Wimbo Na. 71
Roho Takatifu—Zawadi Kutoka kwa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Baba, mwenye rehema,
Mioyo yetu waijua.
Tuondolee mahangaiko,
Tupe faraja ya roho yako.
2. Ee! Baba, sisi ni wakosaji;
Mara kwa mara twakosea.
Tunakusihi, tunakuomba
Utuongoze kwa roho yako.
3. Tunapochoka, na kulemewa,
Roho yako yatuinua.
Kama tai twaruka kwa nguvu.
Tupe roho yako takatifu.
(Ona pia Zab. 51:11; Yoh. 14:26; Mdo. 9:31.)