Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb23 Septemba uku. 5
  • Mtegemee Yehova Unaposhughulika na Mtu Anayekuonea

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtegemee Yehova Unaposhughulika na Mtu Anayekuonea
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
  • Habari Zinazolingana
  • Kuacha Udhalimu
    Amkeni!—2003
  • Nifanye Nini Ninapoonewa?
    Vijana Huuliza
  • Nifanye Nini Ninapoonewa Shuleni?
    Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Dhuluma Baadhi ya Visababishi na Matokeo
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
mwb23 Septemba uku. 5
Msichana tineja akiwaonyesha wazazi simu yake na kuwaeleza hisia zake. Wazazi wanamsikiliza kwa makini.

MAISHA YA MKRISTO

Mtegemee Yehova Unaposhughulika na Mtu Anayekuonea

Waoneaji wanaweza kutusababishia maumivu ya kimwili na ya kihisia. Hata wanaweza kutudhuru kiroho ikiwa tutaogopa wanapopinga ibada yetu. Unaweza kujilindaje dhidi ya mtu anayekuonea?

Waabudu wengi wa Yehova wamemtegemea yeye na wamefaulu kushughulika na watu wanaowaonea. (Zb 18:17) Kwa mfano, Esta alimshtaki mwoneaji mwovu aliyeitwa Hamani na hivyo kufunua njama zake. (Est 7:​1-6) Kabla ya kufanya hivyo, alionyesha kwamba anamtegemea Yehova kwa kufunga kula. (Est 4:​14-16) Yehova alibariki matendo ya Esta kwa kulimlinda yeye na Wayahudi.

Kijana, unapokabiliwa na mwoneaji, mwombe Yehova msaada na uzungumzie tatizo lako na mtu mzima mkomavu, kama vile mzazi. Uwe na uhakika kwamba Yehova atakusaidia kama tu alivyomsaidia Esta. Unaweza kufanya nini kingine ili kukabiliana na watu wanaokuonea?

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA MAISHA YANGU YA UTINEJA—NITAFANYA NINI NIKIONEWA? KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Vijana wanaweza kujifunza nini kutokana na mifano ya Charlie na Ferin?

  • Wazazi wanaweza kujifunza nini kutokana na maelezo ya Charlie na Ferin kuhusu kuwasaidia watoto kukabiliana na mtu anayewaonea?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki