Wimbo 142
Tumaini la Kukomboa Uumbaji
1. Viumbe vyote vinayo dhiki;
Wavuna walichopanda.
Wamemukana Mungu wakawa
Chini ya madhara mengi.
2. Kutazamia wokovu watu,
Watumainie Mungu.
Anasaidia, ni rafiki
Ya wote wanaolia.
3. Jamaa ya kibinadamu
Itarudishwa iwe huru.
Na Yesu amewekwa, kibali
Watu wapate kwa Mungu.
4. Kuwa na “taifa” la Yehova
Ni baraka kwa wapole.
Wanangoja kwa shauku nyingi,
Shangwe za ule Ufalme.