Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • rs uku. 302-uku. 303
  • Toharani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Toharani
  • Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Biblia Inazungumza Kuhusu Toharani?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Misa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Urithi wa Upapa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Nafsi
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
Pata Habari Zaidi
Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
rs uku. 302-uku. 303

Toharani

Maana: “Kulingana na fundisho la Kanisa [Katoliki], ni mahali, au hali, baada ya mtu kufa . . . ambapo nafsi za wale wanaokufa wakiwa katika hali ya neema, lakini ambao bado hawajakuwa wakamilifu kabisa, zinafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zinazoweza kusamehewa au kwa ajili ya adhabu ya muda kwa sababu ya dhambi zinazoweza kusamehewa na zenye kuleta kifo ambazo tayari zimesamehewa na, kwa kufanya hivyo, zinatakaswa kabla ya kuingia mbinguni.” (New Catholic Encyclopedia, 1967, Buku la 11, uku. 1034) Hilo si fundisho la Biblia.

Msingi wa fundisho la toharani ni nini?

Baada ya kuchunguza mambo ambayo waandikaji Wakatoliki wamesema kuhusu maandiko kama vile 2 Wamakabayo 12:39-45, Mathayo 12:32, na 1 Wakorintho 3:10-15, New Catholic Encyclopedia (1967, Buku la 11, uku. 1034) inakiri hivi: “Kwa ujumla, msingi wa fundisho la Kikatoliki kuhusu toharani ni mapokeo, si Maandiko Matakatifu.”

“Kanisa limetegemea mapokeo ili kuunga mkono mahali palipo katikati ya mbingu na motoni.”—U.S. Catholic, Machi 1981, uku. 7.

Kuhusu hali ya toharani, wasemaji wa Kikatoliki wana maoni gani?

“Wengi wanafikiri kwamba kuteseka toharani huhusiana na ufahamu wa kuahirishwa kwa muda kwa maono ya raha, ijapokuwa wengi wanafikiri kwamba, zaidi ya hayo, kuna adhabu fulani ya hakika . . . Katika Kanisa Katoliki kwa ujumla watu wengi wanashikilia kwamba maumivu hayo yanasababishwa na moto halisi. Hata hivyo, jambo hilo si lazima ili kuamini toharani. Hata si hakika. . . . Hata mtu akiamua, kama vile wanatheolojia wa Mashariki, kulikataa wazo la kuteseka kunakosababishwa na moto, inampasa mtu huyo awe mwangalifu asije akapuuza kabisa wazo la hali ya kuteseka halisi toharani. Bado kuna mateso halisi, huzuni, kuudhika, aibu ya dhamiri, na huzuni nyingine za kiroho zinazoweza kuiumiza nafsi kikweli. . . . Inapasa kukumbukwa kabisa kwamba, nafsi hizo zinapokuwa katika mateso, pia zinaona shangwe kubwa kwa kuwa zina hakika zitaokolewa.”—New Catholic Encyclopedia (1967), Buku la 11, uku. 1036, 1037.

“Hakuna mtu anayejua hakika jambo linalotendeka toharani.”—U.S. Catholic, Machi 1981, uku. 9.

Je, nafsi huendelea kuishi baada ya mwili kufa?

Eze. 18:4, ZSB: “Nafsi [Kiebrania, neʹphesh; “yeyote,” BHN; “roho,” UV] inayofanya zambi, itakufa.”

Yak. 5:20, NAJ: “Yeyote amrudishaye mwenye dhambi kutoka katika makosa yake, ataiokoa nafsi yake kutokana na mauti, na kufunika dhambi nyingi.” (Italiki zimeongezwa.) (Ona kwamba mstari huo unasema kuhusu mauti, yaani, kifo, cha nafsi.)

Kwa habari zaidi, ona vichwa “Kifo” na “Nafsi.”

Je, mtu huendelea kuadhibiwa baada ya kufa kwake?

Rom. 6:7, UV: “Yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.” (NAJ: “Mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi.”)

Je, wafu wanaweza kuwa na shangwe kwa sababu wanatarajia kuokolewa?

Mhu. 9:5, UV: “Walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote.”

Isa. 38:18, UV: “Kuzimu [“Kaburi,” NW] hakuwezi kukusifu [Yehova]; mauti haiwezi kukuadhimisha; wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.” (Basi, hao wafu wanawezaje “kuwa na shangwe kwa sababu wanatarajia kuokolewa”?)

Kulingana na Biblia, dhambi husafishwaje?

1 Yoh. 1:7, 9, UV: “Tukienenda nuruni, kama yeye [Mungu] alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. . . . Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote [“uovu wote,” BHN].

Ufu. 1:5, UV: “Yesu Kristo . . . atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki