Wimbo Na. 111
Ataita
Makala Iliyochapishwa
1. Lo! Uhai ni kama ukungu,
Nao kesho haupo.
Watokea kisha watoweka.
Huzuni kwa wapendwa.
Mutu akifa, je, ataishi?
Mungu ameahidi:
(KORASI)
Aki’ta; Wataitika,
Watoke na kuishi.
Mungu anatamani,
Kazi ya mikonoye.
Usiwe na shaka kamwe,
Yehova ’tatwinua,
Kisha twishi milele,
Sisi ni mali yake.
2. Rafikize Yehova wakifa,
Hawasahau kamwe.
Walalao katika Kaburi,
Watainuka tena.
Tufurahie uzima nao,
Duniani milele.
(KORASI)
Aki’ta; Wataitika,
Watoke na kuishi.
Mungu anatamani,
Kazi ya mikonoye.
Usiwe na shaka kamwe,
Yehova ’tatwinua,
Kisha twishi milele,
Sisi ni mali yake.
(Ona pia Yoh. 6:40; 11:11, 43; Yak. 4:14.)