WIMBO NA. 18
Tunathamini Fidia
Makala Iliyochapishwa
1. Twasimama mbele
za kiti cha enzi,
Yah ulituonyesha
Upendo mkubwa.
Ulitoa Mwana wako
wa pekee.
Ni zawadi kubwa sana,
twaithamini.
(KORASI)
Alimwaga damu yake.
Tupate kuwekwa huru.
Twashukuru,
kwa moyo wetu wote milele.
2. Kwa hiari Yesu
Katoa dhabihu.
Na kwa upendo katoa
Uhai wake.
Kafungua njia
Tupate wokovu.
Sasa tumaini la
uzima tunalo.
(KORASI)
Alimwaga damu yake.
Tupate kuwekwa huru.
Twashukuru,
kwa moyo wetu wote milele.
(Ona pia Ebr. 9:13, 14; 1 Pet. 1:18, 19.)