imeondolea mbali uwezo wa dhabihu hizo kusafisha dhambi. Vyovyote vile, tuna hakika kwamba Paulo hangekubali kufanya chochote ambacho kingechafua dhamiri yake.
d Watu fulani wamesema kwamba inawezekana Paulo hakuwa akiona vizuri kwa hiyo hakumtambua kuhani mkuu. Au huenda alikuwa mbali na Yerusalemu kwa muda mrefu sana hivi kwamba hakumjua kuhani mkuu wa wakati huo. Au kwa sababu ya umati wa watu uliokuwapo labda Paulo hangeweza kuona ni nani aliyetoa amri apigwe.
e Mwaka wa 49 W.K., mitume na wazee walipokuwa wakijadiliana ikiwa Watu wa Mataifa wanapaswa kushika Sheria ya Musa, baadhi ya Wakristo waliokuwako waliitwa “baadhi ya wale wa madhehebu ya Mafarisayo ambao sasa walikuwa waamini.” (Mdo. 15:5) Inaonekana kwa kiasi fulani waamini hao walikuwa bado wakihusianishwa na asili yao ya Kifarisayo.

“Jipe Moyo!”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
SURA YA 24
“Jipe Moyo!”
Paulo anusurika kifo na anajitetea mbele ya Feliksi
1, 2. Kwa nini Paulo hashangazwi na mateso anayokabili jijini Yerusalemu?
BAADA ya kuokolewa kutoka kwenye umati wenye hasira kali jijini Yerusalemu, Paulo awekwa kizuizini tena. Mateso anayokabili katika jiji la Yerusalemu hayamshangazi mtume huyo mwenye bidii. Aliambiwa atazamie ‘kufungwa gerezani na kupatwa na dhiki’ katika jiji hilo. (Mdo. 20:22, 23) Ijapokuwa Paulo hajui kitakachompata, anajua kwamba atateseka kwa ajili ya jina la Yesu.—Mdo. 9:16.
2 Hata manabii Wakristo walimwonya Paulo kwamba atafungwa na kutiwa “mikononi mwa watu wa mataifa.” (Mdo. 21:4, 10, 11) Siku chache zilizotangulia, umati wa Wayahudi ulijaribu kumuua, na muda mfupi baadaye, washiriki wa Sanhedrini karibu ‘wangemrarua-rarua’ walipokuwa wakibishana kwa sababu ya mambo aliyosema. Sasa mtume huyo ni mfungwa chini ya ulinzi wa askari jeshi Waroma, akikabili kesi na mashtaka mengi. (Mdo. 21:31; 23:10) Bila shaka, mtume Paulo anahitaji kutiwa moyo!
3. Sisi hutiwa moyo jinsi gani kuendelea kuhubiri?
3 Katika siku hizi za mwisho, tunajua kwamba “wote wanaotamani kuishi kwa ujitoaji-kimungu katika ushirika na Kristo Yesu watateswa pia.” (2 Tim. 3:12) Mara kwa mara, sisi pia tunahitaji kutiwa moyo ili tuendelee katika kazi yetu ya kuhubiri. Tunathamini sana maneno yenye kutia moyo na yenye kufariji tunayopata kwa wakati unaofaa, kupitia machapisho na mikutano inayotayarishwa na “mtumwa mwaminifu na mwenye busara”! (Mt. 24:45) Yehova ametuhakikishia kwamba hakuna adui wa habari njema atakayefanikiwa. Hawawezi kuwaangamiza watumishi wake wakiwa kikundi wala kukomesha kazi yao ya kuhubiri. (Isa. 54:17; Yer. 1:19) Namna gani mtume Paulo? Je, alitiwa moyo kuendelea kutoa ushahidi kamili licha ya upinzani? Ikiwa ndivyo, alitiwa moyo jinsi gani, naye alifanya nini?
‘Hila Iliyofungwa kwa Kiapo’ Yazimwa (Mdo. 23:11-34)
4, 5. Paulo alitiwa moyo jinsi gani, na kwa nini alitiwa moyo kwa wakati unaofaa?
4 Mtume Paulo alitiwa moyo sana usiku uliofuata, baada ya kuokolewa kutoka kwa Sanhedrini. Masimulizi yaliyoongozwa na roho yanasema: “Bwana akasimama kando yake na kumwambia: ‘Jipe moyo! Kwa maana kama vile ambavyo umekuwa ukitoa ushahidi kamili kunihusu katika Yerusalemu, ndivyo utakavyotoa ushahidi huko Roma pia.’” (Mdo. 23:11) Maneno hayo ya Yesu yanayotia moyo yalimhakikishia Paulo kwamba atakombolewa. Alijua kwamba atafika Roma na kutoa ushahidi kumhusu Yesu.
“Wanaume zaidi ya 40 kati yao walio tayari kumvizia.”—Matendo 23:21
5 Paulo alitiwa moyo kwa wakati unaofaa. Siku iliyofuata, wanaume Wayahudi zaidi ya 40, “wakafanya hila na kujifunga kwa kiapo cha laana, wakisema hawatakula wala kunywa mpaka watakapomuua Paulo.” ‘Hila iliyofungwa kwa kiapo,’ ilionyesha jinsi Wayahudi hao walivyoazimia kabisa kumuua mtume huyo. Waliamini kwamba, ikiwa hawangefanikiwa katika hila yao, basi wangestahili kulaaniwa, au kupatwa na mabaya. (Mdo. 23:12-15) Wakiwa na kibali cha wakuu wa makuhani na wazee, walipanga Paulo arudishwe mbele ya mahakama ya Sanhedrini ili kujibu maswali zaidi, kana kwamba kuna mambo yanayomhusu ambayo wanataka kuhakikisha. Hata hivyo, lengo lao lilikuwa kumvizia Paulo akiwa njiani na kumuua.
6. Njama ya kumuua Paulo ilifunuliwaje, na vijana wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa mpwa wa Paulo?
6 Hata hivyo, mpwa wa Paulo alipata habari kuhusu njama hiyo, naye akamjulisha Paulo. Kisha, Paulo akamwagiza kijana huyo amwambie Klaudio Lisia, kiongozi wa jeshi la Roma. (Mdo. 23:16-22) Bila shaka, Yehova anawapenda vijana ambao, kama mpwa huyo wa Paulo, hutanguliza kwa ujasiri hali njema ya watu wa Mungu na kufanya kwa uaminifu yote wawezayo ili kuendeleza kazi ya Ufalme.
7, 8. Klaudio Lisia alifanya nini ili kuhakikisha usalama wa Paulo?
7 Mara tu baada ya kuambiwa kuhusu njama iliyopangwa dhidi ya Paulo, Klaudio Lisia, aliyekuwa akisimamia askari 1,000, akaamuru kikosi cha askari 470—askari jeshi, wenye mikuki, na wapanda farasi—kiende Yerusalemu usiku huo na kumsindikiza Paulo mpaka Kaisaria. Akiwa huko alipaswa kufikishwa mbele ya Gavana Feliksi.a Jiji la Kaisaria lilikuwa kituo cha serikali ya Roma katika mkoa wa Yudea. Kulikuwa na Wayahudi wengi, lakini wakaaji wengi zaidi walikuwa Watu wa Mataifa. Mkoa huo ulikuwa tofauti kabisa na Yerusalemu, ambako watu wengi walionyesha chuki ya kidini na kusababisha ghasia. Kaisaria lilikuwa pia makao makuu ya majeshi ya Roma katika mkoa wa Yudea.
8 Kupatana na sheria za Roma, Lisia alimtumia Feliksi barua kumweleza mashtaka yaliyotolewa. Lisia alitaja kwamba alipojua Paulo ni raia wa Roma, alimwokoa ili ‘asiuawe’ na Wayahudi. Lisia alisema kwamba hakumpata Paulo na hatia yoyote ya ‘kustahili kifo au kufungwa gerezani,’ lakini kwa sababu ya hila iliyopangwa dhidi ya Paulo, alimtuma kwa Feliksi ili awasikilize wanaomshtaki na kutoa hukumu.—Mdo. 23:25-30.
9. (a) Haki za Paulo akiwa raia wa Roma zilikiukwa jinsi gani? (b) Kwa nini huenda tukahitaji kutumia haki zetu tukiwa raia wa nchi?
9 Je, mambo yote ambayo Lisia aliandika yalikuwa kweli? Hapana. Inaonekana alikuwa anajitafutia sifa. Ukweli ni kwamba hakumwokoa Paulo kwa kuwa alijua kwamba mtume huyo ni raia wa Roma. Isitoshe, Lisia hakutaja kwamba alikuwa ameamuru Paulo “afungwe kwa minyororo miwili” na baadaye alitoa amri Paulo “ahojiwe huku akipigwa mijeledi.” (Mdo. 21:30-34; 22:24-29) Lisia alikuwa amekiuka haki za Paulo akiwa raia wa Roma. Leo, Shetani hutumia wapinzani wa kidini kuchochea mateso, na huenda uhuru wetu wa ibada ukavurugwa. Hata hivyo, kama Paulo alivyofanya, watu wa Mungu wanaweza kutumia haki zao wakiwa raia wa nchi ili kutafuta ulinzi wa kisheria.
“Nami Nafurahi Kujitetea Mbele Yako” (Mdo. 23:35–24:21)
10. Paulo alishtakiwa mambo gani mazito?
10 Akiwa Kaisaria, Paulo ‘aliwekwa chini ya ulinzi katika jumba la kifalme la Herode’ akingojea waliomshtaki wafike kutoka Yerusalemu. (Mdo. 23:35) Siku tano baadaye, wakafika—Kuhani Mkuu Anania, wakili anayeitwa Tertulo, na kikundi cha wazee. Tertulo alianza kwa kumsifu Feliksi kwa mambo aliyokuwa akiwafanyia Wayahudi, huenda ili apate kibali chake.b Kisha, akianza mashtaka yake, Tertulo alisema kwamba Paulo ni “msumbufu, akichochea uasi miongoni mwa Wayahudi wote katika dunia yote inayokaliwa, naye ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazareti. Pia alijaribu kulichafua hekalu, basi tukamkamata.” Wale Wayahudi wengine “wakajiunga katika shambulio hilo, wakisisitiza kwamba mambo hayo ni ya kweli.” (Mdo. 24:5, 6, 9) Kuchochea uasi, kuongoza madhehebu hatari, na kulichafua hekalu—hayo yalikuwa mashtaka mazito ambayo yangeweza kufanya mtu ahukumiwe kifo.
11, 12. Paulo alikanushaje mashtaka yaliyoletwa dhidi yake?
11 Kisha, Paulo akaruhusiwa azungumze. Akasema hivi: “Nami nafurahi kujitetea mbele yako.” Kisha, akakanusha mashtaka hayo. Mtume huyo hakuwa amelichafua hekalu, wala kujaribu kuchochea uasi. Alisema kwamba hata hakuwa Yerusalemu kwa “miaka kadhaa” na kwamba alikuwa amefika kuleta “zawadi za rehema”—michango kwa ajili ya Wakristo ambao walikuwa maskini kwa sababu ya njaa na mateso. Paulo alisisitiza kwamba kabla ya kuingia hekaluni, alikuwa ‘ametakaswa kisherehe’ naye aliazimia “kudumisha dhamiri safi mbele za Mungu na wanadamu.”—Mdo. 24:10-13, 16-18.
12 Paulo alikiri kwamba alikuwa akitoa utumishi mtakatifu kwa Mungu wa mababu zake “kulingana na njia wanayoiita madhehebu.” Hata hivyo, alisisitiza kwamba anaamini “mambo yote yaliyo katika Sheria na yaliyoandikwa katika Manabii.” Na kama washtaki wake, alikuwa na tumaini la “ufufuo wa waadilifu na wasio waadilifu pia.” Kisha, Paulo akawataka washtaki wake watoe uthibitisho wa madai yao: “Uwaambie watu walio hapa waseme wenyewe kosa walilopata nilipokuwa nimesimama mbele ya Sanhedrini, isipokuwa jambo hili moja nililosema kwa sauti kubwa nilipokuwa nimesimama kati yao: ‘Mimi ninahukumiwa leo mbele yenu kwa sababu ya ufufuo wa wafu!’”—Mdo. 24:14, 15, 20, 21.
13-15. Ni kwa njia gani Paulo alituwekea mfano mzuri wa kutoa ushahidi kwa ujasiri tunaposhtakiwa?
13 Paulo alituwekea mfano mzuri tunaoweza kufuata ikiwa tutashtakiwa kwa sababu ya ibada yetu na tukishtakiwa kuwa wachochezi, waasi, au washiriki wa “madhehebu hatari.” Paulo hakujaribu kujipendekeza mbele ya gavana, akimsifu kama alivyofanya Tertulo. Paulo alikuwa mtulivu na mwenye heshima. Kwa busara, alitoa ushahidi wenye kusadikisha na wa kweli. Paulo alitaja kwamba “Wayahudi fulani kutoka mkoa wa Asia” waliodai kwamba alichafua hekalu hawako, na kulingana na sheria wanapaswa kuwapo ili wathibitishe mashtaka yao.—Mdo. 24:18, 19.
14 Zaidi ya yote, Paulo hakuogopa kutoa ushahidi kuhusu imani yake. Kwa ujasiri mtume alitaja tena na tena imani yake katika ufufuo, suala ambalo lilisababisha vurugu alipokuwa mbele ya Sanhedrini. (Mdo. 23:6-10) Alipokuwa akijitetea, Paulo alikazia tumaini la ufufuo. Kwa nini? Kwa sababu Paulo alikuwa akitoa ushahidi kumhusu Yesu na ufufuo wake—jambo ambalo wapinzani hao hawakukubali. (Mdo. 26:6-8, 22, 23) Vurugu zilizotokea zilitokana na suala la ufufuo, imani katika Yesu na ufufuo wake.
15 Kama Paulo alivyofanya, tunaweza kutoa ushahidi kwa ujasiri, nasi tunaweza kutiwa moyo na maneno ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Mtachukiwa na watu wote kwa sababu ya jina langu. Lakini yule atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.” Je, tunapaswa kuhangaikia tutakalosema? Hapana, kwa kuwa Yesu alitoa uhakikisho huu: “Watakapokuwa wakiwapeleka kuwashtaki, msihangaike kuhusu jambo mtakalosema; bali semeni jambo mtakalopewa saa hiyo, kwa maana si ninyi mnaosema, bali ni roho takatifu.”—Marko 13:9-13.
“Feliksi Akaogopa” (Mdo. 24:22-27)
16, 17. (a) Feliksi alishughulikia jinsi gani kesi ya Paulo? (b) Huenda ni kwa nini Feliksi aliogopa, hata hivyo ni kwa nini aliendelea kukutana na Paulo?
16 Hiyo haikuwa mara ya kwanza Gavana Feliksi kusikia kuhusu imani ya Kikristo. Masimulizi hayo yanasema: “Feliksi, akiwa anajua vizuri ukweli kuhusu Njia hii [jina lililotumiwa kufafanua Ukristo wa mapema], akaahirisha kesi yao kwa kusema: ‘Lisia kamanda wa jeshi atakapokuja, nitaamua mambo haya yanayowahusu.’ Naye akamwagiza ofisa wa jeshi kwamba mtu huyo awekwe chini ya kizuizi lakini apewe uhuru fulani, na watu wake waruhusiwe kumhudumia.”—Mdo. 24:22, 23.
17 Siku kadhaa baadaye, Feliksi na mke wake Myahudi, Drusila, waliwatuma watu wamwite Paulo ili ‘wamsikilize akizungumza kuhusu imani katika Kristo Yesu.’ (Mdo. 24:24) Hata hivyo, Paulo alipozungumzia “uadilifu na kujizuia na hukumu itakayokuja, Feliksi akaogopa,” huenda kwa sababu dhamiri yake ilimsumbua kwa kuwa alijua anaishi maisha mapotovu. Kwa hiyo akamruhusu Paulo aondoke na kumwambia: “Kwa sasa unaweza kwenda, lakini nitakapopata nafasi nitakuita tena.” Baada ya hapo Feliksi alikutana na Paulo mara nyingi, si kwa sababu alitaka kujua kweli, lakini kwa sababu alitumaini kwamba Paulo atampa rushwa.—Mdo. 24:25, 26.
18. Kwa nini Paulo alizungumza na Feliksi na mke wake kuhusu “uadilifu na kujizuia na hukumu itakayokuja”?
18 Kwa nini Paulo alizungumza na Feliksi na mke wake kuhusu “uadilifu na kujizuia na hukumu itakayokuja”? Kumbuka, walitaka kujua “imani katika Kristo Yesu” inahusisha nini. Kwa kuwa Paulo alijua kwamba walikuwa wakiishi maisha mapotovu, walikuwa wakatili, na wasiotenda haki, aliwaonyesha wazi kinachohitajika ili kuwa wafuasi wa Yesu. Mambo ambayo Paulo alisema yalionyesha tofauti kubwa kati ya viwango vya Mungu vya uadilifu na mwenendo wa Feliksi na mke wake. Hayo yangewasaidia kuona kwamba wanadamu wote wanawajibika mbele ya Mungu kuhusu wanavyofikiri, kusema, na kutenda na kwamba jambo muhimu zaidi kuliko hukumu ambayo Paulo anakabili ni hukumu watakayokabili mbele za Mungu. Ndiyo sababu Feliksi ‘aliogopa’!
19, 20. (a) Tunapohubiri, tunapaswa kushughulika jinsi gani na watu wanaoonekana kana kwamba wanapendezwa na kweli, lakini wana sababu za kibinafsi? (b) Tunajuaje kwamba Feliksi hakuwa rafiki ya Paulo?
19 Tunapohubiri, huenda tukawapata watu walio kama Feliksi. Mwanzoni wanaweza kuonekana wanapendezwa na kweli, lakini labda wakawa na sababu za kibinafsi. Tunapaswa kuwa waangalifu tunaposhughulika nao. Hata hivyo, kama Paulo alivyofanya, tunaweza kutumia busara kuwaambia kuhusu viwango vya Mungu vya uadilifu. Huenda kweli ikagusa mioyo yao. Lakini, tukiona wazi kwamba hawana nia ya kuacha njia zao mbaya, tunawaacha na kutafuta wale wanaoitafuta sana kweli.
20 Nia ya Feliksi inaonekana wazi kutokana na maneno haya: “Miaka miwili ilipokwisha, Porkio Festo alichukua nafasi ya Feliksi; na kwa sababu Feliksi alitamani kukubaliwa na Wayahudi, akamwacha Paulo akiwa amefungwa.” (Mdo. 24:27) Feliksi hakuwa rafiki wa kweli wa Paulo. Feliksi alijua kwamba wafuasi wa “Ile Njia” hawakuwa wachochezi wala wafanya mapinduzi. (Mdo. 19:23) Pia, alijua kwamba Paulo hakuwa amevunja sheria yoyote ya Roma. Hata hivyo, Feliksi alimtia mtume huyo kifungoni ili ‘akubaliwe na Wayahudi.’
21. Ni nini kilichompata Paulo baada ya Porkio Festo kuwa gavana, na ni nini kilichoendelea kumwimarisha Paulo?
21 Kama tunavyoona katika mstari wa mwisho wa Matendo sura ya 24, bado Paulo alikuwa gerezani Porkio Festo alipoanza kutawala baada ya Feliksi. Kukawa na mfululizo wa kesi, naye Paulo akapelekwa kutoka kwa ofisa mmoja hadi mwingine. Kwa kweli, mtume huyo mwenye ujasiri ‘alipelekwa mbele ya wafalme na magavana.’ (Luka 21:12) Kama tutakavyoona, baadaye alitoa ushahidi mbele ya mtawala mwenye nguvu zaidi wa siku zake. Wakati wote huo, imani ya Paulo haikuyumba kamwe. Bila shaka, aliendelea kuimarishwa na maneno ya Yesu: “Jipe moyo!”
a Ona sanduku lenye kichwa, “Feliksi—Gavana wa Mkoa wa Yudea.”
b Tertulo alimshukuru Feliksi kwa “amani nyingi” aliyoileta katika taifa hilo. Hata hivyo, ukweli ni kwamba amani iliyokuwa Yudea Feliksi akiwa gavana, ilikuwa ndogo ukilinganisha na amani nyingi iliyokuwako wakati wa wale magavana wengine waliotangulia mpaka uasi dhidi ya Roma ulipotokea. Pia, hakusema kweli alipotaja kwamba Wayahudi walitoa “shukrani nyingi sana” kwa marekebisho ambayo Feliksi alikuwa amefanya. Ukweli ni kwamba Wayahudi wengi walimchukia Feliksi kwa sababu ya kuwakandamiza na kuwatendea kikatili walipoasi.—Mdo. 24:2, 3.
-