WIMBO NA 76
Unahisije?
Makala Iliyochapishwa
1. We‘ unahisije
kuhusu kuhubiri?
Kuwafundisha watu
wanaopendezwa?
Ujitahidipo
Kutimiza huduma
Na Yehova afanye
kazi ya kukuza.
(KORASI)
Tuna shangwe, twafurahi
kujitoa kikamili.
Basi tumsifu Mungu.
Daima dawamu.
2. We‘ unahisije
wanaposikiliza?
Wanapoitikia
ujumbe wa kweli?
Hata wakatae
bado twautangaza.
Twafurahi kuitwa kwa
jina la Mungu.
(KORASI)
Tuna shangwe, twafurahi
kujitoa kikamili.
Basi tumsifu Mungu.
Daima dawamu.
3. We‘ unahisije
kuwa na pendeleo,
Alilotupa Mungu
la kumwakilisha?
Tunajivunia
kutangaza Ufalme
Kuwatafuta watu
wanaostahili.
(KORASI)
Tuna shangwe, twafurahi
kujitoa kikamili.
Basi tumsifu Mungu.
Daima dawamu.
(Ona pia Mdo. 13:48; 1 The. 2:4; 1 Tim. 1:11.)