Wimbo 77
“Yehova Ni Mchungaji Wangu”
1. Yehova Muchunga wangu;
Kwa nini niogope?
Atunzaye sana kondoo
Hamusahau wake.
Huniongoza kwa maji,
Huhuisha nafusi.
Huongoza hatua zangu
Njiani adilifu.
Huongoza hatua zangu
Njiani adilifu.
2. Nijapopita bonde la
Uvuli, siogopi,
Muchunga yu nami daima
Fimbo y’ondoa hofu.
Hupaka kichwa mafuta;
Kikombe akijaza.
Fadhili zitanifuata,
Nikae nyumba yake.
Fadhili zitanifuata,
Nikae nyumba yake.
3. Mchungaji wa hekima!
Sifa zake naimba.
Habari za utunzi wake
Niletee kondoo.
Nitatii sana Neno,
Kwenda njiani mwake.
Hazina ya huduma yangu
Nitumie daima.
Hazina ya huduma yangu
Nitumie daima.