Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 33

      Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya

      Njozi ya 11—Ufunuo 17:1-18

      Habari: Babuloni Mkubwa apanda hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye mwishowe amgeukia na kumteketeza

      Wakati wa utimizo: Kuanzia 1919 hadi dhiki kubwa

      1. Mmoja wa malaika saba anafunulia Yohana nini?

      KASIRANI ya Yehova ya uadilifu lazima imiminwe mpaka utimilifu, mabakuli saba yayo! Malaika wa sita alipomimina bakuli lake katika kata ya Babuloni wa kale, ilifananisha kwa kufaa tauni kwa Babuloni Mkubwa huku matukio yakienda kasi kuelekea vita ya mwisho kabisa ya Har–Magedoni. (Ufunuo 16:1, 12, 16) Yaelekea, malaika uyu huyu ndiye anayefunua sasa ni kwa nini na jinsi gani Yehova anatekeleza hukumu zake za uadilifu. Yohana anapatwa na mshangao kwa sababu ya anachofuata kusikia na kuona: “Na mmoja wa wale malaika saba ambao walikuwa na mabakuli saba akaja na kunena na mimi, kusema: ‘Njoo, mimi nitaonyesha wewe hukumu juu ya kahaba mkubwa ambaye huketi juu ya maji mengi, ambaye wafalme wa dunia walifanya uasherati na yeye, huku wale ambao huikaa dunia walifanywa kulewa divai ya uasherati wake.’”—Ufunuo 17:1, 2, NW.

      2. Kuna ithibati gani kwamba “kahaba mkubwa” (a) si Roma ya kale? (b) si biashara kubwa-kubwa? (c) ni dini?

      2 “Kahaba mkubwa”! Kwa nini jina lenye kugutusha hivyo? Yeye ni nani? Wengine wametambulisha kahaba huyu wa ufananisho kuwa Roma ya kale. Lakini Roma ilikuwa mamlaka ya kisiasa. Kahaba huyu hufanya uasherati na wafalme wa dunia, kwa wazi kutia ndani wafalme wa Roma. Mbali na hilo, baada ya kuharibiwa kwake, “wafalme wa dunia,” husemekana kuombolezea kufa kwake. Hivyo, yeye hawezi kuwa mamlaka ya kisiasa. (Ufunuo 18:9, 10) Kwa kuongezea, kwa kuwa anaombolezewa pia na wafanya biashara wa ulimwengu, yeye hawezi kufananisha biashara kubwa-kubwa. (Ufunuo 18:15, 16) Hata hivyo, sisi tunasoma kwamba, ‘kwa mazoea yake ya uwasiliano na roho mataifa yote yaliongozwa vibaya.’ (Ufunuo 18:23, NW) Hilo linafanya iwe wazi kwamba huyu kahaba mkubwa lazima awe dini ya ulimwenguni pote.

      3. (a) Kwa nini kahaba mkubwa lazima afananishe zaidi ya Kanisa Katoliki la Roma, au hata Jumuiya ya Wakristo yote? (b) Ni mafundisho gani ya Kibabuloni yanayopatikana katika dini nyingi za Mashariki na pia katika mafarakano ya Jumuiya ya Wakristo? (c) John Henry Newman kardinali Mkatoliki alikiri nini juu ya asili ya mafundisho, sherehe na mazoea mengi ya Jumuiya ya Wakristo? (Ona kielezi cha chini.)

      3 Dini ipi? Je! yeye ni Kanisa Katoliki la Roma, kama vile wengine wameshikilia? Au je! yeye ni Jumuiya ya Wakristo yote? Hapana, lazima yeye awe mpana hata zaidi ya hizi ikiwa yeye ataongoza vibaya mataifa yote. Kwa hakika yeye ni milki ya ulimwengu mzima wote ya dini bandia. Chanzo chake katika mafumbo ya Babuloni huonyeshwa kwa njia ya kwamba mengi ya mafundisho na mazoea ya Kibabuloni ni mambo ya kawaida ya dini nyingi kotekote duniani. Mathalani, itikadi ya kwamba nafsi ya kibinadamu ina kutokufa, moto wa mateso, na utatu wa miungu itapatikana katika dini nyingi za Mashariki pamoja na katika mafarakano ya Jumuiya ya Wakristo. Dini bandia, iliyoanguliwa miaka zaidi ya 4,000 iliyopita katika jiji la kale la Babuloni, imesitawi ikawa dubwana la ki-siku-hizi, ambalo kwa kufaa huitwa, Babuloni Mkubwa.a Ingawa hivyo, sababu gani anaelezwa kwa usemi usiopendeza “kahaba mkubwa”?

      4. (a) Ni katika njia zipi Israeli wa kale alifanya uasherati? (b) Ni katika njia gani ya kutokeza Babuloni Mkubwa amefanya uasherati?

      4 Babuloni (au Babeli, kumaanisha “Mvurugo”) lilifikia kilele chalo cha ukubwa wakati wa Nebukadneza. Lilikuwa dola la dini-siasa lenye mahekalu na vikanisa zaidi ya elfu moja. Ukuhani walo ulitumia nguvu kubwa. Ingawa muda mrefu tangu hapo Babuloni limeacha kuwa serikali ya ulimwengu, Babuloni Mkubwa wa kidini huendelea kuwapo, na kwa kufuata kigezo cha kale, yeye angali anatafuta kuvuta na kuunda mambo ya kisiasa. Lakini je! Mungu anatoa idhini ya dini kuwa katika siasa? Katika Maandiko ya Kiebrania, Israeli alisemwa kuwa alifanya ukahaba wakati alipojihusisha katika ibada bandia na wakati badala ya kuitibari katika Yehova, alifanya mafungamano na mataifa. (Yeremia 3:6, 8, 9; Ezekieli 16:28-30) Babuloni Mkubwa pia hufanya uasherati. Kwa kutokeza, yeye amefanya lolote analoona linafaa ili kupata uvutano na mamlaka juu ya wafalme wa dunia wenye kutawala.—1 Timotheo 4:1.

      5. (a) Viongozi wa kidini hufurahia umashuhuri gani? (b) Kwa nini kutamani umashuhuri wa kilimwengu kunapingana moja kwa moja na maneno ya Yesu Kristo?

      5 Leo, mara nyingi viongozi wa kidini hugombea cheo cha juu katika serikali, na katika mabara fulani, wanashiriki katika serikali, hata wakishikilia vyeo katika bunge. Katika 1988 viongozi wa kidini wa Kiprotestanti wawili wenye kujulikana sana waligombea cheo cha rais wa United States. Viongozi katika Babuloni Mkubwa hupenda umashuhuri; foto zao mara nyingi zitaonekana katika nyusipepa za umma wanapofuatana na wanasiasa mashuhuri. Kwa kutofautiana, Yesu aliepuka kujihusisha katika siasa na akasema hivi kwa habari ya wanafunzi wake: “Wao si sehemu ya ulimwengu, kama vile mimi si sehemu ya ulimwengu.”—Yohana 6:15; 17:16, NW; Mathayo 4:8-10; ona pia Yakobo 4:4.

      ‘Ukahaba’ wa Ki-Siku-Hizi

      6, 7. (a) Chama cha Nazi cha Hitla kilipataje mamlaka katika Ujeremani? (b) Itifaki ambayo Vatikani ilifanya pamoja na Ujeremani ya Nazi ilisaidiaje Hitla katika jitihada yake kubwa ya kutawala ulimwengu?

      6 Kupitia udukizi wake katika siasa, huyu kahaba mkubwa ameletea aina ya binadamu huzuni isiyoelezeka. Mathalani, fikiria mambo ya hakika yaliyomwezesha Hitla kuinuka kwenye mamlaka katika Ujeremani—mambo ya hakika yenye kuchukiza sana ambayo baadhi ya watu wangependa kuyafuta kutoka katika vitabu vya historia. Katika Mei 1924 Chama cha Nazi kilishikilia viti 32 katika Bunge la Ujeremani. Kufikia Mei 1928 vilikuwa vimepungua vikawa viti 12. Lakini, ule Mshuko Mkubwa wa Thamani ya Pesa ukagharikisha ulimwengu katika 1930; kufuata huo, Wanazi walipata nafuu yenye kutokeza, wakijipatia viti 230 kati ya 608 katika machaguzi ya Ujeremani ya Julai 1932. Hivyo, wakawa chama kikubwa zaidi ya vyote katika Bunge. Upesi baadaye, Franz von Papen, Mheshimiwa Kipapa, aliyekuwa Chansela hapo kwanza, akaja kusaidia Wanazi. Kulingana na wanahistoria, von Papen alikuwa na njozi ya Milki Takatifu ya Kiroma mpya. Muda wake mwenyewe mfupi wa kuwa Chansela ulikuwa umekuwa usiofanikiwa, hivyo sasa yeye alitumainia kujipatia mamlaka kupitia Wanazi. Kufikia Januari 1933, yeye alikuwa amepata uungaji-mkono kwa ajili ya Hitla kutoka kwa wenye viwanda, na kwa njama za hila yeye alihakikisha kwamba Hitla amekuwa Chansela wa Ujeremani katika Januari 30, 1933. Yeye mwenyewe alifanywa makamu wa Chansela na yeye alitumiwa na Hitla apate uungaji-mkono wa sehemu za Kikatoliki za Ujeremani. Kwa muda wa miezi miwili ya kujipatia mamlaka, Hitla alivunja bunge, akapeleka maelfu ya viongozi wapinzani kwenye kambi za mateso, na akaanza kampeni iliyo wazi ya kuwaonea Wayahudi.

      7 Katika Julai 20, 1933, upendezi wa Vatikani katika mamlaka iliyokuwa ikiinuka ya Unazi ulionyeshwa wakati Kardinali Pacelli (ambaye baadaye akawa Papa Pius 12) alipotia sahihi itifaki katika Roma kati ya Vatikani na Ujeremani ya Nazi. Von Papen alitia sahihi hati hiyo akiwa mwakilishi wa Hitla, na huko huko Pacelli akampa von Papen medali ya juu ya kipapa ya Msalaba Mtukufu wa Daraja la Pius.b Katika kitabu chake Satan in Top Hat, Tibor Koeves huandika juu ya hili, akitaarifu: “Itifaki ilikuwa ushindi mkubwa kwa ajili ya Hitla. Ilimpa uungaji-mkono wa kwanza wa kiadili aliokuwa amepokea kutoka ulimwengu wa nje, na huo kutoka chimbuko lililokwezwa zaidi sana.” Itifaki hiyo ilitaka Vatikani iondoe uungaji-mkono wayo kutoka kwa Chama cha Kati cha Kikatoliki, na hivyo kuidhinisha “serikali jumla” ya Hitla ya chama kimoja.c Zaidi, sehemu ya 14 yayo ilisema: “Uwekwaji rasmi wa maaskofu wakuu, maaskofu, na wengine kama hao utatolewa baada tu ya gavana, aliyewekwa na Serikali, kuhakikisha kabisa kwamba hakuna shaka lolote kwa habari ya mafikirio ya ujumla ya kisiasa.” Kufikia mwisho wa 1933 (uliotangazwa na Papa Pius 11 kuwa “Mwaka Mtakatifu”), uungaji-mkono wa Vatikani ulikuwa umekuwa umechangia sana jitihada kubwa ya Hitla kwa ajili ya utawala wa ulimwengu.

      8, 9. (a) Vatikani na pia Kanisa Katoliki na viongozi wa kidini wayo walitendaje katika kuitikia ukatili wa Nazi? (b) Ni taarifa gani ambayo Maaskofu Wakatoliki wa Ujeremani walitoa mwanzoni mwa Vita ya Ulimwengu 2? (c) Mahusiano ya dini-siasa yamekuwa na matokeo gani?

      8 Ingawa mapadri na watawa wa kike wachache waliteta dhidi ya matendo ya ubahaimu ya Hitla—na wakapata mateso kwa kufanya hivyo—Vatikani pamoja na Kanisa Katoliki na jeshi layo la viongozi wa kidini waliunga mkono ukatili wa Nazi ama kwa vitendo au kwa kutoteta, waliuona kuwa kinga dhidi ya kusonga mbele kwa Ukomunisti wa ulimwengu. Akijikalia kitako katika Vatikani, Papa Pius 12 aliachilia Uharibifu Mkubwa wa Wayahudi na unyanyaso wa ukatili juu ya Mashahidi wa Yehova na wengine uendelee bila kuchambuliwa. Ni kinyume kwamba Papa John Paul 2, alipozuru Ujeremani katika Mei 1987, alipaswa kutukuza msimamo wa padri mmoja mwenye moyo mweupe wa kupinga Unazi. Yale maelfu mengine ya viongozi wa kidini wa Ujeremani walikuwa wakifanya nini wakati wa utawala wa kuogofya wa Hitla? Barua moja ya uchungaji iliyotolewa na maaskofu wa Ukatoliki wa Ujeremani katika Septemba 1939 ilipotokea Vita ya Ulimwengu 2, inatoa nuru juu ya jambo hili. Kwa sehemu inasomwa hivi: “Katika saa hii ya kukata maneno sisi twashauri askari-jeshi Wakatoliki kufanya wajibu wao katika utii kwa Fuehrer na kuwa tayari kudhabihu nafsi nzima yao. Sisi tunasihi Waaminifu wajiunge katika sala zenye idili kwamba huu Mwongozo wa Kimungu uweze kupeleka vita hii kwenye ufanisi wenye baraka.”

      9 Ubalozi huu wa Katoliki unatoa kielezi cha namna ya ukahaba ambao dini imejitia ndani yao katika miaka zaidi ya 4,000 iliyopita katika kubembeleza Serikali ya kisiasa ili kupata mamlaka na faida. Mahusiano kama hayo ya dini-siasa yamesitawisha vita, minyanyaso, na taabu kwa aina ya binadamu kwa kadiri kubwa mno. Jinsi aina ya binadamu inavyoweza kuwa na furaha kwamba hukumu ya Yehova juu ya huyu kahaba mkubwa imekaribia karibu! Na itekelezwe upesi!

      Kuketi Juu ya Maji Mengi

      10. Ni “maji mengi” gani ambayo Babuloni Mkubwa hutegemea kuwa himaya, na yanapatwa na nini?

      10 Babuloni wa kale aliketi juu ya maji mengi—Mto Eufrati na mifereji mingi. Haya yalikuwa himaya yake pamoja na chimbuko la biashara iliyotokeza utajiri, mpaka yalipokaushwa usiku mmoja. (Yeremia 50:38; 51:9, 12, 13) Babuloni Mkubwa pia hutegemea “maji mengi” yampe himaya na kumtajirisha. Maji haya ya ufananisho ni “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi,” yaani, maelfu ya mamilioni yote ya binadamu ambao juu yao yeye ametawala na ambao kutoka kwao yeye amechota msaada wa vitu vya kimwili. Lakini maji haya ya ufananisho yanakauka pia, au kuondoa msaada.—Ufunuo 17:15, NW; linga Zaburi 18:4; Isaya 8:7.

      11. (a) Jinsi gani Babuloni wa kale ‘alifanya dunia yote ilewe’? (b) Babuloni Mkubwa ‘amefanyaje dunia yote ilewe’?

      11 Na zaidi, Babuloni wa kale alielezwa kuwa “kikombe cha dhahabu katika mkono wa Yehova, akifanya dunia yote ilewe.” (Yeremia 51:7, NW) Babuloni wa kale alilazimisha mataifa jirani kumeza maonyesho ya kasirani ya Yehova alipoyashinda kijeshi, kuyafanya dhaifu kama wanadamu waliolewa. Katika njia hiyo, alikuwa chombo cha Yehova. Babuloni Mkubwa, pia, amefanya ushindi mwingi kwa kadiri ya kuwa milki ya ulimwenguni pote. Lakini yeye kwa uhakika si chombo cha Yehova. Badala ya hivyo, yeye ametumikia “wafalme wa dunia” ambao pamoja nao yeye hufanya uasherati wa kidini. Yeye hufurahisha wafalme hawa kwa kutumia mafundisho yake ya uwongo na mazoea yenye kutumikisha ili kuweka matungamo ya watu, “wale wanaoikaa dunia,” kuwa dhaifu kama wanadamu waliolewa, wakitii watawala wao bila kuwa na la kufanya.

      12. (a) Kisehemu kimoja cha Babuloni Mkubwa katika Japani kilikuwaje na daraka la kumwagwa kwa damu nyingi wakati wa Vita ya Ulimwengu 2? (b) Jinsi gani “maji” yenye kuunga mkono Babuloni Mkubwa yaliondolewa katika Japani, na kukiwa na tokeo gani?

      12 Japani ya Shinto hutoa kielelezo kinachostahili kuangaliwa cha jambo hili. Askari-jeshi Wajapani waliiona kuwa heshima ya juu zaidi sana kutoa uhai wao kwa ajili ya maliki—mungu mkuu wa Shinto. Wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, askari-jeshi Wajapani wapatao 1,500,000 walikufa vitani; karibu kila mtu aliona kusalimu amri kuwa utovu wa heshima. Lakini likiwa tokeo la ushinde wa Japani, Maliki Hirohito alilazimika kukana dai lake la uungu. Hilo lilitokeza mwondoleo mkubwa wa “maji” yaliyounga mkono kisehemu cha Shinto cha Babuloni Mkubwa—loo! baada ya Ushinto kuidhinisha umwagaji wa ndoo nyingi za damu katika uwanja wa vita wa Pasifiki! Mdhoofisho huu wa uvutano wa Shinto ulifungua pia njia katika miaka ya juzi kwa ajili ya Wajapani 200,000, ambao walio wengi wao walikuwa hapo kwanza Washinto na Wabuddha, wawe wahudumu walio wakfu na waliobatizwa wa Yehova Bwana Mwenye Enzi Kuu.

      Kahaba Apanda Hayawani

      13. Ni mwono gani wenye kushangaza anaoona Yohana wakati malaika anapompeleka katika jangwa kwa nguvu ya roho?

      13 Unabii hufumbua nini zaidi kwa habari ya kahaba mkubwa na msiba wake? Kama Yohana anavyosimulia sasa, mandhari nyingine iliyo wazi sana yaonekana: “Na yeye [malaika] akapeleka mimi mbali kwa nguvu ya roho kuingia ndani ya jangwa. Na mimi nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye alikuwa amejaa majina ya kufuru na ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”—Ufunuo 17:3, NW.

      14. Ni kwa nini inafaa kwamba Yohana alipelekwa jangwani?

      14 Ni kwa nini Yohana anapelekwa ndani ya jangwa? Tamko la mapema zaidi la uangamivu dhidi ya Babuloni wa kale lilielezwa kuwa “dhidi ya jangwa la bahari.” (Isaya 21:1, 9, NW) Hilo lilitoa onyo linalostahili kwamba, ujapokuwa ulinzi wake mwingi wa kimaji, Babuloni wa kale angekuwa ukiwa usio na uhai. Inafaa, basi, kwamba yampasa Yohana apelekwe katika njozi yake kwenye jangwa akaone msiba wa Babuloni Mkubwa. Yeye pia lazima awe ukiwa na utupu. (Ufunuo 18:19, 22, 23) Ingawa hivyo, Yohana anashangazwa na anachoona nje kule. Kahaba mkubwa hayuko peke yake! Yeye anaketi juu ya dubwana la hayawani-mwitu!

      15. Ziko tofauti gani kati ya hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1 na yule wa Ufunuo 17:3?

      15 Hayawani-mwitu huyu ana vichwa saba na pembe kumi. Basi, je! yeye ni hayawani-mwitu yule yule ambaye Yohana aliona mapema zaidi, ambaye pia alikuwa na vichwa saba na pembe kumi? (Ufunuo 13:1) La, ziko tofauti. Hayawani-mwitu huyu ni rangi-nyekundu-nyangavu na, tofauti na hayawani-mwitu aliyetangulia, hasemwi kuwa ana mataji. Badala ya yeye kuwa na majina ya kufuru juu ya vichwa vyake saba tu, yeye ‘anajaa majina ya kufuru.’ Hata hivyo, lazima pawe na uhusiano kati ya hayawani-mwitu mpya na yule aliyetangulia; mifanano kati yao ni mingi mno kuwa ya nasibu.

      16. Ni nini utambulisho wa huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na imetaarifiwa nini kwa habari ya kusudi lake?

      16 Basi, hayawani-mwitu mpya rangi-nyekundu-nyangavu ni nini? Yeye ni lazima awe ule mfano wa hayawani-mwitu ambao ulitokezwa kwa himizo la hayawani-mwitu Uingereza-Amerika aliyekuwa na pembe mbili mithili ya mwana-kondoo. Baada ya mfano huo kuwa umefanywa, huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili aliruhusiwa kuupa pumzi huo mfano wa hayawani-mwitu. (Ufunuo 13:14, 15) Yohana anaona sasa mfano ulio hai, unaopumua. Ni picha ya tengenezo la Ushirika wa Mataifa ambalo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alileta kwenye uhai katika 1920. Rais Wilson wa U.S. alikuwa na njozi ya kwamba Ushirika huo “ungekuwa baraza la kutolea watu wote haki na kufutilia mbali milele tisho la vita.” Lilipofufuliwa baada ya vita ya ulimwengu ya pili likiwa Umoja wa Mataifa, kusudi la katiba yalo lilikuwa “kudumisha amani na usalama wa kimataifa.”

      17. (a) Ni katika njia gani huyo hayawani-mwitu wa ufananisho rangi-nyekundu-nyangavu anajaa majina ya kufuru? (b) Ni nani anayempanda huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? (c) Dini ya Kibabuloni ilijifungamanishaje na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao pale pale mwanzoni?

      17 Ni katika njia gani huyu hayawani-mwitu wa ufananisho anajaa majina ya kufuru? Katika njia ya kwamba wanadamu wameisimamisha sanamu hii ya kuabudiwa na mataifa mengi ikiwa kibadala cha Ufalme wa Mungu—itimize jambo ambalo Mungu husema ni Ufalme wake pekee unaoweza kutimiza. (Danieli 2:44; Mathayo 12:18, 21) Ingawa hivyo, jambo lenye kutokeza kuhusu njozi ya Yohana ni kwamba, Babuloni Mkubwa anapanda hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu. Kupatana na ukweli wa unabii, dini ya Kibabuloni, hasa katika Jumuiya ya Wakristo, imejifungamanisha yenyewe na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao. Mapema kama Desemba 18, 1918, shirika ambalo sasa linajulikana kuwa Baraza la Taifa la Makanisa ya Kristo katika Amerika lilipitisha julisho-wazi lililojulisha wazi kwa sehemu hivi: “Ushirika kama huo si manufaa ya kisiasa tu; badala ya hivyo ni wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani. . . . Kanisa linaweza kutoa roho ya nia njema, ambayo bila hiyo hakuna Ushirika wa Mataifa unaoweza kudumu. . . . Ushirika wa Mataifa una mizizi katika Gospeli. Kama Gospeli, lengo lao ni ‘amani duniani, nia njema kuelekea wanadamu.’”

      18. Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walionyeshaje uungaji-mkono wao kwa Ushirika wa Mataifa?

      18 Katika Januari 2, 1919, San Fransisco Chronicle lilikuwa na kichwa kikuu cha habari kwenye ukurasa wa kwanza: “Papa Asihi Ukubaliwe Ushirika wa Maitafa wa Wilson.” Katika Oktoba 16, 1919, ombi rasmi lililotiwa sahihi na makasisi wa vikundi mashuhuri 14,450 lilitolewa kwenye Seneti ya U.S., kuhimiza baraza hilo ‘liidhinishe mwafaka wa amani wa Paris uliotia ndani agano la ushirika wa mataifa.’ Ingawa Seneti ya U.S. ilishindwa kuidhinisha mwafaka huo, viongozi wa Jumuiya ya Wakristo waliendelea kufanya kampeni kwa ajili ya huo Ushirika. Na Ushirika huo ulizinduliwaje? Habari iliyopelekwa kutoka Uswisi, yenye tarehe ya Novemba 15, 1920, ilisomwa hivi: “Kufunguliwa kwa kusanyiko la kwanza la Ushirika wa Mataifa kulitangazwa kwenye saa tano asubuhi hii kwa kupigwa kengele zote za kanisa katika Geneva.”

      19. Wakati hayawani-mwitu alipotokea, jamii ya Yohana ilichukua mwendo gani wa tendo?

      19 Je! jamii ya Yohana, kikundi pekee duniani ambacho kilikubali kwa hamu nyingi Ufalme wa Kimesiya uliokuwa ukija, kilishiriki pamoja na Jumuiya ya Wakristo katika kumpa shikamoo huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? Mbali kabisa na hilo! Jumapili, Septemba 7, 1919, mkusanyiko wa watu wa Yehova kwenye Sida Pointi, Ohaiyo, ulikuwa na hotuba ya watu wote iliyokuwa na kichwa “Tumaini kwa Binadamu Wenye Kutaabika.” Siku iliyofuata, Star-Journal ya Sandusky iliripoti kwamba J. F. Rutherford, katika kuhutubia watu karibu 7,000, alikuwa “amesisitiza kwamba kutopendezwa kwa Bwana ni hakika kutajilia Ushirika . . . kwa sababu viongozi wa kidini—Wakatoliki na Waprotestanti—wakidai kuwa wawakilishi wa Mungu, wameacha mpango wake na wakakubali Ushirika wa Mataifa, wakiushangilia kuwa wonyesho wa kisiasa wa ufalme wa Kristo duniani.”

      20. Ni kwa sababu gani ilikuwa kufuru viongozi wa kidini kushangilia Ushirika wa Mataifa kuwa “wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani”?

      20 Ushinde wenye kusikitisha sana wa Ushirika wa Mataifa ulipaswa kuashiria viongozi wa kidini kwamba vyombo hivyo vyenye kufanywa na mwanadamu si sehemu ya Ufalme wa Mungu duniani. Ni kufuru kama nini kudai hivyo! Hufanya ionekane kana kwamba Mungu alishiriki kufanyiza Ushirika wa Mataifa ambao ni kazi ya ovyo sana. Kwa habari ya Mungu “utendaji wake ni mkamilifu.” Ufalme wa Yehova wa kimbingu chini ya Kristo—wala si muungano wa wanasiasa wenye kuzozana, wengi wao wakiwa hawaitikadi kuwako kwa Mungu—ndiyo njia ambayo kwayo yeye ataleta amani na kufanya penzi lake lifanywe duniani kama katika mbingu.—Kumbukumbu 32:4; Mathayo 6:10, NW.

      21. Ni nini kinachoonyesha kwamba kahaba mkubwa anaunga mkono na kusifu mno mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa?

      21 Namna gani mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa? Tangu mwanzo wao, baraza hili limekuwa na kahaba akilipanda mgongoni mwalo, akishirikiana nalo waziwazi na akijaribu kuongoza liendako. Mathalani, katika ukumbusho wa mwaka wao wa 20 katika Juni 1965, wawakilishi wa Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa Orthodoksi la Mashariki, pamoja na Waprotestanti, Wayahudi, Wahindu, Wabuddha, na Waislamu—waliosemekana kuwakilisha idadi ya watu wa dunia elfu mbili milioni—walikusanyika katika San Francisco kusherehekea uungaji-mkono na usifaji wao wa UM. Alipozuru UM Oktoba 1965, Papa Paul 6 alieleza habari zao kuwa “hilo tengenezo la kimataifa kubwa zaidi ya yote” na akaongeza: “Vikundi vya watu wa dunia vinategemea Umoja wa Mataifa kuwa ndilo tumaini la mwisho la itifaki na amani.” Mgeni mwingine wa kipapa, Papa John Paul 2, akihutubia UM katika Oktoba 1979, alisema: “Mimi natumaini Umoja wa Mataifa utadumu daima ukiwa ndilo baraza kuu la amani na haki.” Kwa uwazi sana, huyo papa alimtaja Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu mara chache sana katika hotuba yake. Wakati wa ziara yake United States katika Septemba 1987, kama ilivyoripotiwa na The New York Times, “John Paul alisema kirefu juu ya daraka chanya la Umoja wa Mataifa katika kuendeleza . . . ‘ushirikiano mpya wa ulimwenguni pote.’”

      Jina, Fumbo

      22. (a) Ni hayawani wa aina gani ambaye kahaba mkubwa amechagua kupanda? (b) Yohana anaelezaje habari ya kahaba wa ufananisho Babuloni Mkubwa?

      22 Karibuni mtume Yohana atajifunza kwamba kahaba mkubwa amechagua kupanda hayawani hatari. Ingawa hivyo, kwanza uangalifu wake wageukia Babuloni Mkubwa mwenyewe. Yeye amepambwa kitajiri, lakini, oh, jinsi anavyokirihisha! “Na huyo mwanamke alikuwa amepambwa zambarau na nyekundu-nyangavu na alikuwa amerembwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu na katika mkono wake alikuwa na kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake. Na juu ya kipaji cha uso wake paliandikwa jina, fumbo: ‘Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia.’ Na mimi nikaona kwamba mwanamke alikuwa amelewa damu ya watakatifu na damu ya mashahidi wa Yesu.”—Ufunuo 17:4-6a, NW.

      23. Ni jina gani kamili la Babuloni Mkubwa, na maana yalo ni nini?

      23 Kama ilivyokuwa desturi katika Roma ya kale, malaya huyu anatambuliwa kwa jina lililo juu ya kipaji cha uso wake.d Ni jina refu: “Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia.” Jina hilo ni “fumbo,” jambo fulani lenye maana iliyofichwa. Lakini kwa wakati wa Mungu fumbo hilo litafafanuliwa. Kwa kweli, malaika anampa Yohana habari ya kutosha kuruhusu watumishi wa Yehova leo wafahamu umaana kamili wa jina hili lenye maelezo. Sisi tunatambua Babuloni Mkubwa kuwa dini bandia yote. Yeye ndiye “mama ya makahaba” kwa sababu dini bandia zote moja moja katika ulimwengu, kutia ndani mafarakano katika Jumuiya ya Wakristo, ni kama mabinti wake, zikimwiga yeye katika kufanya ukahaba wa kiroho. Yeye pia ni mama ya “vitu vya kunyarafisha” katika njia ya kwamba yeye amezaa wazao wenye makuruhu kama vile ibada ya sanamu, uwasiliano na roho, kupiga ramli, unajimu, uaguzi wa kutazama vitanga vya mikono, kudhabihu binadamu, umalaya wa hekaluni, ulevi katika kuheshimu miungu bandia, na mazoea mengine machafu.

      24. Ni kwa sababu gani inafaa kwamba Babuloni Mkubwa amevalia “zambarau na rangi-nyekundu-nyangavu” na “amepambwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu”?

      24 Babuloni Mkubwa amevalia “zambarau na nyekundu-nyangavu,” rangi za jamaa ya kifalme, na “amerembwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu.” Inafaa kama nini! Fikiria tu yale majengo yote mazuri mno, sanamu-umbo na taswira azizi, aikoni zenye bei sana, na vikorokoro vingine vya kidini, pamoja na kiasi ambacho ni vigumu kuitikadi cha mali na pesa, kisichohesabika ambacho dini za ulimwengu huu zimerundika. Iwe ni katika Vatikani, katika milki ya uevanjeli wa TV ambao kitovu chayo ni United States, au katika misikiti na mahekalu yenye kuvutia ya Mashariki, Babuloni Mkubwa amerundika kama tungamo—na nyakati nyingine akapoteza—ukwasi mwingi mno.

      25. (a) Ni nini kinachofananishwa na “kikombe cha dhahabu ambacho kilijaa vitu vya kunyarafisha?” (b) Ni katika maana gani kahaba wa ufananisho amelewa?

      25 Tazama sasa alicho nacho kahaba huyu mkononi mwake. Haikosi Yohana alitweta kwa mshangao kukiona—kikombe cha dhahabu “kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake”! Hiki ndicho kikombe ambacho ndani yacho mna “divai ya kasirani ya uasherati wake” ambacho kwa hicho amefanya mataifa yote yalewe. (Ufunuo 14:8; 17:4) Kwa nje kinaonekana kuwa chenye utajiri, lakini yaliyomo ni yenye kunyarafisha, si safi. (Linga Mathayo 23:25, 26.) Ndani kina mazoea yote machafu na uwongo mwingi ambao huyo kahaba mkubwa ametumia kutongoza mataifa na kuwaleta chini ya uvutano wake. Lenye makuruhu hata kuchukiza zaidi, Yohana anaona kwamba huyo kahaba mwenyewe amelewa, amekunywa sana damu ya watumishi wa Mungu! Kwa kweli, baadaye sisi tunasoma kwamba “katika yeye ilipatikana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” (Ufunuo 18:24, NW) Ni hatia ya damu kubwa mno kama nini!

      26. Kuna ithibati gani ya hatia ya damu upande wa Babuloni Mkubwa?

      26 Kwa muda wa karne zilizopita, milki ya ulimwengu ya dini bandia imemwaga damu nyingi kama bahari. Mathalani, katika Japani ya zamani za kale, mahekalu katika Kyoto yaligeuzwa kuwa ngome, na watawa-mashujaa-vita, wakiliitia “jina takatifu la Buddha,” walipigana vita mpaka barabara zikawa nyekundu kwa damu. Katika karne ya 20, viongozi wa kidini walipiga miguu wakiwa pamoja na majeshi ya nchi zao, na walichinjana, kukiwa na hasara ya angalau maisha milioni mia moja. Katika Oktoba 1987 Nixon aliyekuwa rais wa U.S. alisema: “Karne ya 20 imekuwa ndiyo yenye damu nyingi zaidi ya zote katika historia. Watu zaidi wameuawa katika vita vya karne hii kuliko katika vita vyote vilivyopiganwa kabla ya karne hii kuanza.” Dini za ulimwengu zimehukumiwa vibaya na Mungu kwa sababu ya ushiriki wazo katika yote haya; Yehova hukirihi “mikono ambayo inamwaga damu isiyo na hatia.” (Mithali 6:16, 17, NW) Mapema zaidi, Yohana alisikia kilio kutoka madhabahu: “Ni mpaka lini, Bwana Mwenye Enzi Kuu mtakatifu na wa kweli, wewe unajizuia usihukumu na kulipiza kisasi damu yetu juu ya wale ambao wanakaa juu ya dunia?” (Ufunuo 6:10, NW) Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia, atahusika sana ujapo wakati wa kujibu swali hilo.

  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 34

      Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa

      1. (a) Yohana anatendaje kama itikio anapoona kahaba mkubwa na mpandwaji wake mwenye kutia hofu, na kwa nini? (b) Jamii ya Yohana inatendaje leo kama itikio, matukio yanapokunjuka katika utimizo wa njozi ya kiunabii?

      TENDO-MWITIKIO la Yohana ni nini anapomwona “kahaba mkubwa” na mpandwaji wake mwenye kutia hofu? Yeye mwenyewe ajibu: “Basi, nilipoona yeye mimi nilistaajabu kwa staajabu kubwa.” (Ufunuo 17:6b, NW) Mawazo vivi hivi tu ya kibinadamu hayangeweza kutunga mwono kama huo. Hata hivyo ndio huo—mbali kule jangwani—malaya mpujufu akimpanda hayawani-mwitu wa kutisha mwenye rangi-damu-nyangavu! (Ufunuo 17:3) Jamii ya Yohana leo pia hustaajabu kwa staajabu kubwa matukio yanapokunjuka katika utimizo wa njozi ya kiunabii. Kama watu wa ulimwengu wangeweza kuiona, wao wangepaaza sauti kusema, ‘Haisadikiki!’ na watawala wa ulimwengu wangerudisha mwangwi wakisema, ‘Haifikiriki!’ Lakini njozi hiyo inakuwa uhalisi wenye kugutusha katika siku zetu. Tayari watu wa Mungu wamekuwa na ushiriki wenye kutokeza katika utimizo wa njozi hiyo, na hiyo inawahakikishia kwamba unabii huo utasonga mbele moja kwa moja mpaka upeo wao wenye kupiga butaa.

      2. (a) Katika kuitikia mshangao mkubwa wa Yohana, malaika anamwambia nini? (b) Jamii ya Yohana imefunuliwa nini, na hilo limefanywaje?

      2 Malaika anaona mshangao mkubwa wa Yohana. “Na hivyo,” Yohana aendelea, “malaika akasema kwa mimi: ‘Kwa nini wewe ulistaajabu? Mimi nitakuambia fumbo la mwanamke na la hayawani-mwitu ambaye anabeba yeye na ambaye ana vichwa saba na pembe kumi.’” (Ufunuo 17:7, NW) Aha, sasa malaika atalifumbua fumbo! Yeye amfafanulia Yohana mwenye kukodoa macho nyuso mbalimbali za njozi na matukio ya kidrama yanayokaribia kukunjuka. Hali kadhalika, inapotumikia chini ya mwelekezo wa kimalaika leo, jamiii ya Yohana yenye kutazama imefunuliwa uelewevu wa huo unabii. Je! “kufasiri si kazi ya Mungu?” Kama Yosefu mwaminifu, sisi tunaitikadi kwamba ni yake. (Mwanzo 40:8; linga Danieli 2:29, 30.) Watu wa Mungu wamewekwa kana kwamba wako katikati ya jukwaa, Yehova anapowafasiria maana ya njozi na matokeo yayo juu ya maisha zao. (Zaburi 25:14) Kwa wakati barabara, yeye amewafungulia uelewevu wao fumbo la mwanamke na hayawani-mwitu.—Zaburi 32:8.

      3, 4. (a) Ni hotuba gani ya watu wote iliyotolewa na N. H. Knorr katika 1942, nayo ilimtambulishaje hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? (b) Ni maneno gani ambayo malaika alisema kwa Yohana yaliyozungumzwa na N. H. Knorr?

      3 Kutoka Septemba 18 kufika 20, 1942, wakati wa upeo wa Vita ya Ulimwengu 2, Mashahidi wa Yehova katika United States walikuwa na Ulimwengu Mpya wa Kitheokrasi Kusanyiko. Jiji kuu la kusanyiko, Cleveland, Ohaiyo, lilifunganishwa kwa waya za simu na majiji mengine zaidi ya 50 ya mkusanyiko, kukiwa na kilele cha hadhirina 129,699. Mahali ambako hali za wakati wa vita ziliruhusu, mikusanyiko mingine ilirudia programu hiyo kuzunguka ulimwengu. Wakati ule, wengi wa watu wa Yehova walitaraji kwamba vita hiyo ingeongezeka na kuwa vita ya Mungu ya Har–Magedoni; kwa sababu hiyo kile kichwa cha hotuba ya watu wote, “Amani—Je! Inaweza Kudumu?,” kiliamsha udadisi mwingi. N. H. Knorr, msimamizi mpya wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi angewezaje kuthubutu kuongea juu ya amani wakati kinyume kabisa ndilo jambo lililoelekea kuwa akibani kwa ajili ya mataifa?a Sababu ilikuwa kwamba jamii ya Yohana ilikuwa ikitoa “zaidi ya uangalifu wa kawaida” kwenye Neno la kiunabii la Mungu.—Waebrania 2:1; 2 Petro 1:19, NW.

      4 Hotuba “Amani—Je! Inaweza Kudumu?” ilitupa nuru gani juu ya unabii? Akitambulisha waziwazi hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa Ufunuo 17:3 kuwa Ushirika wa Mataifa, N. H. Knorr aliendelea kuzungumzia mwendo wao wenye msukosuko juu ya msingi wa maneno yafuatayo ya malaika kwa Yohana: “Hayawani-mwitu ambaye wewe uliona alikuwako, lakini hayuko, na bado yu karibu kupanda atoke ndani ya abiso, na yeye anapaswa kwenda zake ndani ya uharibifu.”—Ufunuo 17:8a, NW.

      5. (a) Ni jinsi gani kwamba “hayawani-mwitu . . . alikuwako” na kisha “hayuko”? (b) N. H. Knorr alijibuje swali “Je! Ushirika utabaki katika shimo?”

      5 “Hayawani-mwitu . . . alikuwako.” Ndiyo, alikuwa amekuwako akiwa Ushirika wa Mataifa kutoka Januari 10, 1920, na kuendelea, kukiwa na mataifa 63 yenye kushiriki kwa wakati mmoja au mwingine. Lakini, kwa zamu, Japani, Ujeremani, na Italia zilijiondoa, na nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti ziliondolewa kutoka Ushirika huo. Katika Septemba 1939 dikteta Mnazi wa Ujeremani alianzisha Vita ya Ulimwengu 2.b Ukiwa umeshindwa kuendeleza amani katika ulimwengu, Ushirika wa Mataifa ulitumbukia kabisa ndani ya abiso ya kutotenda. Kufikia 1942 ulikuwa haupo kabisa. Wala kabla ya hapo wala kwenye tarehe fulani ya baadaye Yehova hakufasiria watu wake kina kamili cha maana ya njozi hiyo, ila kwenye wakati huo hasa wenye hatari! Kwenye Ulimwengu Mpya wa Kitheokrasi Kusanyiko, N. H. Knorr angeweza kujulisha wazi, kupatana na unabii, kwamba “hayawani-mwitu . . . hayuko.” Kisha akauliza swali, “Je! Ushirika utabaki katika shimo?” Akinukuu Ufunuo 17:8, NW, yeye akajibu: “Ushirika wa mataifa ya kilimwengu utainuka tena.” Na ndivyo ikathibitika kuwa hasa—katika kutetea ukweli wa Neno la Yehova la kiunabii!

      Kupanda Kutoka Abiso

      6. (a) Ni lini hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu alipopanda kutoka abiso, na kwa jina gani jipya? (b) Ni kwa nini kwa kweli Umoja wa Mataifa ni uhuisho wa hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu?

      6 Hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu alipanda kweli kweli kutoka katika abiso. Katika Juni 26, 1945, kukiwa na kishindo cha sherehe ya vigelegele katika San Francisco, U.S.A., mataifa 50 yalipiga kura kukubali Katiba ya tengenezo la Umoja wa Mataifa. Baraza hili lilipaswa “kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Kulikuwako mifanano mingi kati ya Ushirika na UM. The World Book Encyclopedia hueleza: “Katika njia fulani, UM hushabihi Ushirika wa Mataifa, ambao ulipangwa kitengenezo baada ya Vita ya Ulimwengu 1 . . . Mengi ya mataifa yaliyoasisi UM yalikuwa pia yameasisi ule Ushirika. Kama Ushirika, UM ulisimamishwa kusaidia kutunza amani kati ya mataifa. Ala kuu za UM zafanana sana na zile za Ushirika.” Basi, UM kwa kweli ni uhuisho wa hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu. Uanachama wao wa mataifa yapatayo 190 unazidi kwa mbali sana ule wa Ushirika wenye mataifa 63; umechukua pia madaraka makubwa zaidi ya yale ya mtangulizi wao.

      7. (a) Ni katika njia gani wakaaji wa dunia wamestaajabu kwa kusifu mno huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu aliyehuishwa? (b) Ni mradi gani ambao umetatiza UM, naye katibu mkuu wao alisema nini kwa habari hii?

      7 Mwanzoni, matumaini makubwa yalionyeshwa kwa ajili ya UM. Hiyo ilikuwa katika utimizo wa maneno haya ya malaika: “Na wakati wao waona jinsi hayawani-mwitu alikuwako, lakini hayuko, na bado atakuwapo, wale ambao hukaa juu ya dunia watastaajabu kwa kusifu mno, lakini majina yao hayajaandikwa juu ya hati-kunjo ya uhai tangu kuasisiwa kwa ulimwengu.” (Ufunuo 17:8b, NW) Wakaaji wa dunia wamesifu mno dude jipya hili, linalotenda kutoka makao makuu yalo yenye fahari kwenye East River wa New York. Lakini amani ya kweli na usalama vimetatiza UM. Katika sehemu kubwa ya karne ya 20, amani ya ulimwengu ilidumishwa tu kwa tisho la “angamizano hakika,” nayo mashindano ya kuunda silaha yameendelea kuongezeka kwa kadiri kubwa mno. Baada ya jitihada ya Umoja wa Mataifa ya miaka karibu 40, aliyekuwa katibu mkuu wao, Javier Pérez de Cuéllar, aliomboleza hivi katika 1985: “Sisi tunaishi katika enzi nyingine ya washupavu, na sisi hatujui la kufanya juu ya hilo.”

      8, 9. (a) Ni kwa nini UM hauna jawabu kwa matatizo ya ulimwengu, nao utapatwa na nini kulingana na amri ya Mungu? (b) Ni kwa nini waasisi na wasifaji wa UM hawakuandikisha majina yao katika “hati-kunjo ya uhai” ya Mungu? (c) Ufalme wa Yehova utatimiza jambo gani kwa kufaulu?

      8 UM hauna jawabu. Na kwa nini? Kwa sababu Mpaji uhai wa aina ya binadamu yote siye mpaji-uhai wa UM. Urefu wa maisha yao utakuwa mfupi, kwa kuwa kulingana na amri ya Mungu, ‘wapaswa kwenda zao ndani ya uharibifu.’ Waasisi na wasifaji mno wa UM hawakuandikisha majina yao katika hati-kunjo ya uhai ya Mungu. Watu wenye dhambi, wenye kufa, wengi wao wakiwa wadhihaki wa jina la Mungu, wangewezaje kufanikiwa kupata kupitia UM kitu ambacho Yehova Mungu amejulisha wazi kwamba yeye yu karibu kutimiza, si kwa njia za kibinadamu, bali kupitia Ufalme wa Kristo wake?—Danieli 7:27; Ufunuo 11:15.

      9 Kwa kweli UM ni kitu bandia chenye makufuru cha Ufalme wa Kimesiya wa Mungu kupitia Yesu Kristo, Mwana-Mfalme wa Amani wake—ambaye utawala wake wa kifalme hautakuwa na mwisho. (Isaya 9:6, 7, NW) Hata kama UM ungeweza kutiatia kama viraka amani fulani ya kitambo, vita vingefyatuka tena. Hiyo ni asili ya watu wenye dhambi. “Majina yao hayajaandikwa juu ya hati-kunjo ya uhai tangu kuasisiwa kwa ulimwengu.” Ufalme wa Yehova kupitia Kristo hautasimamisha tu amani ya milele duniani bali, juu ya msingi wa dhabihu ya ukombozi ya Yesu, utainua wafu, waadilifu na wasio waadilifu ambao wamo katika kumbukumbu la Mungu. (Yohana 5:28, 29; Matendo 24:15) Hii inatia ndani kila mmoja ambaye amebaki akiwa imara ijapokuwa mashambulizi ya Shetani na mbegu yake, na wengine ambao wangali watajionyesha wenyewe kuwa watiifu. Kwa wazi, hati-kunjo ya uhai ya Mungu haitakuwa kamwe na majina ya wafuasi washupavu wa Babuloni Mkubwa au ya wowote wanaoendelea kuabudu hayawani-mwitu.—Kutoka 32:33, NW; Zaburi 86:8-10; Yohana 17:3; Ufunuo 16:2; 17:5.

      Amani na Usalama —Tumaini la Bure

      10, 11. (a) UM ulipiga mbiu ya nini katika 1986, na itikio lilikuwa nini? (b) Ni “jamaa za kidini” ngapi zilizokusanyika katika Assisi, Italia, kusali kwa ajili ya amani, na je! Mungu anajibu sala kama hizo? Fafanua.

      10 Katika jitihada za kutegemeza matumaini ya aina ya binadamu, Umoja wa Mataifa ulipiga mbiu ya 1986 kuwa “Mwaka wa Amani ya Kimataifa,” ukiwa na kichwa “Kulinda Salama Amani na Wakati Ujao wa Binadamu.” Mataifa yenye kupiga vita yaliombwa yalaze silaha zayo, angalau kwa mwaka mmoja. Itikio layo lilikuwa nini? Kulingana na ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa, watu wapatao milioni tano walikufa kwa sababu ya vita wakati wa 1986 pekee! Ingawa sarafu kadhaa za pekee na stampu za mwadhimisho zilitolewa, mataifa yaliyo mengi yalifanya kidogo sana kwa habari ya kufuatia wazo bora la amani katika mwaka huo. Hata hivyo, dini za ulimwengu—zikitamani sikuzote kuafikiana na UM—zilianza kutangaza mwaka huo kwa njia mbalimbali. Katika Januari 1, 1986, Papa John Paul 2 alisifu kazi ya UM na akaweka wakfu mwaka mpya kwa ajili ya amani. Na katika Oktoba 27, akakusanya viongozi wa nyingi za dini za ulimwengu katika Assisi, Italia, ili kusali kwa ajili ya amani.

      11 Je! Mungu anajibu sala kama hizo kwa ajili ya amani? Basi, viongozi wa kidini hao walikuwa wakisali kwa Mungu yupi? Kama ungewauliza, kila kikundi kingekupa jibu tofauti. Je! kuna jamii ya mamilioni ya miungu inayoweza kusikia na kujibu maombi rasmi yaliyotolewa kwa njia nyingi mbalimbali? Wengi wa washiriki waliabudu Utatu wa Jumuiya ya Wakristo.c Wabuddha, Wahindu, na wengine walitoa sala zao kwa miungu isiyo na hesabu. Kwa ujumla, “jamaa za kidini” 12 zilikusanyika, zikiwa zinawakilishwa na watu mashuhuri kama Askofu Mkuu wa Kianglikana wa Kantabari, Dalai Lama wa Buddha, kasisi wa Orthodoksi la Urusi, Msimamizi wa Ushirika wa Patakatifu pa Shinto wa Tokyo, waabudu-mizimu wa Kiafrika, na Wahindi Waamerika wawili waliovalia vazi la kichwani la manyoya-manyoya. Kilikuwa kikundi chenye rangi za namna namna, bila kusema zaidi, kikifanyiza kipindi cha TV chenye kutazamisha. Kikundi kimoja kilisali bila kukoma kwa saa 12 katika wakati mmoja. (Linga Luka 20:45-47.) Lakini je! yoyote ya sala hizo ilipenya mawingu ya mvua yaliyoning’inia juu ya mkusanyiko huo? Kwa sababu zinazofuata, la:

      12. Ni kwa sababu zipi Mungu hakujibu sala za viongozi wa kidini wa ulimwengu kwa ajili ya amani?

      12 Tofauti na wale ambao “hutembea katika jina la Yehova,” hakuna mwanadini hata mmoja wa hao aliyekuwa akisali kwa Yehova, Mungu aliye hai, ambaye jina lake huonekana mara zapata 7,000 katika maandishi asilia ya Biblia. (Mika 4:5; Isaya 42:8, 12, NW)d Wakiwa kikundi wao hawakumwendea Mungu kwa jina la Yesu, walio wengi wao wakiwa hata hawaitikadi katika Yesu Kristo. (Yohana 14:13; 15:16) Hakuna baadhi yao wanaofanya mapenzi ya Mungu kwa ajili ya siku yetu, ambayo ni kupiga mbiu ulimwenguni pote ya Ufalme unaokuja wa Mungu—si UM—kuwa ndilo tumaini halisi kwa aina ya binadamu. (Mathayo 7:21-23; 24:14; Marko 13:10) Kwa sehemu iliyo kubwa zaidi matengenezo ya kidini yao yamejihusisha katika vita vyenye umwagaji-damu vya historia, kutia na vita viwili vya ulimwengu vya karne ya 20. Kwa hao, Mungu husema: “Hata ingawa nyinyi mnafanya sala nyingi, mimi sisikilizi; mikono yenu imejawa na umwagaji-damu.”—Isaya 1:15, NW; 59:1-3.

      13. (a) Ni kwa nini ni jambo la maana kwamba viongozi wa kidini wa ulimwengu wamepaswa kuungana mikono na UM katika kutoa mwito kwa ajili ya amani? (b) Vilio kwa ajili ya amani vitafikia upeo gani uliotabiriwa kimungu?

      13 Na zaidi, ni jambo la maana yenye kina kwamba viongozi wa kidini wamepaswa kuungana mikono na Umoja wa Mataifa katika kutoa mwito kwa ajili ya amani wakati huu. Wao wangependa kutumia uvutano juu ya UM kwa faida yao wenyewe, hasa katika enzi hii ya ki-siku-hizi wakati watu wao wanaacha dini. Kama viongozi wasio waaminifu katika Israeli wa kale, wao wanalia, “‘Kuna amani! Kuna amani!’ wakati hakuna amani.” (Yeremia 6:14, NW) Pasipo shaka vilio vyao kwa ajili ya amani vitaendelea, vikiwa vinainuka katika kuunga mkono upeo ambao kuhusu huo mtume Paulo alitolea unabii: “Siku ya Yehova inakuja sawasawa kama mwivi katika usiku. Wakati wowote wanaposema: ‘Amani na usalama!’ ndipo uharibifu wa ghafula utakuwa juu yao papo hapo kama maumivu makali ya ghafula ya taabu juu ya mwanamke mwenye mimba; na wao hawataponyoka kwa vyovyote.”—1 Wathesalonike 5:2, 3, NW.

      14. Huenda kilio cha “Amani na usalama!” kitakuwa cha namna gani, na mmoja anaweza kuepukaje kuongozwa vibaya?

      14 Katika miaka ya hivi karibuni, wanasiasa wametumia maneno “amani na usalama” kuelezea mipango mbalimbali ya wanadamu. Je! jitihada hizo za viongozi wa ulimwengu zinaonyesha mwanzo wa utimizo wa andiko la 1 Wathesalonike 5:3? Au je, Paulo alikuwa akizungumzia tukio hususa na lenye kutokeza sana hivi kwamba lingetambuliwa ulimwenguni? Kwa kuwa mara nyingi unabii wa Biblia hueleweka kikamili tu baada ya kutimia au wakati unapoendelea kutimia, itatubidi tungoje tuone itakuwaje. Kwa sasa, Wakristo wanajua kwamba hata ingawa huenda ikaonekana kana kwamba mataifa yamepata amani na usalama, hakuna kitu ambacho kwa kweli kitakuwa kimebadilika. Ubinafsi, chuki, uhalifu, mvunjiko wa jamaa, ukosefu wa adili, magonjwa, huzuni, na kifo bado vitakuwapo. Ndiyo sababu si lazima wewe uongozwe vibaya na kilio chochote cha “amani na usalama,” ikiwa umeamka kuona maana ya matukio ya ulimwengu na unatii maonyo ya kiunabii katika Neno la Mungu.—Marko 13:32-37; Luka 21:34-36.

      [Maelezo ya Chini]

      a J. F. Rutherford alikufa Januari 8, 1942, na N. H. Knorr alimfuata kuwa msimamizi wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi.

      b Katika Novemba 20, 1940, Ujeremani, Italia, Japani, na Hungary zilitia sahihi kwa ajili ya “Ushirika wa Mataifa mpya,” ikifuatwa siku nne baadaye na msambazo-redio wa Vatikani wa Misa na sala kwa ajili ya amani ya kidini na kwa ajili ya utaratibu mpya wa mambo. Huo ‘Ushirika mpya’ haukutokea.

      c Dhana ya Utatu ina shina kutoka Babuloni wa kale, ambako mungu-jua Shamashi, mungu-mwezi Sin, na mungu-nyota Ishta waliabudiwa wakiwa utatu. Misri ilifuata kigezo icho hicho, ikiabudu Osirisi, Isisi, na Horusi. Asshuri, mungu mkuu wa Ashuru, huonyeshwa taswira ya vichwa vitatu. Kwa kufuata kigezo hicho, mifano inapatikana katika makanisa ya Kikatoliki ikionyesha Mungu kuwa ana vichwa vitatu.

      d Webster’s Third New International Dictionary ya 1993 hufasili Yehova Mungu kuwa “mungu mkuu kupita wote anayetambuliwa na mungu pekee anayeabudiwa na Mashahidi wa Yehova.”

      [Picha katika ukurasa wa 250]

      Kinyume cha “Amani”

      Ingawa 1986 ulipigiwa mbiu na UM kuwa Mwaka wa Amani ya Kimataifa, shindano la ujiuaji la kuunda silaha liliongezeka. World Military and Social Expenditures 1986 hutoa fasili hizi zenye kumakinisha:

      Katika 1986 matumizi ya kijeshi ya tufe lote yalifikia dola milioni elfu 900.

      Matumizi ya kijeshi ya tufe lote ya saa moja yangetosha kuchanja watu milioni 3.5 ambao walikufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuambukiza yenye kuzuilika.

      Ulimwenguni pote, mtu mmoja kati ya watano aliishi katika umaskini wenye kuumiza. Watu hao wote wenye kufa-njaa wangeweza kulishwa kwa mwaka mmoja kwa gharama ya kile kiasi ambacho ulimwengu ulitumia kwa ajili ya silaha katika siku mbili.

      Nishati ya baruti iliyo katika rundo la silaha za nyukilia za ulimwengu ilikuwa kubwa zaidi ya ule mlipuko wa Chernobyl kwa mara 160,000,000.

      Bomu moja la nyukilia lingeweza kupelekwa likiwa na nguvu za mlipuko mara zaidi ya 500 ya bomu lililoangushwa juu ya Hiroshima katika 1945.

      Maghala ya zana za nyukilia yalikuwa na nguvu za baruti zinazolingana na Hiroshima zaidi ya milioni moja. Yaliwakilisha mara 2,700 za nguvu za baruti zilizoachiliwa katika Vita ya Ulimwengu 2, wakati watu milioni 38 walikufa.

      Vita vilikuwa vikitokea mara nyingi zaidi na ni vyenye kufisha zaidi. Vifo kutokana na vita vilikuwa jumla ya milioni 4.4 katika karne ya 18, milioni 8.3 katika karne ya 19, milioni 98.8 katika miaka 86 ya kwanza ya karne ya 20. Tangu karne ya 18, vifo kutokana na vita vimeongezeka zaidi ya mara sita kuliko idadi ya watu ya ulimwengu. Kulikuwako vifo mara kumi kwa kila vita katika karne ya 20 kuliko ilivyokuwa katika karne ya 19.

      [Picha katika ukurasa wa 247]

      Kama unabii ulivyotolewa juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu Ushirika wa Mataifa ulitiwa katika abiso wakati wa Vita ya Ulimwengu 2 lakini ulihuishwa ukiwa Umoja wa Mataifa

      [Picha katika ukurasa wa 249]

      Katika kuunga mkono “Mwaka wa Amani” wa UM, wawakilishi wa dini za ulimwengu walitoa sala ya mvurugo katika Assisi, Italia, lakini hakuna mmoja wao aliyetoa sala kwa Mungu aliye hai, Yehova

  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 35

      Kufisha Babuloni Mkubwa

      1. Malaika anaelezaje habari ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na ni hekima ya aina gani inayohitajiwa kuelewa mifananisho ya Ufunuo?

      KATIKA kueleza zaidi habari ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa Ufunuo 17:3, malaika anamwambia Yohana: “Hapa ndipo elimu iliyo na hekima inapofaa: Vichwa saba humaanisha milima saba, ambako mwanamke huketi juu ya kilele. Na wako wafalme saba: watano wameanguka, mmoja yupo, mwingine hajawasili bado, lakini yeye awasilipo lazima yeye abaki kitambo kifupi.” (Ufunuo 17:9, 10, NW) Malaika anawasilisha hekima kutoka juu, hekima pekee inayoweza kutoa uelewevu wa mifananisho katika Ufunuo. (Yakobo 3:17) Hekima hii inaipa jamii ya Yohana na waandamani wayo nuru juu ya hatari ya nyakati tunamoishi. Inajenga katika mioyo yenye kujitoa uthamini wa hukumu za Yehova, ambazo sasa karibu kutimizwa, na inakaza kikiki hofu yenye afya kuelekea Yehova. Kama Mithali 9:10, NW inavyotaarifu: “Hofu ya Yehova ndio mwanzo wa hekima, na maarifa ya kumjua Mmoja Aliye Mtakatifu Zaidi Sana ndio uelewevu.” Hekima ya kimungu inatufunulia nini juu ya hayawani-mwitu?

      2. Ni nini maana ya vichwa saba vya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na inakuwaje kwamba “watano wameanguka, mmoja yupo”?

      2 Vichwa saba vya hayawani-mwitu mkali sana husimamia “milima” saba, au “wafalme” saba. Semi zote mbili hutumiwa Kimaandiko kurejezea mamlaka za kiserikali. (Yeremia 51:24, 25; Danieli 2:34, 35, 44, 45) Katika Biblia, serikali za ulimwengu sita hutajwa kuwa zikiathiri mambo ya watu wa Mungu: Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, na Roma. Kati ya hizi, tano zilikuwa tayari zimekuja na zikaenda kufikia wakati Yohana alipopokea Ufunuo, lakini Roma ilikuwa ingali sana serikali ya ulimwengu. Hii inalingana vizuri na maneno haya, “watano wameanguka, mmoja yupo.” Lakini namna gani juu ya “mwingine” aliyekuwa akitazamiwa kuja?

      3. (a) Milki ya Roma ilikujaje kugawanywa? (b) Ni matukio gani yaliyotukia katika Magharibi? (c) Milki Takatifu ya Roma yapasa ionweje?

      3 Milki ya Roma ilidumu na hata ikapanuka kwa mamia ya miaka baada ya siku ya Yohana. Katika 330 W.K. Maliki Konstantino alihamisha jiji kuu lake kutoka Roma kwenda Bizanshamu, ambalo alilipa jina Konstantinopo. Katika 395 W.K., Milki ya Roma iligawanywa ikawa sehemu za Mashariki na Magharibi. Katika 410 W.K., Roma liliangushwa na Alariki, mfalme wa Wavisigothi (kabila la Kijeremani ambalo lilikuwa limeongolewa kuwa la “Ukristo” wa aina ya Aria). Makabila ya Kijeremani (ya “Kikristo” pia) yalishinda Hispania na eneo lililo kubwa zaidi la Roma katika Afrika Kaskazini. Zilikuwako karne za misukosuko, kutotulia, na kujirekebisha upya katika Ulaya. Wamaliki wenye sifa waliinuka katika Magharibi, kama vile Charlemagne, ambaye alifanya fungamano na Papa Leo 3 katika karne ya 9, na Frederick 2, ambaye alitawala katika karne ya 13. Lakini milki yao, ingawa iliitwa Milki Takatifu ya Roma ilikuwa ndogo zaidi ya ile Milki ya Roma ya mapema zaidi, wakati wa kilele cha usitawi wayo. Ilikuwa zaidi mrudisho au mwendelezo wa hiyo serikali ya kale kuliko kuwa milki mpya.

      4. Milki ya Mashariki ilikuwa na mafanikio gani, lakini kulitukia nini kwa sehemu kubwa ya lililokuwa eneo la Roma ya kale katika Afrika Kaskazini, Hispania, na Siria?

      4 Milki ya Mashariki ya Roma, yenye kitovu katika Konstantinopo, iliendelea ikiwa na uhusiano wenye wasiwasi na Milki ya Magharibi. Katika karne ya sita, maliki wa Mashariki Justiniani 1 aliweza kushinda sehemu kubwa ya Afrika ya Kaskazini, na pia akaingilia Hispania na Italia. Katika karne ya saba, Justiniani 2 alikombolea Milki hiyo maeneo ya Makedonia ambayo yalikuwa yameshindwa na wanamakabila wa Kislavi. Hata hivyo, Kufikia karne ya nane eneo kubwa la zamani la Roma ya kale katika Afrika Kaskazini, Hispania, na Siria lilikuwa limekuja chini ya milki mpya ya Islamu na hivyo likapita kutoka udhibiti wa Konstantinopo na Roma pia.

      5. Ingawa jiji la Roma lilianguka 410 W.K., ilikuwaje kwamba ilichukua karne nyingi zaidi kabla ya visehemu vyote vya Milki ya Roma ya kisiasa kutoweka katika mandhari ya ulimwengu?

      5 Jiji la Konstanipo lenyewe lilidumu kwa muda mrefu zaidi kidogo. Liliokoka mashambulizi ya mara nyingi kutoka kwa Waajemi, Waarabu, Wabulgari, na Warusi mpaka mwishowe katika 1203 likaangushwa—si na Waislamu bali na Wakrusedi kutoka Magharibi. Ingawa hivyo, katika 1453, lilikuja chini ya mamlaka ya mtawala Mwislamu wa Ottomani Mehmedi 2 na upesi likawa jiji kuu la Milki ya Ottomani, au ya Kituruki. Hivyo, ijapokuwa jiji la Roma lilianguka katika 410 W.K., ilichukua karne nyingi zaidi kabla ya visehemu vyote vya Milki ya Roma ya kisiasa kutoweka katika mandhari ya ulimwengu. Na hata hivyo, uvutano wayo bado ulitambulikana katika milki za kidini zenye msingi wa upapa wa Roma na makanisa ya Orthodoksi ya Mashariki.

      6. Ni milki zipi mpya kabisa zilizotokea, na ni ipi iliyopata kuwa yenye kufanikiwa zaidi sana?

      6 Hata hivyo, kufikia karne ya 15, nchi fulani zilikuwa zikijenga milki mpya kabisa. Ingawa baadhi ya serikali hizi mpya za kibepari zilipatikana katika maeneo ambayo hapo kwanza yalikuwa makoloni ya Roma, milki zazo hazikuwa mwendelezo vivi hivi wa Milki ya Roma. Ureno, Hispania, Ufaransa, na Uholanzi zote zikawa makao ya milki zilizotapakaa sana. Lakini iliyofanikiwa zaidi sana ilikuwa Uingereza, ambayo ikaja kusimamia milki kubwa mno ambayo juu yayo ‘jua halikutua kamwe.’ Milki hii ilienea katika nyakati mbalimbali juu ya sehemu kubwa ya Amerika Kaskazini, Afrika, India, na Esia Kusini-mashariki, pamoja na maeneo ya Pasifiki Kusini.

      7. Serikali ya ulimwengu ya uwili ilikujaje kuwako, na Yohana alisema ni kwa muda gani ‘kichwa’ au serikali ya ulimwengu ya saba ingeendelea?

      7 Kufikia karne ya 19, baadhi ya makoloni katika Amerika Kaskazini yalikuwa yamekwisha kujitenga na Uingereza yakaunda United States ya Amerika yenye kujitawala. Kisiasa, hitilafu fulani ziliendelea kati ya taifa jipya na iliyokuwa nchi-mama yao. Hata hivyo, vita ya ulimwengu ya kwanza ilizilazimisha hizo nchi zote mbili kutambua masilahi yazo ya pamoja na zikatia nguvu uhusiano maalumu kati yazo. Hivyo, namna ya serikali ya ulimwengu ya uwili ikatokea, ikiwa inafanyizwa na United States ya Amerika, sasa ikiwa ndilo taifa la ulimwengu lenye ukwasi zaidi sana, na Uingereza, kao la milki ya ulimwengu iliyo kubwa zaidi sana. Basi, hiki, ndicho ‘kichwa’ cha saba, au serikali kubwa ya ulimwengu, ambayo inaendelea mpaka ndani ya wakati wa mwisho na katika maeneo ambamo Mashahidi wa ki-siku-hizi wa Yehova walijiimarisha kwanza. Kikilinganishwa na utawala mrefu wa kichwa cha sita, hiki cha saba ‘chabaki kitambo kifupi’ mpaka Ufalme wa Mungu uangamizapo mataifa yote.

      Kwa Nini Huitwa Mfalme wa Nane?

      8, 9. Malaika anamwitaje hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu na ni katika njia gani huchipuka kutoka kwa wafalme saba?

      8 Malaika anamweleza Yohana zaidi hivi: “Na hayawani-mwitu ambaye alikuwako lakini hayuko, yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane, lakini huchipuka kutoka kwa wale saba, na yeye huenda zake ndani ya uharibifu.” (Ufunuo 17:11, NW) Hayawani-mwitu wa ufananisho rangi-nyekundu-nyangavu “huchipuka kutoka” kwa vichwa saba; yaani, yeye anazaliwa na, au yuko kwa sababu ya vichwa hivyo vya ‘hayawani-mwitu kutoka bahari,’ ambaye hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ni mfano wake. Kwa njia gani? Basi, katika 1919 serikali ya Uingereza-Amerika ilikuwa ndiyo kichwa chenye kutawala. Vile vichwa sita vilivyotangulia vilikuwa vimeanguka, nacho cheo cha serikali kubwa ya ulimwengu yenye kutawala kilikuwa kimepitishwa kwenye kichwa hiki cha uwili na sasa kikawa katika kitovu chacho. Hiki kichwa cha saba, kikiwa ndicho mwakilishi wa sasa wa mstari wa serikali za ulimwengu, kilikuwa ndicho kani yenye kutenda katika kusimamisha Ushirika wa Mataifa na kingali ndicho mwendelezaji na mtegemezaji kifedha mkuu wa Umoja wa Mataifa. Hivyo, kwa njia ya ufananisho hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu—mfalme wa nane—“huchipuka kutoka” kwa vile vichwa saba vya kwanza. Ikionwa katika njia hii, taarifa ya kwamba yeye alichipuka kutoka kwa vichwa saba inapatana vizuri na ufunuo wa mapema zaidi kwamba hayawani-mwitu mwenye pembe mbili mithili ya mwana-kondoo (Serikali ya Ulimwengu Uingereza-Amerika, kichwa cha saba cha hayawani-mwitu wa kwanza) alihimiza kufanyizwa kwa huo mfano na akaupa uhai.—Ufunuo 13:1, 11, 14, 15.

      9 Kwa kuongezea, washiriki wa kwanza kabisa wa Ushirika wa Mataifa walikuwamo, pamoja na Uingereza, serikali ambazo zilitawala katika makao ya baadhi ya vichwa vilivyotangulia, yaani, Ugiriki, Irani (Uajemi), na Italia (Roma). Hatimaye, serikali zenye kutawala maeneo yaliyodhibitiwa na serikali za ulimwengu sita zilizotangulia zikaja kuwa washiriki waungaji mkono wa mfano wa hayawani-mwitu. Katika maana hii, vilevile, ingeweza kusemwa kwamba huyu hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu alichipuka kutoka kwa serikali za ulimwengu saba.

      10. (a) Inaweza kusemwaje kwamba hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu “yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane”? (b) Kiongozi mmoja wa nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti alionyeshaje uungaji-mkono wake wa Umoja wa Mataifa?

      10 Angalia kwamba hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu “yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane.” Hivyo, Umoja wa Mataifa leo unakusudiwa uonekane kuwa serikali ya ulimwengu. Nyakati fulani hata umetenda hivyo, ukituma majeshi uwanjani kusuluhisha magomvi ya kimataifa, kama vile katika Korea, Peninsula ya Sinai, nchi fulani za Kiafrika, na Lebanoni. Lakini huo ni mfano tu wa mfalme. Kama vile mfano wa kidini, huo hauna uvutano au uwezo halisi isipokuwa ule ambao unapewa na wale ambao waliutokeza na wanaouabudu. Katika pindi fulani, hayawani-mwitu huyu wa ufananisho huonekana dhaifu; lakini hajapatwa kamwe na aina ya kuachwa kwa wingi na washiriki wenye maelekeo ya udikteta ambao walifanya Ushirika wa Mataifa utetereke na kutumbukia ndani ya abiso. (Ufunuo 17:8) Ingawa anashikilia maoni yanayotofautiana sana katika maeneo mengine, kiongozi mmoja mashuhuri wa nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti katika 1987 alijiunga na mapapa wa Roma katika kuonyesha uungaji-mkono wa UM. Yeye hata alitaka kuwe na “mfumo mpana wa usalama wa kimataifa” wenye kutegemea UM. Kama Yohana ajifunzavyo upesi, wakati utakuja ambapo UM utatenda kwa mamlaka kubwa. Kisha huo, katika zamu yao, “huenda zake ndani ya uharibifu.”

      Wafalme Kumi kwa Saa Moja

      11. Malaika wa Yehova anasema nini juu ya pembe kumi zilizo juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa ufananisho?

      11 Katika sura ya Ufunuo iliyotangulia, malaika, wa sita na wa saba walimimina mabakuli ya kasirani ya Mungu. Hivyo sisi tuliarifiwa kwamba wafalme wa dunia wanakusanywa kwenye vita ya Mungu kwenye Har–Magedoni na kwamba ‘Babuloni Mkubwa apaswa kukumbukwa katika mwono wa Mungu.’ (Ufunuo 16:1, 14, 19, NW) Sasa tutajifunza kirefu zaidi jinsi hukumu za Mungu juu ya hawa zitatekelezwa. Sikiliza tena malaika wa Yehova anaponena kwa Yohana. “Na pembe kumi ambazo wewe uliona humaanisha wafalme kumi, ambao bado kupokea ufalme, lakini wao hupokea mamlaka wakiwa wafalme saa moja pamoja na hayawani-mwitu. Hawa wana fikira moja, na hivyo wao humpa hayawani-mwitu nguvu na mamlaka yao. Hawa watapigana na Mwana-Kondoo, lakini, kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, Mwana-Kondoo atashinda wao. Pia, wale wenye kuitwa na wachaguliwa na waaminifu pamoja na yeye watafanya hivyo.”—Ufunuo 17:12-14, NW.

      12. (a) Pembe kumi ni picha ya nini? (b) Ni jinsi gani pembe kumi za ufananisho ‘hazikuwa zimepokea ufalme’? (c) Pembe kumi za ufananisho zinakuwaje na “ufalme” sasa, na ni kwa muda gani?

      12 Pembe kumi ni picha ya serikali zote za kisiasa ambazo zinatawala sasa katika mandhari ya ulimwengu na ambazo huunga mkono hayawani-mwitu. Ni nchi chache sana zilizoko sasa ambazo zilijulikana katika siku ya Yohana. Na zile zilizojulikana, kama Misri na Uajemi (Irani), leo zina muundo wa kisiasa ulio tofauti kabisa. Kwa sababu hiyo, katika karne ya kwanza, ‘pembe kumi hazikuwa zimepokea ufalme.’ Lakini sasa katika siku ya Bwana, zina “ufalme,” au mamlaka ya kisiasa. Milki kubwa-kubwa za kikoloni zilipoanguka, hasa tangu vita ya ulimwengu ya pili, mataifa mengi mapya yamezaliwa. Hizi, pamoja na serikali ambazo zimeimarika muda mrefu, lazima zitawale pamoja na hayawani-mwitu kwa kipindi kifupi—“saa moja” tu—kabla Yehova hajakomesha mamlaka zote za kisiasa za ulimwengu kwenye Har–Magedoni.

      13. Ni katika njia gani pembe kumi zina “fikira moja,” na hiyo huhakikisha mwelekeo gani kwa Mwana-Kondoo?

      13 Leo, utukuzo wa taifa ndio mojapo kani zenye nguvu zaidi sana zinazosukuma pembe kumi hizi. Zina “fikira moja” kwa kuwa hizo zinataka kuhifadhi enzi zao za kitaifa badala ya kukubali Ufalme wa Mungu. Hilo ndilo lilikuwa kusudi lao katika kuchangia Ushirika wa Mataifa na tengenezo la Umoja wa Mataifa katika ile mara ya kwanza—kuhifadhi amani ya ulimwengu na hivyo kulinda salama kuwako kwazo. Mwelekeo kama huo unahakikisha kwamba pembe kumi zitapinga Mwana-Kondoo, “Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme,” kwa sababu Yehova amekusudia kwamba Ufalme wake chini ya Yesu Kristo hivi karibuni utachukua mahali pa falme hizi.—Danieli 7:13, 14; Mathayo 24:30; 25:31-33, 46.

      14. Inawezekanaje kwa watawala wa ulimwengu kupigana na Mwana-Kondoo, na tokeo litakuwa nini?

      14 Bila shaka, watawala wa ulimwengu huu hawawezi kufanya kitu chochote dhidi ya Yesu mwenyewe. Yeye yumo mbinguni, mbali sana wasimoweza kumfikia. Lakini ndugu za Yesu, wabakio wa mbegu ya mwanamke, wangali duniani na inaonekana wazi wanaumizika. (Ufunuo 12:17) Nyingi za pembe zimekwisha onyesha uhasama mkali kuwaelekea, na katika njia hii zimepigana na Mwana-Kondoo. (Mathayo 25:40, 45) Ingawa hivyo, karibuni, wakati utakuja wa Ufalme wa Mungu ‘kuponda-ponda na kuweka mwisho kwenye falme hizi zote.’ (Danieli 2:44, NW) Ndipo, wafalme wa dunia watakuwa katika pigano hadi tamati pamoja na Mwana-Kondoo, kama tutakavyoona karibuni. (Ufunuo 19:11-21) Lakini hapa tunajifunza mambo ya kutosha kung’amua kwamba mataifa hayatafanikiwa. Ingawa hayo pamoja na hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa UM wana “fikira moja” yao, wao hawawezi kumshinda “Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme” aliye mkubwa, wala hawawezi kushinda “wale wenye kuitwa na wachaguliwa na waaminifu pamoja na yeye,” kutia ndani wafuasi wapakwa-mafuta wake ambao wangali duniani. Hawa pia watakuwa wamekwisha shinda kwa kushika ukamilifu katika kujibu mashtaka maovu ya Shetani.—Warumi 8:37-39; Ufunuo 12:10, 11.

      Kuteketeza Kahaba

      15. Malaika anasema nini juu ya kahaba na mwelekeo na tendo la pembe kumi na hayawani-mwitu kuelekea yeye?

      15 Watu wa Mungu sio peke yao wanaochukiwa na pembe kumi. Malaika sasa anavuta uangalifu wa Yohana kwenye kahaba: “Na yeye anasema kwangu mimi: ‘Maji ambayo wewe uliona, ambapo kahaba anaketi, humaanisha vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi. Na pembe kumi ambazo wewe uliona, na hayawani-mwitu, hizi zitachukia kahaba na zitafanya yeye kuwa mwenye kuteketezwa na mwenye uchi, na zitakula kabisa sehemu zake zenye mnofu na zitachoma yeye kabisa kabisa kwa moto.’”—Ufunuo 17:15, 16, NW.

      16. Ni kwa nini Babuloni Mkubwa hataweza kutegemea maji yake yamuunge mkono wa himaya wakati serikali za kisiasa zinapomgeukia?

      16 Kama vile Babuloni wa kale alivyotegemea ulinzi wa maji yake, Babuloni Mkubwa leo anategemea washiriki wake wengi mno “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi.” Kwa kufaa malaika huelekeza uangalifu wetu kwenye hao kabla ya kusimulia tukio lenye kugutusha: Serikali za kisiasa za dunia hii zitamgeukia kijeuri Babuloni Mkubwa. “Vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi” wote hao watafanya nini wakati huo? Tayari watu wa Mungu wanaonya Babuloni Mkubwa kwamba maji ya mto Eufrati yatakauka. (Ufunuo 16:12) Mwishowe maji hayo yatakauka kabisa. Hayo hayataweza kumpa kahaba kizee mwenye kunyarafisha tegemezo lolote lenye kufaa katika saa yake ya uhitaji ulio mkubwa zaidi sana.—Isaya 44:27; Yeremia 50:38; 51:36, 37.

      17. (a) Ni kwa sababu gani ukwasi wa Babuloni Mkubwa hautamwokoa? (b) Mwisho wa Babuloni Mkubwa utakuwaje wenye aibu kabisa? (c) Mbali na pembe kumi, au mataifa moja moja, ni nini kingine kinachojiunga katika jeuri dhidi ya Babuloni Mkubwa?

      17 Kwa hakika, ukwasi mkubwa mno wa vitu vya kimwili hautaweza kumwokoa Babuloni Mkubwa. Huenda hata ukaharakisha kuharibiwa kwake, kwa kuwa njozi huonyesha kwamba wakati hayawani-mwitu na pembe kumi wanapomwonyesha chuki yao watamvua majoho yake ya kifalme na vito vyake vyote vya thamani. Wao watapora ukwasi wake. ‘Wanamfanya kuwa uchi,’ wakifichua kiaibu tabia yake halisi. Mteketezo wee! Pia mwisho wake ni wenye aibu kabisa. Wanamharibu, na ‘kula sehemu zake zenye mnofu,’ wakimwacha mifupa mitupu isiyo na uhai. Mwishowe, wao ‘humchoma kabisa kabisa kwa moto.’ Yeye huchomwa kabisa kama mwenye ugonjwa wa tauni, bila hata maziko ya heshima! Si mataifa yale tu, kama yanavyowakilishwa na pembe kumi, yanayomharibu kahaba mkubwa, bali pia “hayawani-mwitu,” kumaanisha UM wenyewe, hujiunga nayo katika kuonyesha jeuri hii. Utatoa idhini yao ili dini bandia iharibiwe. Yaliyo mengi ya yale mataifa 190 na zaidi yaliyo ndani ya UM yameonyesha tayari, kwa kiolezo chayo cha kupiga kura, uhasama wayo kuelekea dini, hasa ile ya Jumuiya ya Wakristo.

      18. (a) Ni uwezekano gani wa mataifa kugeukia dini za Kibabuloni ambao tayari umeonekana? (b) Ni nini itakayokuwa sababu ya msingi ya shambulio la ujumla juu ya kahaba mkubwa?

      18 Ni kwa nini hayo yangemtenda kijeuri hivyo hawara wao wa zamani? Sisi tumeona katika historia ya hivi majuzi uwezekano kama huo wa kugeukia dini ya Kibabuloni. Upinzani rasmi wa kiserikali umepunguza sana uvutano wa dini katika nchi kama vile China na nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti. Katika maeneo ya Kiprotestanti ya Ulaya, ubaridi wenye kuenea pote na mashaka vimeyaacha makanisa yakiwa tupu, hivi kwamba karibu dini imekufa. Milki kubwa mno ya Kikatoliki imegawanywa na uasi na kutoafikiana ambavyo viongozi wake wameshindwa kutuliza. Ingawa hivyo, haitupasi kupoteza mwono wa uhakika wa kwamba hili shambulio la mwisho kabisa, la ujumla juu ya Babuloni Mkubwa linakuja likiwa wonyesho wa hukumu ya Mungu isiyobadilika juu ya kahaba mkubwa.

      Kufikiliza Fikira ya Mungu

      19. (a) Utekelezo wa hukumu ya Yehova dhidi ya kahaba mkubwa unaweza kutolewaje kielezi na hukumu yake dhidi ya Yerusalemu asi-imani katika 607 K.W.K.? (b) Hali ya ukiwa, ya kutokaliwa ya Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. ilitangulia kutoa tamathali ya nini kwa siku yetu?

      19 Yehova anatekelezaje hukumu hii? Hii inaweza kutolewa kielezi na tendo la Yehova dhidi ya watu wake waasi-imani katika nyakati za kale, ambao kuwahusu yeye alisema: “Katika manabii wa Yerusalemu mimi nimeona vitu vibaya sana, kufanya uzinzi na kutembea katika ubandia; na wao wameimarisha mikono ya watenda maovu ili kwamba isiwapase kurudi, kila mmoja kutoka ubaya wake mwenyewe. Kwangu mimi wao wote wamekuwa kama Sodoma, na wakaaji wake ni kama Gomora.” (Yeremia 23:14, NW) Katika 607 K.W.K., Yehova alitumia Nebukadneza ‘avue mavazi, atwae vitu vizuri, na aache uchi na bila nguo’ jiji hilo lenye uzinzi wa kiroho. (Ezekieli 23:4, 26, 29, NW) Yerusalemu la wakati huo lilikuwa kigezo cha Jumuiya ya Wakristo ya leo, na kama alivyoona Yohana katika njozi ya mapema zaidi, Yehova ataipa Jumuiya ya Wakristo na dini nyingine yote bandia adhabu inayofanana na hiyo. Ukiwa, hali ya kutokaliwa ya Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. huonyesha vile Jumuiya ya Wakristo ya kidini itakavyoonekana baada ya kuvuliwa ukwasi wayo na kufichuliwa kiaibu. Na sehemu inayobaki ya Babuloni Mkubwa haitakuwa afadhali.

      20. (a) Yohana anaonyeshaje kwamba kwa mara nyingine tena Yehova atatumia watawala wa kibinadamu kutekeleza hukumu? (b) “Fikira” ya Mungu ni nini? (c) Ni katika njia gani mataifa yatafikiliza “fikira moja,” yayo lakini kwa kweli ni fikira ya nani itatimizwa?

      20 Kwa mara nyingine tena Yehova anatumia watawala wa kibinadamu kutekeleza hukumu. “Kwa maana Mungu alitia hilo ndani ya mioyo yao kufikiliza fikira yake, hata kufikiliza fikira yao moja kwa kumpa ufalme wao hayawani-mwitu, mpaka hapo maneno ya Mungu yatakuwa yametimilizwa.” (Ufunuo 17:17, NW) “Fikira” ya Mungu ni nini? Kupangia wafishaji wa Babuloni Mkubwa waungane pamoja, ili kumharibu kabisa. Bila shaka, matilaba ya watawala katika kumshambulia yatakuwa kufikiliza “fikira moja” yao wenyewe. Wao watahisi kwamba ni kwa masilahi yao ya utukuzaji wa taifa kumgeukia huyo kahaba mkubwa. Huenda wakaja kuona kule kuendelea kwa dini iliyopangwa kitengenezo ndani ya mipaka yao kuwa tisho kwa enzi zao. Lakini Yehova atakuwa kwa kweli akiongoza mambo kwa werevu; wao watafikiliza fikira yake kwa kuharibu kwa dharuba moja adui yake mzinzi wa muda mrefu!—Linga Yeremia 7:8-11, 34.

      21. Kwa kuwa hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu atatumiwa katika kuharibu Babuloni Mkubwa, kwa wazi mataifa yatafanya nini kwa habari ya Umoja wa Mataifa?

      21 Ndiyo, mataifa yatatumia hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, Umoja wa Mataifa, katika kuharibu Babuloni Mkubwa. Wao hawatendi kwa utangulizi wao wenyewe, kwa maana Yehova hutia ndani ya mioyo yao “hata kufikiliza fikira moja yao kwa kumpa ufalme wao hayawani-mwitu.” Wakati ujapo, kwa wazi mataifa yataona uhitaji wa kuimarisha Umoja wa Mataifa. Itakuwa kana kwamba, wanaupa meno, wakiupa mamlaka yoyote na nguvu waliyo nayo ili kwamba uweze kugeukia dini bandia na kupiga vita kwa kufaulu dhidi yayo “mpaka hapo maneno ya Mungu yatakuwa yametimilizwa.” Hivyo, kahaba wa kale atakuja kwenye mwisho wake kabisa. Na apotelee mbali!

      22. (a) Kwenye Ufunuo 17:18, ni nini kinachoashiriwa kwa njia ambayo malaika humalizia ushahidi wake? (b) Mashahidi wa Yehova wanaitikiaje kufumbuliwa kwa fumbo hilo?

      22 Kana kwamba anakazia uhakika wa kutekelezwa kwa hukumu ya Yehova juu ya milki ya ulimwengu ya dini bandia, malaika anamalizia ushahidi wake kwa kusema: “Na mwanamke ambaye wewe uliona anamaanisha jiji kubwa ambalo lina ufalme juu ya wafalme wa dunia.” (Ufunuo 17:18, NW) Kama Babuloni wa wakati wa Belshaza, Babuloni Mkubwa “amepimwa uzani katika mizani na akapatikana anapungukiwa.” (Danieli 5:27, The New English Bible) Kufishwa kwake kutakuwa kwepesi na kwa kukata maneno. Nao Mashahidi wa Yehova wanaitikiaje kufumbuliwa kwa fumbo la kahaba mkubwa na la hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? Wao huonyesha bidii katika kupiga mbiu ya siku ya hukumu ya Yehova, huku wakijibu “kwa upendezi” watafutaji wa ukweli wenye mioyo myeupe. (Wakolosai 4:5, 6; Ufunuo 17:3, 7, NW) Kama vile sura yetu ifuatayo itakavyoonyesha, wote wenye kutamania kuokoka wakati kahaba mkubwa anapofishwa lazima watende, na kutenda chakachaka!

      [Picha katika ukurasa wa 252]

      Mfuatano wa Serikali Saba za Ulimwengu

      MISRI

      ASHURU

      BABULONI

      UMEDI-UAJEMI

      UGIRIKI

      ROMA

      UINGEREZA-AMERIKA

      [Picha katika ukurasa wa 254]

      “Yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane”

      [Picha katika ukurasa wa 255]

      Wakimgeuzia Mwana-Kondoo visogo vyao, “wao humpa hayawani-mwitu nguvu na mamlaka yao”

      [Picha katika ukurasa wa 257]

      Jumuiya ya Wakristo ikiwa ndiyo sehemu kuu ya Babuloni Mkubwa itashabihi Yerusalemu la kale kuwa gofu kabisa

  • Jiji Kubwa Lateketezwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 36

      Jiji Kubwa Lateketezwa

      Njozi ya 12—Ufunuo 18:1–19:10

      Habari: Anguko na uharibifu wa Babuloni Mkubwa; ndoa ya Mwana-Kondoo yatangazwa

      Wakati wa utimizo: Kutoka 1919 mpaka baada ya ile dhiki kubwa

      1. Ni nini kitakachotia alama mwanzo wa dhiki kubwa?

      CHA GHAFULA, chenye kugutusha, chenye kuteketeza—ndivyo kitakuwa kifo cha Babuloni Mkubwa! Kitakuwa mojapo matukio yenye msiba mkuu zaidi sana katika historia yote, kikifanyiza mwanzo wa “dhiki kubwa kama ambayo haijapata kutokea tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa, la, wala haitatukia tena.”—Mathayo 24:21, NW.

      2. Ingawa milki za kisiasa zimeinuka na zikaanguka, ni milki ya aina gani ambayo imedumu?

      2 Dini bandia imekuwapo kwa muda mrefu. Imekuwapo bila kikomo tangu siku za Nimrodi mwenye kiu cha damu ambaye alipinga Yehova na akaanzisha watu kujenga Mnara wa Babeli. Yehova alipovuruga ndimi za waasi hao na kuwatawanya juu ya dunia, dini bandia ya Babuloni ilienda pamoja nao. (Mwanzo 10:8-10; 11:4-9) Tangu hapo, milki za kisiasa zimeinuka na zikaanguka, lakini dini ya Kibabuloni imedumu. Imechukua sura na maumbo mengi, ikiwa milki ya ulimwengu ya dini bandia, Babuloni Mkubwa aliyetolewa unabii. Sehemu yake yenye kutokeza zaidi sana ni Jumuiya ya Wakristo, ambayo ilikua kutokana na mchanganyo wa mafundisho ya Kibabuloni ya mapema zaidi na mafundisho ya “Ukristo” ulioasi imani. Kwa sababu ya historia ndefu, ndefu mno ya Babuloni Mkubwa, watu wengi wanaliona kuwa jambo gumu kuitikadi kwamba itaangamizwa wakati wowote.

      3. Ufunuo unathibitishaje hukumu ya maangamizi ya dini bandia?

      3 Kwa hiyo inafaa kwamba yaupasa Ufunuo uthibitishe hukumu ya uangamivu wa dini bandia kwa kutupatia maelezo mawili yenye mambo mengi ya kuanguka kwake na matukio yanayofuata yakiongoza kwenye kufanywa ukiwa wake mkubwa. Sisi tumekwisha kumwona yeye akiwa ndiye “kahaba mkubwa” ambaye mwishowe anateketezwa na wale ambao hapo zamani walikuwa wapenzi wake wa milki ya kisiasa. (Ufunuo 17:1, 15, 16, NW) Sasa, katika njozi nyingine bado, sisi tutamwona akiwa jiji, kifananisho cha kidini cha Babuloni wa kale.

      Babuloni Mkubwa Aanguka

      4. (a) Yohana anafuata kuona njozi gani? (b) Sisi tunaweza kumtambuaje malaika, na ni kwa nini inamfaa yeye atangaze anguko la Babuloni Mkubwa?

      4 Yohana aendelea na simulizi, akituambia: “Baada ya vitu hivi mimi nikaona malaika mwingine akishuka kutoka katika mbingu, akiwa na mamlaka kubwa; na dunia ilinururishwa kutokana na utukufu wake. Na yeye akalia kwa sauti imara, kusema: ‘Yeye ameanguka! Babuloni Mkubwa ameanguka.’” (Ufunuo 18:1, 2a, NW) Hii ni mara ya pili kwa Yohana kusikia tangazo hilo la kimalaika. (Ona Ufunuo 14:8.) Hata hivyo, wakati huu umaana walo umekaziwa na utukufu wa huyo malaika wa kimbingu, kwa kuwa utukufu wake unanururisha dunia kwa ujumla! Yeye anaweza kuwa nani? Karne nyingi mapema nabii Ezekieli, akiripoti juu ya njozi ya kimbingu, alitaarifu kwamba “dunia yenyewe iling’aa kwa sababu ya utukufu [wa Yehova].” (Ezekieli 43:2, NW) Malaika pekee wa kung’aa kwa utukufu unaolinganika na wa Yehova angekuwa Bwana Yesu, ambaye ni “ule mrudisho wa utukufu [wa Mungu] na uwakilisho barabara wa kuwako kwake kwenyewe.” (Waebrania 1:3, NW) Katika 1914, Yesu alipata kuwa Mfalme mbinguni, na tangu wakati huo amekuwa akitumia mamlaka juu ya dunia akiwa Mfalme na Hakimu mshirika wa Yehova. Inafaa, basi, kwamba imempasa yeye atangaze kuanguka kwa Babuloni Mkubwa.

      5. (a) Malaika huyo anatumia nani kutoa habari ya anguko la Babuloni Mkubwa? (b) Hukumu ilipoanza juu ya wale wenye kudai kuwa “nyumba ya Mungu,” Jumuiya ya Wakristo ilikuwa hali gani?

      5 Malaika huyu mwenye mamlaka kubwa anatumia nani katika kutoa habari kama hizo zenye kushangaza mbele ya aina ya binadamu? Kwani, ni wale watu wenyewe ambao wanaachiliwa likiwa tokeo la anguko hilo, wale wapakwa-mafuta wabakio duniani, jamii ya Yohana. Kutoka 1914 mpaka 1918, hao waliteseka sana mikononi mwa Babuloni Mkubwa, lakini katika 1918 Bwana Yehova na “mjumbe wa agano [la Kiabrahamu]” wake, Yesu Kristo, alianza hukumu pamoja na “nyumba ya Mungu,” wale wenye kudai kuwa Wakristo. Hivyo Jumuiya ya Wakristo iliyoasi imani ililetwa kwenye jaribio. (Malaki 3:1; 1 Petro 4:17, NW) Hatia ya damu yayo kubwa mno iliyopata wakati wa vita ya ulimwengu ya kwanza, ushiriki wayo katika kunyanyasa mashahidi waaminifu wa Yehova, na itikadi zayo za Kibabuloni havikuisaidia katika wakati wa hukumu yayo; wala hapana sehemu nyingine yoyote ya Babuloni Mkubwa iliyostahili kibali cha Mungu.—Linga Isaya 13:1-9.

      6. Inaweza kusemwaje kwamba Babuloni Mkubwa alikuwa ameanguka kufikia 1919?

      6 Hivyo kufikia 1919 Babuloni Mkubwa alikuwa ameanguka, kufungulia njia watu wa Mungu waachiliwe na warudishwe, kana kwamba kwa siku moja, kwenye bara lao la ufanisi wa kiroho. (Isaya 66:8) Kufikia mwaka huo, Yehova Mungu na Yesu Kristo, Dario Mkubwa Zaidi na Sairasi Mkubwa Zaidi, walikuwa wameongoza mambo kwa werevu ili kwamba dini bandia isiweze tena kuwashikilia watu wa Yehova. Haingeweza tena kuwazuia wasimtumikie Yehova na kujulisha kwa wote ambao yamkini kusikia kwamba Babuloni Mkubwa aliye kama kahaba amehukumiwa uangamivu na kwamba kutetewa kwa enzi kuu ya Yehova kumekaribia karibu.—Isaya 45:1-4; Danieli 5:30, 31.

      7. (a) Ingawa Babuloni Mkubwa hakuharibiwa katika 1919, Yehova alimwonaje? (b) Babuloni Mkubwa alipoanguka katika 1919, tokeo lilikuwa nini kwa watu wa Yehova?

      7 Ni kweli, Babuloni Mkubwa hakuangamizwa katika 1919—kama vile jiji la Babuloni la kale halikuangamizwa katika 539 K.W.K. wakati lilipoanguka mikononi mwa majeshi ya Sairasi Mwajemi. Lakini kwa maoni ya Yehova, tengenezo hilo lilikuwa limeanguka. Yeye alikuwa amepata hukumu mbaya ya kimahakama, akingojea kufishwa; kwa hiyo dini bandia haingeweza kushikilia tena watu wa Yehova katika utekwa. (Linga Luka 9:59, 60.) Hao waliachiliwa wakatumikie wakiwa mtumwa mwaminifu na mwenye uangalifu wa Bwana-Mkubwa wakitoa chakula cha kiroho kwa wakati unaofaa. Wao walikuwa wamepokea hukumu ya ‘Mmefanya vema’ nao walipewa utume wajishughulishe tena na kazi ya Yehova.—Mathayo 24:45-47; 25:21, 23; Matendo 1:8, NW.

      8. Ni tukio gani ambalo mlinzi wa Isaya 21:8, 9 hupigia mbiu, na ni nani leo anayetolewa kivuli na mlinzi huyo?

      8 Mileani nyingi zilizopita Yehova alitumia manabii wengine watabiri tukio hili kubwa lenye kuanzisha muda maalumu. Isaya alisema juu ya mlinzi ambaye “aliendelea kuita kwa sauti kubwa kama simba: ‘Juu ya mnara wa lindo, O Yehova, mimi ninasimama daima mchana, na kwenye kilindio changu mimi nimewekwa mausiku yote.’” Na ni tukio gani analotambua mlinzi huyo na kupiga mbiu kwa ujasiri kama wa simba? Hili: “Yeye ameanguka! Babuloni ameanguka, na mifano yote ya kuchongwa ya miungu yake [Yehova] amevunja hadi kwenye dunia!” (Isaya 21:8, 9, NW) Mlinzi huyu anatolea kivuli vizuri jamii ya Yohana leo ambayo ni yenye kuamka kabisa, inapotumia gazeti Mnara wa Mlinzi na vichapo vingine vya kitheokrasi kuvumisha kotekote habari za kwamba Babuloni ameanguka.

      Mshuko wa Babuloni Mkubwa

      9, 10. (a) Uvutano wa dini ya Kibabuloni umepatwa na mpunguo gani tangu Vita ya Ulimwengu 1? (b) Malaika mwenye nguvu anaelezaje hali ya kuanguka ya Babuloni Mkubwa?

      9 Anguko la Babuloni wa kale katika 539 K.W.K. lilikuwa mwanzo wa mshuko mrefu ambao ulimalizikia katika ukiwa wake. Hali kadhalika, tangu vita ya kwanza ya ulimwengu, uvutano wa dini ya Kibabuloni umeshuka sana kwa kadiri ya tufe lote. Kufuata vita ya ulimwengu ya pili, ibada ya Shinto ya maliki ilikatazwa katika Japani. Katika China, serikali ya Kikomunisti hudhibiti uwekwaji rasmi na utendaji wote wa kidini. Katika Ulaya kaskazini ya Kiprotestanti, watu walio wengi wamekuwa wasiopendezwa na dini. Na hivi majuzi Kanisa Katoliki la Roma limedhoofishwa na mifarakano na kutopatana kwa ndani katika milki yalo ya tufe lote.—Linga Marko 3:24-26.

      10 Pasipo shaka miendo hii yote ni sehemu ya ‘kukauka kwa mto Eufrati’ katika kutayarishia shambulio linalokuja la kivita juu ya Babuloni Mkubwa. ‘Kukauka’ huku kunaonyeshwa, vilevile, katika tangazo la papa la Oktoba 1986 kwamba lazima kanisa ‘liwe mwomba-ombaji tena’—kwa sababu ya upungufu mkubwa mno. (Ufunuo 16:12) Hususa tangu 1919 Babuloni Mkubwa amekuwa akifichuliwa atazamwe na wote kuwa yeye ni bara-tupu la kiroho, kama malaika mwenye nguvu anavyotangaza hapa: “Na yeye amekuwa mahali pa kukaa roho waovu na mahali pa kujibanza kila pumzi isiyo safi na mahali pa kujibanza kila ndege asiye safi na mwenye kuchukiwa!” (Ufunuo 18:2b, NW) Karibuni atakuwa bara-tupu kama hilo kihalisi, akiwa ukiwa kama magofu ya Babuloni katika Iraki ya leo.—Ona pia Yeremia 50:25-28.

      11. Ni katika maana gani Babuloni Mkubwa amekuwa “mahali pa kukaa roho waovu” na ‘mahali pa kujibanza pumzi zisizo safi na pa ndege wasio safi’?

      11 Neno “roho waovu” hapa inaelekea ni mrudisho wa neno “roho waovu wenye umbo-mbuzi” (se‘i·rimʹ) linalopatikana katika elezo la Isaya kuhusu Babuloni aliyeanguka: “Na huko mizuka ya mikoa isiyo na maji kwa hakika italala chini, na nyumba zayo lazima zijawe na tai-bundi. Na huko mbuni lazima wakae, na roho waovu wenye umbo-mbuzi wenyewe wataenda wakirukaruka huko.” (Isaya 13:21, NW) Huenda isirejezee roho waovu halisi bali wanyama wakaa-jangwani wenye nywele za matimutimu ambao mwonekano wao ulifanya watazamaji wafikirie roho waovu. Katika magofu ya Babuloni Mkubwa, kuwako kitamathali kwa wanyama kama hao, pamoja na hewa tuli (“pumzi isiyo safi”) yenye sumu, na ndege wasio safi, huashiria hali yake ya kiroho iliyokufa. Yeye hatolei aina ya binadamu mataraja yoyote ya uhai.—Linga Waefeso 2:1, 2.

      12. Hali ya Babuloni Mkubwa hulandaje unabii wa Yeremia katika sura ya 50?

      12 Hali yake hulanda pia unabii wa Yeremia: “‘Kuna upanga dhidi ya Wakaldayo,’ ni tamko la Yehova, ‘na dhidi ya wakaaji wa Babuloni na dhidi ya wana-wafalme wake na dhidi ya wenye hekima wake. . . . Kuna mteketezo juu ya maji yake, na ni lazima yakaushwe kabisa. Kwa maana ni bara la mifano ya kuchongwa, na kwa sababu ya njozi zao zenye kujaa kikuli wao huendelea kutenda kikichaa. Kwa hiyo mizuka ya mikoa isiyo na maji itakaa pamoja na wanyama wenye kulia, na ndani yake yeye lazima mbuni wakae; naye hatakaliwa tena kamwe milele, wala yeye hatakaa kizazi baada ya kizazi.’” Ibada ya sanamu na kuimbwa kwa sala za kurudiwarudiwa hakuwezi kumwokoa Babuloni Mkubwa asipatwe na lipo linaloshabihi kuangushwa kwa Sodoma na Gomora na Mungu.—Yeremia 50:35-40, NW.

      Divai Yenye Kuamsha Harara

      13. (a) Malaika mwenye nguvu avutaje uangalifu kwenye mweneo mpana wa ukahaba wa Babuloni Mkubwa? (b) Ni utovu wa adili gani ulioenea sana katika Babuloni wa kale unaopatikana pia katika Babuloni Mkubwa?

      13 Kisha malaika mwenye nguvu anaelekeza uangalifu kwenye mweneo mpana wa ukahaba wa Babuloni Mkubwa, akipiga mbiu hivi: “Kwa sababu ya divai yenye kuamsha harara ya uasheratia wake mataifa yote yameanguka yakiwa majeruhi, na wafalme wa dunia walifanya uasherati na yeye, na wauza-bidhaa wasafiri wa dunia wakawa na utajiri kwa sababu ya nguvu za anasa yake isiyo ya aibu.” (Ufunuo 18:3, NW) Yeye amefundisha mataifa yote ya aina ya binadamu katika njia zake zisizo safi za kidini. Katika Babuloni wa kale, kulingana na mwanahistoria Herodoto, kila mwanamwali alitakwa aufanyize uasherati ubikira wake katika ibada ya hekalu. Kufikia leo hii ufisadi wa kingono wenye kukirihisha unaonyeshwa kitaswira katika sanamu-choro zilizoharibiwa na vita kwenye Angkor Wat katika Kampuchea na katika mahekalu katika Khajuraho, India, ambazo huonyesha mungu wa Kihindu Vishnu akizungukwa na mandhari za kimahaba zenye kunyarafisha. Katika United States, mafumbuo ya utovu wa adili ambayo yalitetemesha ulimwengu wa waevanjeli wa TV katika 1987, na tena katika 1988, pamoja na ufunuo wa zoea lenye kuenea pote la ugoni-jinsia-moja wa wahudumu wa kidini, hutoa kielezi kwamba hata Jumuiya ya Wakristo huvumilia mazidio yenye kugutusha ya uasherati halisi. Hata hivyo, mataifa yote yamekuwa majeruhi ya aina ya uasherati mbaya hata zaidi.

      14-16. (a) Ni uhusiano gani usio halali wa dini-siasa uliotukia katika Italia ya Ufashisti? (b) Wakati Italia ilipovamia Abisinia, ni taarifa gani walizotoa maaskofu wa Kanisa Katoliki la Roma?

      14 Sisi tumekwisha pitia uhusiano haramu wa dini-siasa uliomweka Hitla katika mamlaka katika Ujeremani ya Nazi. Mataifa mengine pia yalitaabika kwa sababu ya dini kujidukiza katika mambo ya kiserikali. Mathalani, Katika Italia ya Ufashisti, katika Februari 11, 1929, Mwafaka wa Laterani ulitiwa sahihi na Mussolini na Kardinali Gasparri, ukifanya Jiji la Vatikani kuwa dola lenye enzi. Papa Pius 11 alidai kwamba yeye alikuwa ‘ameirudisha Italia kwa Mungu, na Mungu akamrudisha kwa Italia.’ Je! huo ulikuwa ni ukweli? Fikiria yaliyotokea miaka sita baadaye. Katika Oktoba 3, 1935, Italia ilivamia Abisinia, ikidai kwamba lilikuwa “bara la kishenzi ambalo lilikuwa lingali linazoea utumwa.” Ni nani, kwa kweli, aliyekuwa wa kishenzi? Je! Kanisa Katoliki lililaumu vikali ushenzi wa Mussolini? Ingawa papa alitoa taarifa zisizoeleweka, maaskofu wake walisema wazi kabisa katika kubariki majeshi yenye silaha ya Italia “bara-baba” lao. Katika kitabu The Vatican in the Age of the Dictators, Anthony Rhodes huripoti hivi:

      15 “Katika Barua ya Uchungaji yake ya Oktoba 19 [1935], Askofu wa Udine [Italia] aliandika, ‘Si la wakati unaofaa wala lenye kufaa kwa sisi kutamka yanayofaa na yasiyofaa ya kisa hiki. Wajibu wetu tukiwa Waitalia, na hata hivyo zaidi tukiwa Wakristo ni kuchangia fanikio la silaha zetu.’ Askofu wa Padua aliandika katika Oktoba 21, ‘katika hizi saa ngumu ambazo sisi tunazipitia, sisi tunawaomba nyinyi mwe na imani katika watawala wetu na majeshi yenye silaha.’ Oktoba 24, Askofu wa Kremona aliweka wakfu bendera kadhaa za kijeshi na akasema: ‘Baraka ya Mungu na iwe juu ya askari-jeshi hawa ambao, juu ya udongo wa Kiafrika, watashinda mabara mapya na yenye rutuba kwa ajili ya ubunifu wa Italia, na hivyo kuwaletea utamaduni wa Kiroma na Kikristo. Italia na isimame kwa mara nyingine tena ikiwa mshauri wa ulimwengu kwa ujumla.’”

      16 Abisinia ikatwaliwa kinguvu, kwa baraka ya makasisi wa Katoliki ya Roma. Je! yeyote wa hawa angeweza kudai, katika maana yoyote, kwamba wao walikuwa kama mtume Paulo katika kuwa ‘bila hatia ya damu ya watu wote’?

      17. Hispania ilitesekaje kwa sababu ya viongozi wa kidini wayo kushindwa ‘kufua panga zao ziwe majembe ya plau’?

      17 Ongezea Ujeremani, Italia, na Abisinia taifa jingine ambalo limekuwa jeruhi kwa uasherati wa Babuloni Mkubwa—Hispania. Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe ya 1936-39 katika bara hilo, kwa sehemu, ilianzishwa kwa sababu ya serikali ya kidemokrasi kuchukua hatua ya kupunguza nguvu kubwa mno za Kanisa Katoliki la Roma. Vita hiyo ilipoanza, Franko, kiongozi Mfashisti Mkatoliki wa majeshi ya Kimapinduzi, alijieleza mwenyewe kuwa “Jenerali Mkuu wa Kikristo wa Krusedi Takatifu,” jina la cheo ambalo baadaye aliacha. Mamia ya maelfu kadhaa ya Wahispania walikufa katika kupigana. Mbali na hilo, kulingana na kadirio dogo, Wateteaji wa Taifa wa Franko walikuwa wameua kimakusudi wanachama 40,000 wa Popular Front, hali hao wa pili nao walikuwa wameua kimakusudi makasisi—watawa wa kiume, mapadri, watawa wa kike, na makasisi wapya 8,000. Hilo ndilo ogofyo na msiba wa vita ya wenyewe kwa wenyewe, ikionyesha hekima ya kutii maneno haya ya Yesu: “Rudisha upanga wako mahali pao, kwa maana wale wote ambao huchukua upanga watapotelea mbali kwa upanga.” (Mathayo 26:52, NW) Ni jambo lenye kunyarafisha kama nini kwamba Jumuiya ya Wakristo hujiingiza katika umwagaji-damu mkubwa hivyo! Kweli kweli viongozi wayo wa kidini wameshindwa kabisa kabisa ‘kufua panga zao ziwe majembe ya plau’!—Isaya 2:4, NW.

      Wauza-Bidhaa Wasafiri

      18. Ni nani walio “wauza-bidhaa wasafiri wa dunia”?

      18 Ni nani walio “wauza-bidhaa wasafiri wa dunia”? Pasipo shaka sisi tungewaita leo wachuuzi, wanabiashara wakubwa-wakubwa, walanguzi chapuchapu na biashara kubwa-kubwa. Hii si kusema kwamba ni kosa kufanya biashara halali. Biblia huandaa shauri la hekima kwa watu wa biashara, ikiwaonya dhidi ya utovu wa haki, pupa, na kadhalika. (Mithali 11:1; Zekaria 7:9, 10; Yakobo 5:1-5) Pato lililo kubwa zaidi ni “kujitoa kwa ajili ya Mungu pamoja na ujitoshelevu.” (1 Timotheo 6:6, 17-19, NW) Hata hivyo, ulimwengu wa Shetani haufuati kanuni za uadilifu. Ufisadi ni tele. Unapatikana katika dini, katika siasa—na katika biashara kubwa-kubwa. Wakati kwa wakati vyombo vya habari hufichua kashifa, kama vile maofisa wa serikali wa vyeo vya juu kutumia vibaya mali ya serikali na kuuza silaha kimagendo.

      19. Ni mambo hakika gani ya uchumi wa ulimwengu husaidia kueleza sababu kwa nini wauza-bidhaa wasafiri wa dunia hupata mtajo usiopendeleka katika Ufunuo?

      19 Uchuuzi wa kimataifa wa silaha unapanda juu sana kupita dola 1,000,000,000,000 kila mwaka, huku mamia ya mamilioni ya wanadamu wakinyimwa lazima za maisha. Hilo ni baya vya kutosha. Lakini silaha huonekana kuwa tegemezo la msingi la uchumi wa ulimwengu. Katika Aprili 11, 1987, makala moja katika Spectator ya London iliripoti hivi? “Kuhesabu viwanda vinavyohusiana moja kwa moja, kazi 400,000 zinahusika katika U.S. na 750,000 katika Ulaya. Lakini ajabu ni kwamba, kadiri daraka la kijamii na kiuchumi la kuunda silaha linavyoongezeka, lile swali hasa la kama waundaji wanakingwa vizuri limesahauliwa.” Faida kubwa mno zinapatikana kadiri mabomu na silaha nyinginezo zinachuuzwa kotekote duniani, hata na kwa wanaoweza kuwa maadui. Siku moja huenda mabomu hayo yakarudi katika mteketeo wa moto kuwaharibu wale wanaoyauza. Ni kinyume kama nini! Ongezea hilo ulanguzi unaohusika katika biashara hii ya silaha. Katika United States pekee, kulingana na Spectator, “kila mwaka kwa njia isiyoelezeka Pentagoni hupoteza silaha na vifaa vya thamani ya dola milioni 900.” Si ajabu kwamba wauza-bidhaa wa dunia wanatajwa isivyopendeleka katika Ufunuo!

      20. Ni kielelezo gani kinachoonyesha kujihusisha kwa dini katika mazoea yenye ufisadi ya shughuli za biashara?

      20 Kama ilivyotabiriwa na malaika mwenye utukufu, dini imehusika sana katika mazoea yenye ufisadi ya biashara. Mathalani, kuna kujihusisha kwa Vatikani katika anguko la Banco Ambrosiano katika 1982. Kesi hiyo imejikokota muda wote wa miaka ya 1980, lile swali ambalo halijajibiwa likiwa: Fedha zilienda wapi? Katika Februari 1987 mahakimu wa Milani walitoa waranti ili makasisi watatu wa Vatikani wakamatwe, kutia na askofu mkuu mmoja Mwamerika, kwa mashtaka ya kwamba wao walikuwa washiriki kwenye ufilisi wenye udanganyifu, lakini Vatikani ilitupilia mbali ombi la kuwakabidhi wakahukumiwe. Katika Julai 1987, katikati ya makelele ya kuteta, zile waranti zilibatilishwa na Mahakama ya Rufani ya juu zaidi sana kwa msingi wa mwafaka wa zamani kati ya Vatikani na serikali ya Italia.

      21. Sisi twajuaje kwamba Yesu hakuwa na uhusiano na mazoea ya kibiashara yenye kutilika mashaka ya siku yake, lakini sisi tunaona nini leo katika dini ya Kibabuloni?

      21 Je! Yesu alijihusisha katika mazoea ya kibiashara yenye kutilika mashaka ya siku yake? La. Yeye hata hakuwa mwenye mali yoyote, kwa maana yeye alikuwa “hana mahali pa kulaza chini kichwa chake.” Mtawala mmoja kijana tajiri alishauriwa na Yesu hivi: “Uza vitu vyote ulivyo navyo na kugawia maskini, na wewe utakuwa na hazina katika mbingu; na uje uwe mfuasi wangu.” Hilo lilikuwa shauri jema, kwa maana lingaliweza kumwondolea mbali wasiwasi wote juu ya mambo ya kibiashara. (Luka 9:58; 18:22, NW) Kwa kutofautisha, dini ya Kibabuloni mara nyingi ina mafungamano mabaya na biashara kubwa-kubwa. Mathalani, katika 1987 Albany Times Union liliripoti kwamba msimamizi wa mambo ya kifedha wa akidayosisi ya Miami, Florida, U.S.A., alikubali kwamba kanisa lina hisa katika makampuni ambayo hufanyiza silaha za nyukilia, sinema zisizofaa, na sigareti.

      “Ondokeni Katika Yeye, Watu Wangu”

      22. (a) Sauti kutoka katika mbingu inasema nini? (b) Ni nini kilichoongoza kwenye mshangilio wa watu wa Mungu katika 537 K.W.K., na katika 1919?

      22 Maneno yanayofuata ya Yohana yanaelekeza kwenye utimizo zaidi wa kigezo cha kiunabii: “Na mimi nikasikia sauti nyingine kutoka katika mbingu ikisema: ‘Ondokeni katika yeye, watu wangu, ikiwa nyinyi hamtaki kushiriki pamoja na yeye katika madhambi yake, na ikiwa nyinyi hamtaki kupokea sehemu ya tauni zake.’” (Ufunuo 18:4, NW) Unabii wa anguko la Babuloni wa kale katika Maandiko ya Kiebrania unatia ndani pia amri ya Yehova kwa watu wake: “Kimbieni mtoke katikati ya Babuloni.” (Yeremia 50:8, 13, NW) Hali moja na hiyo, kwa sababu ya ukiwa unaokuja wa Babuloni Mkubwa, watu wa Mungu wanahimizwa sasa waponyoke. Katika 537 K.W.K. fursa ya kuponyoka kutoka Babuloni ilileta mshangilio mkubwa upande wa Waisraeli waaminifu. Katika njia iyo hiyo, kuachiliwa kwa watu wa Mungu kutoka utekwa wa Babuloni Mkubwa kuliongoza kwenye mshangilio upande wao. (Ufunuo 11:11, 12) Na tangu wakati huo mamilioni ya wengine yametii amri hiyo wakimbie.

      23. Sauti kutoka katika mbingu inakaziaje umuhimu wa kukimbia kutoka katika Babuloni Mkubwa?

      23 Je! ni jambo la muhimu kweli kweli kadiri hiyo kukimbia kutoka katika Babuloni Mkubwa, kujiondoa katika uanachama wa dini za ulimwengu na kujitenga kabisa? Ndivyo, kwa maana sisi tunahitaji kuchukua oni la Mungu juu ya dubwana hili la kale la kidini, Babuloni Mkubwa. Yeye hakuepa kumwita kahaba mkubwa. Kwa hiyo sasa sauti kutoka katika mbingu inamwarifu Yohana zaidi hivi kuhusu malaya huyu: “Kwa maana madhambi yake yametungamana pamoja moja kwa moja hadi kwenye mbingu, na Mungu amekumbuka matendo yake yasiyo ya haki. Rudisha kwa yeye hata kama vile yeye mwenyewe alirudisha, na fanya kwa yeye mara mbili ya vile yeye alifanya, ndiyo, mara mbili ya hesabu ya alivyofanya; katika kikombe ambacho ndani yacho yeye aliweka mchanganyiko wekea yeye mara mbili ya mchanganyiko huo. Kwa kadiri ambayo yeye alijitukuza mwenyewe na akaishi katika anasa ya kutoona aibu, kwa kadiri hiyo mpe yeye teso na ombolezo. Kwa maana katika moyo wake yeye hufuliza kusema, ‘Mimi naketi nikiwa malkia, na mimi si mjane, na mimi sitaona kamwe ombolezo.’ Hiyo ndiyo sababu katika siku moja tauni zake zitakuja, kifo na ombolezo na njaa kuu, na yeye atachomwa kabisa kwa moto, kwa sababu Yehova Mungu, ambaye alihukumu yeye, ni imara sana.”—Ufunuo 18:5-8, NW.

      24. (a) Ni lazima watu wa Mungu wakimbie kutoka Babuloni Mkubwa ili waepuke nini? (b) Wale wanaoshindwa kukimbia kutoka katika Babuloni Mkubwa wanashiriki naye madhambi gani?

      24 Ni maneno yenye nguvu, hayo! Kwa hiyo tendo linatakwa. Yeremia alihimiza watu katika siku yake watende, akisema: “Kimbieni kutoka katikati ya Babuloni, . . . kwa maana ni wakati wa kisasi ambacho ni cha Yehova. Kuna tendeo ambalo yeye analipa kurudisha kwa yeye. Ondokeni katikati yake, O watu wangu, na kila mmoja aandalilie nafsi yake mponyoko kutoka kasirani yenye kuwaka ya Yehova.” (Yeremia 51:6, 45, NW) Katika njia kama hiyo, sauti kutoka katika mbingu inaonya watu wa Mungu leo wakimbie kutoka Babuloni Mkubwa ili wasipokee sehemu ya tauni zake. Hukumu za Yehova zilizo kama tauni juu ya ulimwengu huu, kutia na Babuloni Mkubwa, zinapigiwa mbiu sasa. (Ufunuo 8:1–9:21; 16:1-21) Watu wa Mungu wanahitaji kujitenga wenyewe na dini bandia ikiwa wao wenyewe hawataki kupatwa na tauni hizi na mwishowe kabisa wafe naye. Waaidha, kubaki ndani ya tengenezo hilo kungewafanya washiriki katika madhambi yake. Wao wangekuwa na hatia kama yeye ya uzinzi wa kiroho na ya kumwaga damu “ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.”—Ufunuo 18:24, NW; linga Waefeso 5:11; 1 Timotheo 5:22.

      25. Ni katika njia zipi watu wa Mungu waliondoka katika Babuloni wa kale?

      25 Ingawa hivyo, ni jinsi gani watu wa Mungu huondoka katika Babuloni Mkubwa? Katika kisa cha Babuloni wa kale, Wayahudi walikuwa sharti wafanye safari halisi kutoka katika jiji la Babuloni moja kwa moja hadi Bara la Ahadi. Lakini zaidi ya hilo lilihusika. Kiunabii Isaya aliambia Waisraeli hivi: “Geukeni mbali, geukeni mbali, ondokeni humo, msiguse kitu kisicho safi; ondokeni katikati yake, jitunzeni wenyewe safi, nyinyi ambao mnapeleka vyombo vya Yehova.” (Isaya 52:11, NW) Ndiyo, wao walipaswa waache mazoea yote yasiyo safi ya dini ya Kibabuloni ambayo yangeelekea kuitia kutu ibada yao kwa Yehova.

      26. Wakristo Wakorintho walitiije maneno haya, ‘Ondokeni kutoka miongoni mwao na mwache kabisa kugusa kitu kisicho safi’?

      26 Mtume Paulo alinukuu maneno ya Isaya katika barua yake kwa Wakorintho, akisema: “Msipate kuwa wenye kufungiwa nira isivyofaa pamoja na wasioitikadi. Kwa maana ni ushirika gani uadilifu unao pamoja na ukosefu wa kutii sheria? Au ni hisa gani nuru inayo pamoja na giza? . . . ‘Kwa hiyo ondokeni kutoka miongoni mwao, na kujitenga nyinyi wenyewe,’ asema Yehova, ‘Na acheni kabisa kugusa kitu kisicho safi.’” Haikuwa lazima Wakristo wa Korintho waache Korintho ili watii amri hiyo. Hata hivyo, wao walikuwa na lazima ya kuepuka kihalisi mahekalu yasiyo safi ya dini bandia, pamoja na kujitenga wenyewe kiroho na matendo yasiyo safi ya waabudu sanamu hao. Katika 1919 watu wa Mungu walianza kukimbia kutoka katika Babuloni Mkubwa kwa njia hiyo, wakijisafisha wenyewe mabaki yoyote ya mafundisho na mazoea yasiyo safi. Hivyo, waliweza kutumikia yeye wakiwa watu wake waliosafishwa.—2 Wakorintho 6:14-17, NW; 1 Yohana 3:3.

      27. Ni milingano gani iliyopo kati ya hukumu juu ya Babuloni wa kale na juu ya Babuloni Mkubwa?

      27 Anguko la Babuloni wa kale na ukiwa uliofuata lilikuwa adhabu kwa ajili ya madhambi yake. “Kwa maana moja kwa moja hukumu zake zimefika katika zile mbingu.” (Yeremia 51:9, NW) Hali moja na hiyo, madhambi ya Babuloni Mkubwa “yametungamana pamoja moja kwa moja hadi kwenye mbingu,” ili ziangaliwe na Yehova mwenyewe. Yeye ana hatia ya utovu wa haki, ibada ya sanamu, utovu wa adili, uonevu, unyakuzi, na uuaji kimakusudi. Anguko la Babuloni wa kale lilikuwa kwa sehemu, kisasi kwa yale ambayo lilikuwa limefanyia hekalu la Yehova na waabudu wa kweli wake. (Yeremia 50:8, 14; 51:11, 35, 36) Anguko la Babuloni Mkubwa na uharibifu wake utakaofuata hali moja na hiyo huonyesha kisasi kwa yale ambayo yeye amefanyia waabudu wa kweli katika muda wote wa karne zilizopita. Kweli kweli, uharibifu wake wa mwisho kabisa ni mwanzo wa “siku ya kisasi upande wa Mungu wetu.”—Isaya 34:8-10; 61:2, NW; Yeremia 50:28.

      28. Ni kiwango gani cha haki anachotumia Yehova kwa Babuloni Mkubwa, na kwa sababu gani?

      28 Chini ya Sheria ya Musa, ikiwa Mwisraeli aliiba kutoka wananchi wenzake, alikuwa sharti alipe ili kurudisha angalau maradufu katika kufidia. (Kutoka 22:1, 4, 7, 9) Katika uharibifu unaokuja wa Babuloni Mkubwa, Yehova atatumia kiwango kinacholinganika na hicho cha haki. Yeye atapokea maradufu ya yale aliyotoa. Hakutakuwa na rehema kwa sababu Babuloni Mkubwa hakuonyesha rehema yoyote kwa majeruhi wake. Yeye alijilisha kidusia juu ya watu wa dunia ili kujidumisha mwenyewe katika “anasa ya kutoona aibu.” Sasa yeye atateseka na kuomboleza. Babuloni wa kale alihisi alikuwa katika hali ya usalama kabisa, akijigamba: “Mimi sitaketi kama mjane, na mimi sitajua hasara ya watoto.” (Isaya 47:8, 9, 11, NW) Babuloni Mkubwa huhisi yu salama. Lakini uharibifu wake, ulioamriwa na Yehova ambaye “ni imara sana,” utatukia chakachaka, kana kwamba “katika siku moja”!

      [Maelezo ya Chini]

      a New World Translation Reference Bible, kielezi cha chini.

      [Sanduku katika ukurasa wa 263]

      “Wafalme . . . Walifanya Uasherati na Yeye”

      Mapema katika miaka ya 1800 wauza-bidhaa wa Ulaya walikuwa wakiingiza kimagendo ndani ya China viasi vikubwa vya kasumba. Katika Machi 1839 maofisa Wachina walijaribu kukomesha uchuuzi huo usio halali kwa kukamata masanduku 20,000 ya dawa hiyo ya kulevya kutoka kwa wauza-bidhaa Waingereza. Hili liliongoza kwenye wasiwasi kati ya Uingereza na China. Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yalipozorota, baadhi ya wamisionari Waprotestanti walihimiza Uingereza kwenda vitani, kwa taarifa kama hizi zifuatazo:

      “Jinsi magumu haya yanavyoshangilisha moyo wangu kwa sababu mimi nafikiri huenda serikali ya Uingereza ikakasirishwa vikali, na Mungu, katika nguvu Zake huenda akavunjavunja migogoro inayozuia gospeli ya Kristo isiingie China.”—Henrietta Shuck, misionari wa Baptisti ya Kusini.

      Hatimaye, vita ikafyatuka—vita ambayo leo hujulikana kuwa Vita ya Kasumba. Kwa moyo wote wamisionari walichochea Uingereza kwa maelezo kama haya:

      “Mimi nalazimika kutazama nyuma juu ya hali ya sasa ya mambo sana sana si kuwa ni shauri la kasumba au la Uingereza, kuwa ndilo kusudi kubwa la Mwelekezo wa Kimungu ili kufanya uovu wa mwanadamu utii makusudi Yake ya rehema kuelekea China katika kupenya ukuta wayo wa kujitenga.”—Peter Parker, misionari Mkongrigeshonali.

      Misionari mwingine Mkongrigeshonali, Samuel W. Williams, aliongeza hivi: “Mkono wa Mungu ni wazi katika yale yote ambayo yamefanyika kwa jinsi ya kutokeza, na sisi hatutii shaka kwamba Yeye ambaye alisema alikuja kuleta upanga juu ya dunia amekuja hapa na kwamba ni kwa ajili ya uharibifu mwepesi wa maadui Wake na kusimamishwa kwa ufalme Wake. Yeye atapindua na kupindua mpaka Yeye awe amemthibitisha Mwana-Mfalme wa Amani.”

      Kwa mintarafu ya chinjo lenye kuogofya la wanataifa Wachina, misionari J. Lewis Shuck aliandika: “Mimi huona mandhari kama hizo . . . kuwa ala za Bwana za moja kwa moja katika kuondolea mbali takataka ambayo inazuia usongaji mbele wa Ukweli wa Kimungu.”

      Misionari Mkongrigeshonali Elijah C. Bridgman aliongeza: “Mara nyingi Mungu ametumia mkono imara wa mamlaka ya kiserikali ili kutayarisha njia kwa ajili ya ufalme Wake . . . Chombo katika nyakati hizi zenye maana ni cha kibinadamu; nguvu yenye kuelekeza ni ya kimungu. Gavana mkuu wa mataifa yote ametumia Uingereza kuadhibu na kunyenyekeza China.”—Manukuu yamechukuliwa kutoka “Ends and Means,” 1974, insha ya Stuart Creighton Miller iliyotangazwa katika The Missionary Enterprise in China and America (Durusi la Harvard lililohaririwa na John K. Fairbank).

      [Picha katika ukurasa wa 264]

      “Wauza-Bidhaa Wasafiri . . . Wakawa na Utajiri”

      “Kati ya 1929 na mfyatuko wa Vita ya Ulimwengu 2, [Bernadino] Nogara [msimamizi wa mambo ya kifedha wa Vatikani] aligawia Vatikani jiji kuu na mawakili wa Vatikani kufanya kazi katika maeneo ya namna namna ya uchumi wa Italia—hasa katika nguvu za umeme, mawasiliano ya simu, karidhi na kazi za benki, njia za reli ndogondogo, na ufanyizaji wa zana za kilimo, saruji, na nyuzi za nguo za kubuniwa. Nyingi za shughuli hizi zilifanikiwa.

      “Nogara alinyakua kampuni kadhaa kutia na La Società Italiana della Viscosa, La Supertessile, La Società Meridionale Industrie Tessili, na La Cisaraion. Akiunganisha hizi kuwa kampuni moja, ambayo aliita CISA-Viscosa na akaiweka chini ya usimamizi wa Baron Francesco Maria Oddasso, mmojapo makabwela wa Vatikani wenye kuitibariwa zaidi sana, kisha Nogara akaongoza mambo kwa werevu ili kampuni hiyo mpya itwaliwe na [kampuni] ya Italia iliyo kubwa zaidi sana ya kufanyiza nguo, SNIA-Viscosa. Hatimaye faida za Vatikani katika SNIA-Viscosa zikakua zikawa kubwa zaidi na zaidi, na baada ya wakati Vatikani ikachukua udhibiti—kama inavyoshuhudiwa na uhakika wa kwamba baadaye Baron Oddasso akawa makamu wa msimamizi.

      “Ndivyo Nogara akapenya ndani ya kiwanda cha nguo. Yeye alipenya ndani ya viwanda vingine katika njia nyingine nyingine, kwa maana Nogara alikuwa mwenye vitimbi vingi. Mtu huyu asiye na ubinafsi . . . pengine alifanya mengi zaidi kutia uhai katika uchumi wa Italia kuliko mwanabiashara mwingine yeyote mmoja katika historia ya Italia . . . Benito Mussolini hakuweza kamwe kupata kabisa milki ambayo yeye aliotea ndoto, lakini yeye aliwezesha Vatikani na Bernadino Nogara kubuni utawala wa aina nyingine.”—The Vatican Empire, cha Nino Lo Bello, kurasa 71-3.

      Hiki ni kielelezo kimoja tu cha ushirikiano wa karibu karibu kati ya wauza-bidhaa wa dunia na Babuloni Mkubwa. Si ajabu kwamba wauza-bidhaa hawa wataomboleza wakati mshirika wao wa kibiashara atakapokuwa hayupo tena!

      [Picha katika ukurasa wa 259]

      Wanadamu walipoenea katika dunia yote, walichukua dini ya Kibabuloni pamoja nao

      [Picha katika ukurasa wa 261]

      Jamii ya Yohana, kama mlinzi, hupiga mbiu kwamba Babuloni ameanguka

      [Picha katika ukurasa wa 266]

      Magofu ya Babuloni wa kale yanaonya kimbele juu ya angamio linalokuja la Babuloni Mkubwa

  • Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 37

      Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni

      1. “Wafalme wa dunia” watatendaje kwa kuitikia uharibifu wa ghafula wa Babuloni Mkubwa?

      MWISHO wa Babuloni ni habari njema kwa watu wa Yehova, lakini mataifa yanauonaje? Yohana anatuambia: “Na wafalme wa dunia ambao walifanya uasherati na yeye na wakaishi katika anasa yenye utovu wa aibu watatoa machozi na kujipigapiga wenyewe kwa kihoro juu yake, wanapotazama moshi kutoka kuchomwa kwake, huku wao wakisimama mbali kwa sababu ya hofu yao ya teso lake na kusema, ‘Ni vibaya mno, ni vibaya mno, wewe jiji kubwa, Babuloni wewe jiji imara, kwa sababu katika saa moja hukumu yako imewasili!’”—Ufunuo 18:9, 10, NW.

      2. (a) Kwa kuwa pembe kumi za ufananisho za hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu zitamharibu Babuloni Mkubwa, ni kwa nini “wafalme wa dunia” wanahuzunikia mwisho wake? (b) Ni kwa nini hao wafalme wenye kihoro husimama mbali na jiji lililohukumiwa maangamizi?

      2 Tendo-mwitikio la mataifa huenda likaonekana kuwa la kushangaza kwa sababu ya uhakika wa kwamba Babuloni aliharibiwa na zile pembe kumi za ufananisho za hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu. (Ufunuo 17:16) Lakini Babuloni atakapokuwa hayupo, kwa wazi “wafalme wa dunia” watang’amua jinsi alivyokuwa mwenye mafaa kwao katika kutuliza watu na kuwatiisha. Viongozi wa kidini wamejulisha wazi vita kuwa vitakatifu, wakatenda wakiwa mawakili wa kuandikisha askari-jeshi, na wakahubiri vijana waingie katika mapigano. Dini imeandaa kisetiri cha utakatifu ambacho nyuma yacho watawala wafisadi wameendesha mambo katika kukandamiza makabwela. (Linga Yeremia 5:30, 31; Mathayo 23:27, 28.) Hata hivyo, angalia kwamba wafalme hawa wenye kihoro sasa wanasimama mbali na hilo jiji lenye kuhukumiwa maangamizi. Wao hawakaribii vya kutosha ili kuliauni. Wao wanahuzunikia kuona linaenda lakini hawahuzuniki vya kutosha kujihatarisha kwa ajili yalo.

      Wauza-Bidhaa Watoa Machozi na Kuomboleza

      3. Ni nani wengine wanaojutia kupita kwa Babuloni Mkubwa, na Yohana hutoa sababu zipi juu ya hilo?

      3 Wafalme wa dunia sio pekee wanaojutia kupita kwa Babuloni Mkubwa. “Pia, wauza-bidhaa wasafiri wa dunia wanatoa machozi na kuomboleza juu ya yeye, kwa sababu hakuna wa kununua tena bidhaa yao kamili, bidhaa kamili ya dhahabu na fedha na jiwe la thamani na lulu na kitani nzuri na zambarau na hariri na rangi-nyekundu-nyangavu; na kila kitu katika mbao zenye kutiwa manukato na kila aina ya kitu cha meno ya tembo na kila aina ya kitu kutokana na mbao iliyo ya thamani kubwa zaidi sana na cha shaba na cha chuma na cha marimari; pia mdalasini na vikolezo vya Kihindi na uvumba na mafuta yaliyotiwa harufu nzuri na ubani na divai na mafuta ya zeituni na unga safi sana na ngano na ng’ombe na kondoo, na farasi na makochi na watumwa na nafsi za kibinadamu. Ndiyo, na tunda zuri ambalo nafsi yako ilitamani limeondoka kutoka kwa wewe [Babuloni Mkubwa], na vitu vitamu-vitamu vyote na vitu vya umaridadi vimepotelea mbali kutoka kwa wewe, na watu hawatavipata tena kamwe.”—Ufunuo 18:11-14, NW.

      4. Ni kwa nini “wauza-bidhaa wasafiri” hutoa machozi na kuombolezea mwisho wa Babuloni Mkubwa?

      4 Ndiyo, Babuloni Mkubwa alikuwa rafiki ya karibu na mteja mwema wa wauza-bidhaa wenye ukwasi. Mathalani, kwa muda wa karne zilizopita nyumba za watawa-waume, nyumba za watawa wa kike na makanisa ya Jumuiya ya Wakristo zimejipatia kiasi kikubwa mno cha dhahabu, fedha, mawe ya thamani, mbao za thamani, na namna nyinginezo za ukwasi wa vitu vya kimwili. Na zaidi, baraka ya kidini imetolewa juu ya shamrashamra za ununuzi wa kianasa na karamu za ulafi, ulevi na uasherati zinazoandamana na mwadhimisho wa Krismasi wenye kuvunjia Kristo heshima na siku nyinginezo zinazoitwa eti takatifu. Wamisionari wa Jumuiya ya Wakristo wamepenya ndani ya mabara ya mbali, wakafungua masoko mapya kwa ajili ya “wauza-bidhaa wasafiri” wa ulimwengu huu. Katika Japani ya karne ya 17, Ukatoliki, uliokuja pamoja na wachuuzi hata ulijihusisha katika vita vyenye uhasama wa daima. Ikiripoti juu ya vita yenye kukata maneno chini ya kuta za ngome ya Osaka, The Encyclopædia Britannica hutaarifu hivi: “Vikosi vya Tokugawa vilijikuta vikipigana dhidi ya adui ambaye bendera zake zilikuwa zimepambwa kwa msalaba na mifano ya Mwokozi na ya [Mt.] James, mtakatifu mfadhili wa Hispania.” Chamkano yenye kushinda ilinyanyasa na karibu imalize Ukatoliki katika bara hilo. Ushiriki wa kanisa katika mambo ya ulimwengu leo vilevile hautaliletea baraka.

      5. (a) Sauti kutoka katika mbingu inaelezaje zaidi kuomboleza kwa hao “wauza-bidhaa wasafiri”? (b) Ni kwa nini wauza-bidhaa ‘wanasimama mbali’ pia?

      5 Sauti kutoka katika mbingu inasema zaidi hivi: “Wauza-bidhaa wasafiri wa vitu hivi, ambao wakawa na utajiri kutokana na yeye, watasimama mbali kwa sababu ya hofu yao ya teso lake na watatoa machozi na kuomboleza, kusema, ‘Ni vibaya mno, ni vibaya mno—jiji kubwa, lililovikwa kitani nzuri na zambarau na rangi-nyekundu-nyangavu, na kurembwa kitajiri kwa madoido ya dhahabu na jiwe la thamani na lulu, kwa sababu katika saa moja utajiri mwingi hivyo umeteketezwa!’” (Ufunuo 18:15-17a, NW) Kwa sababu ya kuharibiwa kwa Babuloni Mkubwa, “wauza-bidhaa” wanaombolezea hasara ya mshirika wa kibiashara huyo. Kwa kweli, “ni vibaya mno, ni vibaya mno” kwao. Hata hivyo, angalia kwamba sababu za kuomboleza kwao ni za ubinafsi kabisa na kwamba wao—kama vile wafalme—‘husimama mbali.’ Wao hawakaribii sana vya kutosha ili wasaidie Babuloni Mkubwa.

      6. Sauti kutoka katika mbingu inaelezaje kuomboleza kwa makapteni wa meli na mabaharia, na ni kwa nini wao hutoa machozi?

      6 Simulizi laendelea: “Na kila kapteni wa meli na kila mtu ambaye husafiri kwa meli kokote, mabaharia na wale wote ambao hupata riziki kwa bahari, walisimama mbali na kupiga kilio kikuu walipotazama moshi wa kuchomwa kwake na kusema, ‘Ni jiji gani lililo kama jiji kubwa?’ Na wao wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao na kupiga kilio kikuu, wakitoa machozi na kuomboleza, na wakasema, ‘Ni vibaya mno, ni vibaya mno—jiji kubwa, ambalo katika hilo wale wote wenye mashua kwenye bahari, wakawa na utajiri kwa sababu ya ughali walo, kwa kuwa katika saa moja limeteketezwa!’” (Ufunuo 18:17b-19, NW) Babuloni wa kale alikuwa jiji la kibiashara na alikuwa na kundi kubwa la meli. Hali moja na hiyo, Babuloni Mkubwa hufanya biashara nyingi sana kwa kutumia “maji mengi” ya watu wake. Hiyo huandaa kuajiriwa kwa raia wake wengi wa kidini. Uharibifu wa Babuloni Mkubwa utakuwa dharuba ya kiuchumi kama nini kwa watu hawa! Hakutakuwa kamwe na chimbuko jingine la riziki kama yeye.

      Kushangilia Juu ya Utowesho Wake

      7, 8. Sauti kutoka katika mbingu inafikiaje upeo wa ujumbe wayo kuhusu Babuloni Mkubwa, na ni nani watakaoitikia maneno hayo?

      7 Babuloni wa kale alipopinduliwa na Wamedi na Waajemi, Yeremia alisema kiunabii hivi: “Na juu ya Babuloni mbingu na dunia na wale wote walio ndani yazo kwa hakika watapiga kilio kikuu kwa kushangilia.” (Yeremia 51:48, NW) Wakati Babuloni Mkubwa aharibiwapo, sauti kutoka katika mbingu inafikisha ujumbe wayo kwenye upeo kwa kusema juu ya Babuloni Mkubwa hivi: “Uwe na nderemo juu yake, O mbingu, pia nyinyi watakatifu na nyinyi mitume na nyinyi manabii, kwa sababu kwa hukumu Mungu ametoza adhabu kutoka kwake kwa ajili ya nyinyi!” (Ufunuo 18:20, NW) Yehova na malaika watapendezwa sana kuona utowesho wa adui wa kale wa Mungu, kama vile watakavyopendezwa mitume na wale manabii Wakristo wa mapema, ambao kwa sasa wamefufuliwa na wamechukua cheo chao katika ule mpango wa wazee 24.—Linga Zaburi 97:8-12.

      8 Kweli kweli, “watakatifu” wote,—wawe wamefufuliwa kwenda kwenye mbingu au wangali wanaendelea kuishi duniani—watapiga kilio kikuu kwa shangwe, kama vile utakavyofanya umati mkubwa wa kondoo wengine unaoshirikiana nao. Baada ya wakati kupita, watu wote waaminifu wa zamani watafufuliwa ndani ya mfumo mpya wa mambo, na wao vilevile watajiunga katika kushangilia. Watu wa Mungu hawakujaribu kujilipiza kisasi wenyewe juu ya wanyanyasaji wao wa dini bandia. Wao wamekumbuka maneno ya Yehova: “Kisasi ni changu mimi; mimi nitalipa, asema Yehova.” (Warumi 12:19; Kumbukumbu 32:35, 41-43, NW) Basi, Yehova amelipa sasa. Damu yote iliyomwagwa na Babuloni Mkubwa itakuwa imekwisha lipizwa kisasi.

      Kuvurumisha Jiwe Kubwa la Kusagia

      9, 10. (a) Sasa malaika kabambe anafanya na kusema nini? (b) Ni tendo gani kama hilo linalofanywa na huyo malaika wa Ufunuo 18:21 lilitukia katika siku ya Yeremia, na hilo lilitoa dhamana gani? (c) Tendo linalochukuliwa na malaika kabambe aliyeonwa na Yohana linatoa dhamana gani?

      9 Jambo ambalo Yohana anafuata kuona linathibitisha kwamba hukumu ya Yehova juu ya Babuloni Mkubwa ni ya kukata maneno: “Na malaika kabambe akainua juu jiwe kama jiwe kubwa la kusagia na kulivurumisha ndani ya bahari, kusema: ‘Hivyo kwa mtupo wa kasi sana Babuloni jiji kubwa atavurumishwa chini, na yeye hatapatikana kamwe tena.’” (Ufunuo 18:21, NW) Katika wakati wa Yeremia, tendo kama hilo likiwa na maana kubwa ya kiunabii lilifanywa. Yeremia alivuviwa aandike katika kitabu “mabaa yote ambayo yangekuja juu ya Babuloni.” Yeye alimpa Seraya kitabu na kumwambia asafiri hadi Babuloni. Huko, akifuata maagizo ya Yeremia, Seraya alisoma julisho-wazi dhidi ya jiji hilo: “O Yehova, wewe mwenyewe umesema dhidi ya mahali hapa, ili kupakatilia mbali pasipate kuwa na mkazi ndani yapo, ama binadamu ama hata mnyama wa nyumbani, bali kwamba pawe mahali patupu tu penye ukiwa hadi wakati usio dhahiri.” Kisha Seraya akafungilia jiwe kwenye kitabu na kukitupa ndani ya mto Eufrati, akisema: “Hivi ndivyo Babuloni litazama chini na halitainuka kamwe kwa sababu ya baa ambalo mimi ninaleta juu yake.”—Yeremia 51:59-64, NW.

      10 Kutupwa kwa kitabu ndani ya mto kikiwa kimefungiliwa jiwe kulikuwa dhamana kwamba Babuloni lingetumbukia ndani ya hali ya kutokomea kabisa, lisipate kupona kamwe. Kuona kwa mtume Yohana malaika kabambe akifanya tendo linalofanana na hilo hali kadhalika ni dhamana yenye nguvu kwamba kusudi la Yehova kuelekea Babuloni Mkubwa litatimizwa. Hali ya kuangamia kabisa ya Babuloni wa kale leo hushuhudia kwa nguvu sana kitakachoangukia dini bandia katika wakati ujao ulio karibu.

      11, 12. (a) Sasa malaika kabambe anahutubiaje Babuloni Mkubwa? (b) Yeremia alitoaje unabii kuhusu Yerusalemu lililoasi imani, na huo uliashiria nini kwa ajili ya siku yetu?

      11 Sasa malaika kabambe anahutubia Babuloni Mkubwa, kusema hivi: “Na sauti ya waimbaji ambao hujifuatanisha kwa kinubi na ya wanamuziki na ya wanafilimbi na ya wanatarumbeta haitasikiwa tena kamwe ndani ya wewe, na hakuna fundi wa kazi ya uchumi yoyote ambaye atapatikana tena wakati wowote ndani ya wewe, na hakuna sauti ya jiwe la kusagia itakayosikika tena wakati wowote ndani yako, na hakuna nuru ya taa ambayo itaangaza tena wakati wowote ndani ya wewe, na hakuna sauti ya bwana-arusi na ya bibi-arusi ambayo itasikiwa tena wakati wowote ndani ya wewe; kwa sababu wauza-bidhaa wasafiri wako walikuwa ndio watu wenye vyeo vya juu wa dunia, kwa maana kwa zoea lako la uwasiliano na roho mataifa yote yaliongozwa vibaya.”—Ufunuo 18:22, 23, NW.

      12 Kwa semi zinazolinganika, Yeremia alitoa unabii kuhusu Yerusalemu asi-imani: “Mimi nitaharibu kutoka wao mvumo wa mchachawo na mvumo wa kushangilia, na sauti ya bwana-arusi na sauti ya bibi-arusi, na mvumo wa kinu cha mkono na nuru ya taa. Na bara hili lote lazima liwe mahali palipoteketezwa na kitu cha kutia kimako.” (Yeremia 25:10, 11, NW) Ikiwa ndiyo sehemu kuu ya Babuloni Mkubwa, Jumuiya ya Wakristo itakuwa magofu yasiyo na uhai, kama vile imeonyeshwa wazi sana na ukiwa wa Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. Jumuiya ya Wakristo ambayo wakati mmoja ilishangilia kwa moyo mkunjufu na ikashughulika kwa kelele ya kila siku itajikuta yenyewe ikiwa imeshindwa na kutupiliwa mbali.

      13. Ni badiliko gani la ghafula linalomfikilia Babuloni Mkubwa, na tokeo ni nini kwa “wauza-bidhaa wasafiri” wake?

      13 Kweli kweli, kama vile malaika huyo anavyomwambia Yohana, Babuloni Mkubwa wote atageuka kutoka milki ya ulimwengu yenye nguvu, na kuwa bara-ukiwa kavu mithili ya mahame. “Wauza-bidhaa” wake, kutia na mamilionea wa vyeo vya juu, wametumia dini yake kwa kujinufaisha kibinafsi au kama kisetiri cha mabaya, na hao viongozi wa kidini wameliona kuwa jambo lenye kufaidi kushiriki pamoja nao katika umashuhuri huo. Lakini wauza-bidhaa hao hawatakuwa tena na Babuloni Mkubwa akiwa mshirika wao katika kufanya mabaya. Yeye hatayapofusha macho tena mataifa ya dunia kwa mazoea ya mafumbo yake ya kidini.

      Hatia ya Damu Yenye Kutisha

      14. Ni nini anayotoa malaika kabambe kuwa ndiyo sababu ya ukali wa hukumu ya Yehova, na Yesu alisema nini hali moja na hivyo wakati alipokuwa duniani?

      14 Kwa kumalizia, malaika kabambe amwambia Yohana sababu ya Yehova kumhukumu Babuloni Mkubwa kwa ukali hivyo. “Ndiyo,” asema malaika, “katika yeye ilipatikana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” (Ufunuo 18:24, NW) Alipokuwa duniani, Yesu aliambia viongozi wa kidini kwamba wao walistahili kutozwa hesabu kwa ajili ya “damu yote yenye uadilifu iliyomwagwa juu ya dunia, kutoka damu ya Abeli mwadilifu” na kuendelea. Kulingana na hilo, kizazi hicho kombokombo kiliharibiwa katika 70 W.K. (Mathayo 23:35-38, NW) Leo, kizazi kingine cha wanadini kinabeba hatia ya damu kwa ajili ya kunyanyasa watumishi wa Mungu.

      15. Kanisa Katoliki katika Ujeremani ya Nazi lilikuwaje na hatia ya damu katika visa viwili?

      15 Katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany, Guenter Lewy anaandika: “Wakati Mashahidi wa Yehova walipokandamizwa katika Bavaria Aprili 13 [1933] Kanisa hata lilikubali mgawo liliopewa na Wizara ya Elimu na Dini wa kuripoti juu ya washiriki wa farakano hilo walioendelea kuzoea dini hiyo iliyokatazwa.” Hivyo Kanisa Katoliki linashiriki daraka la kupelekwa kwa maelfu ya Mashahidi kwenye kambi za mateso; mikono yalo imetiwa madoa ya damu ya uhai wa mamia ya Mashahidi ambao walinyongwa. Wakati Mashahidi vijana, kama Wilhelm Kusserow, walipoonyesha kwamba wangekufa kijasiri kwa kupigwa risasi na kikosi cha wapiga risasi, Hitla aliamua kwamba kikosi cha wapiga risasi hakikuwafaa wakataaji kidhamira; kwa hiyo Wolfgang ndugu ya Wilhelm, akiwa na umri wa miaka 20, alikufa kwa njia ya gilotini. Wakati ule ule, Kanisa Katoliki lilikuwa likiwatia moyo vijana Wakatoliki Wajeremani wafe katika jeshi la bara-baba lao. Hatia ya damu ya hilo kanisa yaonekana wazi!

      16, 17. (a) Ni hatia gani ya damu ambayo ni lazima Babuloni Mkubwa ashtakiwe, na Vatikani ilikuwaje na hatia ya damu kuhusu Wayahudi waliouawa katika michinjo-chinjo ya Kinazi? (b) Ni katika njia gani moja ambayo kwayo dini bandia ina lawama kwa ajili ya kuuawa kwa mamilioni ya watu katika mamia ya vita katika nyakati zetu?

      16 Hata hivyo, unabii unasema kwamba lazima Babuloni Mkubwa ashtakiwe kwa damu ya “wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” Hakika hilo limekuwa kweli katika nyakati za ki-siku-hizi. Mathalani, kwa kuwa hila ya Katoliki ndiyo iliyomsaidia Hitla apate mamlaka katika Ujeremani, Vatikani inashiriki hatia ya damu iliyo mbaya sana juu ya Wayahudi milioni sita waliokufa katika michinjo-chinjo ya Kinazi. Na zaidi, katika nyakati zetu, watu zaidi ya milioni mia moja wameuawa katika mamia ya vita. Je! dini bandia ina lawama kwa habari hii? Ndiyo, kwa njia mbili.

      17 Njia moja ni kwamba vita vingi vinahusiana na tofauti za kidini. Mathalani, jeuri katika India kati ya Waislamu na Wahindu katika 1946-48 ilichochewa na dini. Mamia ya maelfu ya maisha yalipotea. Pambano kati ya Iraki na Irani katika miaka ya 1980 lilihusiana na tofauti za kimafarakano, kukiwa na mamia ya maelfu waliouawa. Jeuri kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika Ailandi ya Kaskazini imetwaa maelfu ya maisha. Akichunguza uwanja huu, mleta habari za magazetini C. L. Sulzberger alisema hivi katika 1976: “Ni ukweli wenye kuhuzunisha kwamba pengine nusu au zaidi ya vita vinavyopiganwa sasa kotekote katika ulimwengu ama kwa wazi ni mapambano ya kidini ama yanahusu mabishano ya kidini.” Kweli kweli, imekuwa hivyo muda wote wa historia yenye msukosuko ya Babuloni Mkubwa.

      18. Ni ipi njia ya pili ambayo kwayo dini za ulimwengu zina hatia ya damu?

      18 Ni ipi ile njia nyingine? Kwa maoni ya Yehova, dini za ulimwengu zina hatia ya damu kwa sababu hizo hazikufundisha kwa kusadikisha wafuasi wazo ukweli wa matakwa ya Yehova kwa ajili ya watumishi wake. Hizo hazikufundisha watu kwa kusadikisha kwamba waabudu wa kweli lazima wamwige Yesu Kristo na kuonyesha wengine upendo bila kujali asili yao ya kitaifa. (Mika 4:3, 5; Yohana 13:34, 35; Matendo 10:34, 35; 1 Yohana 3:10-12) Kwa sababu dini ambazo zinajumlika kuwa Babuloni Mkubwa hazikufundisha vitu hivi, wafuasi wazo wamevutwa kuingizwa ndani ya kizingo cha vita vya kimataifa. Lo! jinsi hilo lilivyokuwa wazi katika vile vita viwili vya ulimwengu vya nusu ya kwanza ya karne ya 20, ambavyo vyote viwili vilianza katika Jumuiya ya Wakristo na vikatokeza kuchinjana kwa wanadini! Ikiwa wote wanaodai kuwa Wakristo wangalishikamana na kanuni za Biblia, vita hivyo havingaliweza kutukia kamwe.

      19. Ni hatia ya damu gani yenye kutisha sana anayobeba Babuloni Mkubwa?

      19 Yehova anaweka lawama la umwagaji-damu huu wote kwenye nyayo za Babuloni Mkubwa. Ikiwa viongozi wa kidini, hasa wale walio katika Jumuiya ya Wakristo, wangalifundisha watu wao ukweli wa Biblia, umwagaji-damu mkubwa sana hivyo haungalitukia. Kwa kweli, basi, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, Babuloni Mkubwa—yule kahaba mkubwa na milki ya ulimwengu ya dini bandia—lazima amjibu Yehova si kwa ajili ya “damu ya manabii na ya watakatifu” tu ambao yeye amenyanyasa na akaua bali pia kwa ajili “ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” Kweli kweli Babuloni Mkubwa anabeba hatia ya damu yenye kutisha sana. Na apotelee mbali wakati uharibifu wake unapotukia!

      [Sanduku katika ukurasa wa 270]

      Gharama ya Kuridhiana

      Guenter Lewy anaandika katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany: “Kama Ukatoliki wa Ujeremani tangu mwanzo ungalishikamana na mwongozo wa kupinga kwa dhati utawala wa Nazi, historia ya ulimwengu ingaliweza kuchukua mwendo tofauti. Hata kama mng’ang’ano huu ungalikosa mwishowe kabisa kumshinda Hitla na kuzuia uhalifu wake mwingi, kwa oni hili ungaliinua sana hadhi ya kiadili ya Kanisa hilo. Gharama ya kibinadamu kwa ukinzani huu ingalikuwa kubwa bila kukanika, lakini dhabihu hizo zingalikuwa zimetolewa kwa ajili ya kusudi kubwa zaidi ya yote. Hitla akiwa haungwi mkono nyumbani, yamkini hangalithubutu kwenda vitani na kihalisi mamilioni ya maisha yangaliokolewa. . . . Wakati Wajeremani wapinga Unazi walipoteswa mpaka kifo katika kambi za mateso za Hitla, wakati weledi wa Polandi walipochinjwa, wakati mamia ya maelfu ya Warusi walipokufa kama tokeo la kutendwa kama Untermenschen [nusu-binadamu] wa Kislavi, na wakati binadamu 6,000,000 walipouawa kimakusudi kwa kuwa ‘si Waarya,’ maofisa wa Kanisa Katoliki katika Ujeremani walitegemeza utawala uliokuwa ukifanya uhalifu huu. Papa katika Roma, kichwa cha kiroho na mwalimu wa kiadili mkuu zaidi ya wote wa Kanisa Katoliki la Roma, alikaa kimya.”—Kurasa 320, 341.

      [Picha katika ukurasa wa 268]

      “Ni vibaya mno, ni vibaya mno,” wasema watawala

      [Picha katika ukurasa wa 268]

      “Ni vibaya mno, ni vibaya mno,” wasema wauza-bidhaa

  • Sifuni Yah kwa Hukumu Zake!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Sura ya 38

      Sifuni Yah kwa Hukumu Zake!

      1. Yohana anasikia maneno gani “kama sauti kubwa ya umati mkubwa katika mbingu”?

      BABULONI MKUBWA hayupo tena! Kwa kweli hizi ni habari zenye shangwe. Si ajabu kwamba Yohana anasikia mipaazo yenye furaha katika mbingu! “Baada ya vitu hivi mimi nikasikia kilichokuwa kama sauti kubwa ya umati mkubwa katika mbingu. Wao walisema: ‘Halleluyah!a Wokovu na utukufu na nguvu ni za Mungu wetu, kwa sababu hukumu zake ni za kweli na za uadilifu. Kwa maana yeye ametekeleza hukumu juu ya kahaba mkubwa ambaye alifisidi dunia kwa uasherati wake, na yeye amelipiza kisasi cha damu ya watumwa wake katika mkono wake.’ Na mara hiyo kwa mara ya pili wao wakasema: ‘Halleluyah!b Na ule moshi kutoka kwake huendelea kupaa milele na milele.’”—Ufunuo 19:1-3, NW.

      2. (a) Neno “Halleluyah” humaanisha nini, na Yohana kulisikia mara mbili kufikia hapa huonyesha nini? (b) Ni nani anayepokea utukufu kwa kuharibu Babuloni Mkubwa? Fafanua.

      2 Halleluyah kweli kweli! Neno hilo humaanisha “Sifuni Yah, nyinyi watu,” “Yah” ikiwa ni namna ya kifupi cha jina la kimungu, Yehova. Tunakumbushwa hapa waadhi ya mtunga zaburi: “Kila kitu chenye kupumua—acheni kisifu Yah. Sifuni Yah, nyinyi watu!” (Zaburi 150:6, NW) Kusikia kwa Yohana korasi ya kimbingu yenye kuchachawa ikiimba “Halleluyah!” mara mbili kufikia hapa katika Ufunuo huonyesha mwendeleo wa ufunuo wa kimungu wa ukweli. Mungu wa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo ndiye Mungu yule yule wa Maandiko ya Kiebrania ya mapema zaidi, na Yehova ndilo jina lake. Mungu aliyesababisha anguko la Babuloni wa kale amehukumu na akaharibu sasa Babuloni Mkubwa. Mpeni utukufu kwa tendo hilo la uhodari! Nguvu iliyoongoza kwa werevu kuanguka kwake ilikuwa yake badala ya kuwa ya mataifa ambayo yeye alitumia kuwa vyombo vya kumwacha ukiwa. Yatupasa sisi kumsifu Yehova pekee kwa ajili ya wokovu.—Isaya 12:2; Ufunuo 4:11; 7:10, 12.

      3. Ni kwa sababu gani kahaba mkubwa amestahili sana hukumu yake?

      3 Ni kwa sababu gani kahaba mkubwa amekuwa mwenye kustahili sana hukumu hii? Kulingana na Sheria ambayo Yehova alitoa kwa Noa—na kupitia yeye kwa aina ya binadamu yote—kumwaga damu kimakusudi kunataka hukumu ya kifo. Taarifa hiyo ilitolewa tena katika Sheria ya Mungu kwa Israeli. (Mwanzo 9:6; Hesabu 35:20, 21) Zaidi ya hilo, chini ya Sheria ya Musa uzinzi wa kiroho na wa kimwili ulistahilisha kifo. (Walawi 20:10; Kumbukumbu 13:1-5) Kwa maelfu ya miaka, Babuloni Mkubwa amekuwa na hatia ya damu, na yeye ni mwasherati mbaya sana. Mathalani, sera ya Kanisa Katoliki la Roma ya kukataza mapadri walo kuoa imetokeza utovu wa adili mbaya sana upande wa wengi wao, na ni wengi wa hawa leo ambao wameambukizwa UKIMWI. (1 Wakorintho 6:9, 10; 1 Timotheo 4:1-3) Lakini madhambi yake makubwa, ‘yakitungamana pamoja moja kwa moja hadi mbinguni,’ ni matendo yalo yenye kugutusha ya uasherati wa kiroho—tendo hili la pili ni katika kufundisha mafundisho bandia na kujipanga upande mmoja na wanasiasa wafisadi. (Ufunuo 18:5) Kwa kuwa adhabu yake mwishowe imemfikilia, halaiki kubwa ya kimbingu sasa yarudisha mwangwi wa pili wa Halleluyah!

      4. Ni nini kinachofananishwa na uhakika wa kwamba moshi kutoka Babuloni Mkubwa “huendelea kupaa milele na milele”?

      4 Babuloni Mkubwa amewashwa moto kama jiji lililoshindwa, na moshi wa kutoka kwake “huendelea kupaa milele na milele.” Wakati jiji halisi linapochomwa na majeshi yenye ushindi, moshi huendelea kupaa kwa muda ambao majivu ni yenye moto. Yeyote anayejaribu kulijenga tena linapoendelea kutoa moshi atachomwa tu na yale magofu yenye kutoa moshi. Kwa kuwa moshi kutoka kwake utainuka “milele na milele” katika kuonyesha hukumu yake yenye kukata maneno, hakuna yeyote atakayeweza wakati wowote kurudisha jiji hilo lenye dhambi. Dini bandia imetoweka milele na milele. Halleluyah, kweli kweli!—Linga Isaya 34:5, 9, 10.

      5. (a) Wazee 24 na viumbe hai wanne wanafanya na kusema nini? (b) Ni kwa sababu gani kibwagizo cha Halleluyah ni cha kimelodia kuliko korasi za Halleluyah zinazoimbwa katika makanisa ya Jumuiya ya Wakristo?

      5 Katika njozi ya mapema zaidi, Yohana aliona kuzunguka kiti cha ufalme viumbe hai wanne, pamoja na wazee 24 ambao ni picha ya warithi wa Ufalme wakiwa katika cheo chao kitukufu cha kimbingu. (Ufunuo 4:8-11) Sasa yeye anawaona tena na wao wanangurumisha Halleluyah ya tatu juu ya uharibifu wa Babuloni Mkubwa: “Na wale wazee ishirini na wanne na viumbe hai wanne wakaanguka chini na kuabudu Mungu aketiye juu ya kiti cha ufalme, na kusema: ‘Ameni! Halleluyah.’”c (Ufunuo 19:4, NW) Basi, korasi tukufu hii ya Halleluyah ni katika kuongezea ule “wimbo mpya” wa sifa kwa Mwana-Kondoo. (Ufunuo 5:8, 9, NW) Wao wanaimba sasa kibwagizo cha ushindi wenye utukufu, wakimpa Yehova Bwana Mwenye Enzi Kuu utukufu wote kwa sababu ya ushindi wake wenye kukata maneno juu ya kahaba mkubwa, Babuloni Mkubwa. Halleluyah hizi zimelia kimelodia kwa mbali zaidi sana kuliko korasi za Halleluyah zozote zilizopata kuimbwa katika makanisa ya Jumuiya ya Wakristo ambamo Yehova, au Yah, amevunjiwa heshima na akadharauliwa. Wimbaji wa kinafiki kama huo unaoshutumu jina la Yehova umekomeshwa sasa milele!

      6. Ni “sauti” ya nani inayosikiwa, nayo inahimiza nini, na ni nani wanaoshiriki katika kuitikia?

      6 Ilikuwa katika 1918 ndipo Yehova alianza kuthawabisha ‘wale wanaohofu jina lake, wadogo na wakubwa’—wa kwanza wa hawa wakiwa wa wale Wakristo wapakwa-mafuta ambao walikuwa wamekufa wakiwa waaminifu, na ambao yeye alifufua na akawaweka katika vyeo vya kimbingu vya wazee 24. (Ufunuo 11:18, NW) Wengine hujiunga na hawa katika kuimba Halleluyah, kwa kuwa Yohana huripoti hivi: “Pia, sauti moja ikatokea katika kiti cha ufalme na kusema: ‘Mwe mkisifu Mungu wetu, nyinyi nyote watumwa wake, ambao huhofu yeye, wadogo na wakubwa.’” (Ufunuo 19:5, NW) Hii ni “sauti” ya Mneni wa Yehova, Mwana wake mwenyewe, Yesu Kristo, ambaye husimama “katikati ya kiti cha ufalme.” (Ufunuo 5:6, NW) Si mbinguni tu bali pia hapa duniani, “nyinyi nyote watumwa wake” shirikini katika kuimba, jamii ya Yohana iliyopakwa mafuta ikiwa inachukua uongozi duniani. Ni kwa kuchachawa kulikoje hawa hushiriki katika kutii amri: “Mwe mkisifu Mungu wetu”!

      7. Baada ya Babuloni Mkubwa kuharibiwa, ni nani watakaokuwa wakisifu Yehova?

      7 Ndiyo, wale wa umati mkubwa pia huhesabiwa wanapewa namba pia miongoni mwa watumwa hawa. Tangu 1935 hawa wamekuwa wakitoka katika Babuloni Mkubwa na wameona utimizo wa ahadi ya Mungu: “Yeye atabariki wale ambao huhofu Yehova, wadogo na wakubwa.” (Zaburi 115:13, NW) Wakati Babuloni Mkubwa aharibiwapo, mamilioni yao watajiunga katika ‘kusifu Mungu wetu’—pamoja na jamii ya Yohana na wingi wote wa kimbingu. Baadaye, wale wenye kufufuliwa duniani, wawe hapo kwanza walikuwa mashuhuri au la, bila shaka wataimba Halleluyah zaidi wanapojifunza kwamba Babuloni Mkubwa ametoweka milele. (Ufunuo 20:12, 15) Sifa yote imwendee Yehova kwa ushindi wake wenye kishindo juu ya kahaba huyo wa tangu zamani!

      8. Korasi za sifa zilizoshuhudiwa na Yohana zapaswa kutupa sisi kichochezi gani sasa, kabla ya Babuloni Mkubwa kuharibiwa?

      8 Hayo yote yanatupa sisi kichochezi kama nini tushiriki katika kazi ya Mungu leo! Watumishi wote wa Yah na wajitoe wenyewe kwa moyo na nafsi kutangaza hukumu za Mungu, pamoja na tumaini tukufu la Ufalme, sasa, kabla ya Babuloni Mkubwa kuondolewa katika kiti na kuharibiwa.—Isaya 61:1-3; 1 Wakorintho 15:58.

      ‘Halleluyah—Yehova Ni Mfalme!’

      9. Ni kwa sababu gani Halleluyah ya mwisho ni yenye mvumo kamili, ni ya sauti timilifu, na ya hali ya juu sana?

      9 Kuna sababu zaidi kwa kushangilia, kama vile Yohana aendeleavyo kutuambia: “Na mimi nikasikia kilichokuwa kama sauti ya umati mkubwa na kama mvumo wa maji mengi na kama mvumo wa ngurumo kubwa. Zikasema: ‘Halleluyah,d kwa sababu Yehova Mungu wetu, Mweza Yote, ameanza kutawala akiwa mfalme.’” (Ufunuo 19:6, NW) Halleluyah hii ya mwisho ndiyo inayofanya mbiu iwe yenye miraba minne, au yenye ulingano. Ni mvumo wa kimbingu wenye nguvu, wa hali ya juu kuliko korasi yoyote ya kibinadamu, yenye fahari ya kifalme zaidi ya poromoko la maji lolote la kidunia, na yenye kuvuvia hofu zaidi kuliko ngurumo yoyote ya kidunia. Mamiriadi ya sauti za kimbingu yanasherehekea uhakika wa kwamba “Yehova Mungu wetu, Mweza Yote, ameanza kutawala akiwa mfalme.”

      10. Ni katika maana gani inaweza kusemwa kwamba Yehova huanza kutawala akiwa mfalme baada ya mteketeo wa Babuloni Mkubwa?

      10 Ingawa hivyo, inakuwaje kwamba Yehova huanza kutawala? Mamileani yamepita tangu mtunga zaburi alipotangaza: “Mungu ni Mfalme wangu tangu zamani za kale.” (Zaburi 74:12, NW) Umaliki wa Yehova ulikuwa wa kale hata wakati huo, kwa hiyo korasi hiyo ya ulimwengu wote mzima ingewezaje kuimba kwamba “Yehova . . . ameanza kutawala akiwa mfalme”? Katika maana ya kwamba wakati Babuloni Mkubwa anapoharibiwa, Yehova hatakuwa tena na mshindani huyo mwenye kimbelembele akikengeusha utii kwake akiwa ndiye Mwenye Enzi Kuu ya Ulimwengu Wote Mzima. Dini bandia haitachochea tena watawala wa dunia wampinge. Wakati Babuloni wa kale alipoanguka kutoka utawala wa ulimwengu, Sayuni ilisikia mbiu ya ushindi: “Mungu wako amekuwa mfalme!” (Isaya 52:7, NW) Baada ya Ufalme kuzaliwa katika 1914, wazee 24 walipiga mbiu hii: “Sisi twashukuru wewe, Yehova Mungu . . . kwa sababu wewe umechukua nguvu kuu zako na umeanza kutawala ukiwa mfalme.” (Ufunuo 11:17, NW) Sasa, baada ya mteketeo wa Babuloni Mkubwa, kilio kinatamkwa tena: “Yehova . . . ameanza kutawala akiwa mfalme.” Hakuna kamungu kalikofanyizwa na mwanadamu kanakobaki kagombee enzi kuu ya Yehova, Mungu wa kweli!

      Ndoa ya Mwana-Kondoo Imekaribia!

      11, 12. (a) Yerusalemu wa kale liliitaje Babuloni wa kale, kuweka kiolezo gani kwa habari ya Yerusalemu Jipya na Babuloni Mkubwa? (b) Masongamano ya kimbingu huimba na kutangaza nini kwa ushindi juu ya Babuloni Mkubwa?

      11 “Wewe mwanamke adui yangu”! Hivyo ndivyo Yerusalemu, mahali pa hekalu la ibada ya Yehova, liliita Babuloni mwabudu sanamu. (Mika 7:8, NW) Hali moja na hiyo, “jiji takatifu, Yerusalemu Jipya,” ambalo ni bibi-arusi mwenye washiriki 144,000, limekuwa na kila sababu ya kuita Babuloni Mkubwa kuwa adui yake. (Ufunuo 21:2) Lakini hatimaye huyo kahaba mkubwa amepatwa na msiba, janga, na angamio. Mazoea yake ya kuwasiliana na roho na wanajimu wake hayakumwokoa. (Linga Isaya 47:1, 11-13.) Ni ushindi mkubwa, kweli kweli, kwa ajili ya ibada ya kweli!

      12 Kahaba mwenye kunyarafisha Babuloni Mkubwa, akiwa ametoweka milele, sasa uangalifu waweza kuelekezwa juu ya bibi-arusi bikira safi wa Mwana-Kondoo! Kwa sababu hiyo, masongamano ya kimbingu yaimba kwa mchachawo katika kusifu Yehova: “Acheni sisi tushangilie na tufurikwe na shangwe, na acheni sisi tumpe yeye utukufu, kwa sababu ndoa ya Mwana-Kondoo imewasili na mke wake amejitayarisha mwenyewe. Ndiyo, amepewa ruhusa kujipamba kwa kitani nyangavu, safi, nzuri sana, kwa maana kitani nzuri sana husimama kwa ajili ya matendo ya uadilifu ya watakatifu.”—Ufunuo 19:7, 8, NW.

      13. Ni tayarisho gani kwa ajili ya ndoa ya Mwana-Kondoo limetukia kwa karne zote?

      13 Kwa muda wa karne zote, Yesu amefanya tayarisho lenye upendo kwa ajili ya ndoa hii ya kimbingu. (Mathayo 28:20; 2 Wakorintho 11:2) Yeye amekuwa akisafisha 144,000 wa Israeli wa kiroho ili “yeye aweze kujiletea yeye mwenyewe kundi katika umaridadi walo, bila kuwa na doa au kunyanzi au lolote la vitu kama hivyo, bali kwamba limepaswa kuwa takatifu na bila waa.” (Waefeso 5:25-27, NW) Wakitaka kufikia “zawadi ya mwito wa juu wa Mungu,” kila Mkristo mpakwa-mafuta amelazimika kuvua utu wa zamani pamoja na mazoea yao, na kuvaa utu mpya wa Kikristo, na kufanya matendo ya uadilifu “kwa nafsi yote kama kwa Yehova.”—Wafilipi 3:8, 13, 14; Wakolosai 3:9, 10, 23, NW.

      14. Shetani amejaribuje kuchafua wanaotazamiwa kuwa washiriki wa mke wa Mwana-Kondoo?

      14 Kutoka Pentekoste 33 W.K. na kuendelea, Shetani alitumia Babuloni Mkubwa akiwa chombo chake katika kujaribu kuchafua wanaotazamiwa kuwa washiriki wa mke wa Mwana-Kondoo. Kufikia mwisho wa karne ya kwanza, yeye alikuwa amepanda mbegu za dini ya Kibabuloni katika kundi. (1 Wakorintho 15:12; 2 Timotheo 2:18; Ufunuo 2:6, 14, 20) Mtume Paulo anaeleza wale ambao walikuwa wakipindua imani kwa maneno haya: “Kwa maana watu kama hao ni mitume bandia, wafanya kazi wadanganyifu, wakijigeuza umbile wenyewe kuwa mitume wa Kristo. Na si ajabu, kwa maana Shetani mwenyewe huendelea kujigeuza umbile mwenyewe kuwa malaika wa nuru.” (2 Wakorintho 11:13, 14, NW) Katika karne zilizoandama, Jumuiya ya Wakristo asi-imani, kama sehemu inayobaki ya Babuloni Mkubwa, ilijivisha yenyewe mavazi ya utajiri na pendeleo, “zambarau na rangi-nyekundu-nyangavu, . . . dhahabu na jiwe la thamani na lulu.” (Ufunuo 17:4, NW) Viongozi wayo wa kidini na mapapa waliandamana na maliki wenye kiu cha kumwaga damu kama vile Konstantino na Charlemagne. Yeye hakupambwa kamwe kwa “matendo ya uadilifu ya watakatifu.” Akiwa bibi-arusi bandia, kwa kweli yeye alikuwa kipeo cha udanganyi wa kishetani. Hatimaye, yeye ametoweka milele!

      Mke wa Mwana-Kondoo Amejitayarisha

      15. Kutiwa muhuri hutukiaje, na ni jambo gani linalotakwa kwa Wakristo wapakwa-mafuta?

      15 Basi sasa, baada ya karibu miaka 2,000, wote 144,000 wa jamii ya bibi-arusi wamejiweka wenyewe tayari. Lakini ni kwenye pindi gani ya wakati inaweza kusemwa kwamba ‘mke wa Mwana-Kondoo amejitayarisha’? Kwa kuendelea, kutoka Pentekoste 33 W.K. wapakwa-mafuta wenye kuitikadi “walitiwa muhuri kwa roho takatifu iliyoahidiwa,” hii ni kwa kutazamia “siku ya kuachiliwa kupitia ukombozi” iliyokuwa ikija. Kama mtume Paulo alivyolisema jambo hilo, Mungu “pia ameweka muhuri wake juu yetu na ametupa sisi ishara ya kitakachokuja, yaani, roho, katika mioyo yetu.” (Waefeso 1:13; 4:30; 2 Wakorintho 1:22, NW) Kila Mkristo aliyepakwa mafuta ‘ameitwa na akachaguliwa,’ na amejithibitisha mwenyewe kuwa ‘mwaminifu.’—Ufunuo 17:14, NW.

      16. (a) Kutiwa muhuri kwa mtume Paulo kulitimilizwa wakati gani, na sisi tunajuaje? (b) Ni wakati gani mke wa Mwana-Kondoo atakuwa ‘amejitayarisha’ kikamili?

      16 Baada ya miongo ya mtihani, Paulo mwenyewe angeweza kujulisha wazi: “Mimi nimepiga vita njema, mimi nimekimbia mwendo hadi mwisho,

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki