Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g03 2/22 uku. 31
  • “Amkeni! Iliokoa Uhai Wangu!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Amkeni! Iliokoa Uhai Wangu!”
  • Amkeni!—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Biblia Itakaziwa Zaidi
    Huduma ya Ufalme—2005
  • Kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2006
  • Kutambua Dalili na Kuchukua Hatua
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2003
g03 2/22 uku. 31

“Amkeni! Iliokoa Uhai Wangu!”

Wachapishaji wa gazeti la Amkeni! walipokea barua ya shukrani kutoka Italia. Sehemu ya barua hiyo inasema hivi:

“Nimesoma Amkeni! kwa muda wa miaka 40, na ninapendezwa na mambo mengi mbalimbali yanayozungumziwa. Hivi majuzi nilipokuwa kazini, nilihisi maumivu makali tumboni na kifuani. Niliamua kwenda nyumbani, lakini nilipohisi maumivu hayo tena, nilikumbuka jambo fulani nililokuwa nimesoma katika makala fulani ya Amkeni! iliyoeleza kuhusu dalili za mshtuko wa moyo. a Niliamua kwenda hospitalini. Nilipokuwa katika chumba cha kungoja kumwona daktari, kichwa changu kilining’nia upande mmoja na nikazirai. Niliambiwa jambo hilo siku iliyofuata nilipokuwa katika chumba cha kuwatunzia wagonjwa mahututi.

“Niko hai leo kwa sababu madaktari stadi walinishughulikia haraka. Hata hivyo, ninawashukuru kwa gazeti lenu ambalo lilinipa habari iliyonisaidia kufanya uamuzi wa busara wa kwenda hospitalini. Amkeni! iliokoa uhai wangu!”

[Maelezo ya Chini]

a Ona toleo letu la Desemba 8, 1996, ukurasa wa 6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki