HAZINA ZA NENO LA MUNGU
Uadilifu Haupimwi kwa Utajiri
Sofari alisisitiza kwamba Mungu huwanyang’anya waovu utajiri, akidai kwamba lazima Ayubu awe alitenda dhambi (Ayu 20:5, 10, 15)
Ayubu alijibu: ‘Basi kwa nini waovu wanapata mafanikio?’ (Ayu 21:7-9)
Mfano wa Yesu unathibitisha kwamba huenda watu waadilifu wasiwe na mali za kimwili (Lu 9:58)
JAMBO LA KUTAFAKARI: Mtu mwadilifu hutanguliza nini, iwe yeye ni tajiri au maskini?—Lu 12:21; w07 8/1 29 ¶12.