Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 1/11 uku. 14
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Tunahitaji Viini Zaidi?
  • Watu Hawawajibiki Kazini Siku Hizi
  • Mzozo Kuhusu Mpaka “Wasuluhishwa”
  • Calcutta—Jiji Lenye Pilikapilika na Utofautiano
    Amkeni!—1998
  • Kisiwa Kilichotokea na Kutoweka
    Amkeni!—2004
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
  • Kisasi cha Vijiumbe-Maradhi
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 1/11 uku. 14

Kuutazama Ulimwengu

Kwa wastani, daktari mmoja nchini Tanzania anawahudumia watu 64,000.—THE CITIZEN, TANZANIA.

‘Angalau maskini bilioni 1 wanaishi wakiwa na utapiamlo wa kudumu, na Malengo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza idadi ya watu walio na njaa ulimwenguni kufikia 2015, hayatafikiwa.’—SCIENCE, MAREKANI.

“Kampuni 100 kubwa zaidi ulimwenguni zinazotengeneza silaha” ziliuza silaha zinazogharimu dola bilioni 385 katika mwaka wa 2008, ongezeko la dola bilioni 39 kuliko ilivyokuwa katika mwaka wa 2007.—TAASISI YA UCHUNGUZI WA AMANI YA KIMATAIFA YA STOCKHOLM, SWEDEN.

Je, Tunahitaji Viini Zaidi?

Thomas McDade, ambaye ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Northwestern, Illinois, Marekani, alisema hivi: “Utafiti wetu umeonyesha kwamba kuna uwezekano wa watoto waliolelewa katika mazingira safi kupita kiasi, kupata miwasho mingi zaidi wanapokuwa watu wazima na hivyo kuambukizwa magonjwa mengi.” Katika uchunguzi fulani uliohusisha watoto Wafilipino na wale Wamarekani, ilionekana kwamba kwa ujumla wale Wafilipino waliambukizwa magonjwa mengi zaidi kuliko wale Wamarekani walipokuwa wachanga. Hata hivyo, tofauti na matarajio ya wengi, damu ya vijana wengi Wafilipino ilikuwa na viwango vya chini vya protini ambayo huangamiza na kuondoa viini mwilini na ambayo huongezeka miwasho inapotokea. Tunajifunza nini kutokana na utafiti huo? Mtu anapoathiriwa na bakteria za kawaida anapokuwa mtoto, anapata kinga ya magonjwa hatari anapokuwa mtu mzima.

Watu Hawawajibiki Kazini Siku Hizi

Waajiri wengi nchini Finland wanashangazwa sana na kizazi kipya cha watu ambao hawajui hata kidogo jinsi ya kuwa na uhusiano mzuri pamoja na watu ambao utawasaidia kudumisha kazi. Anne Mikkola msimamizi wa mkahawa fulani alisema hivi alipokuwa akihojiwa na shirika la kitaifa la utangazaji nchini Finland: “Wakati mwingi makurutu hufikiri kwamba saa za kazi zilizowekwa rasmi zinaweza kubadilishwa wakati wowote ule.” Pia wao huwa na matatizo ya kutambua jinsi ya kujiendesha na kuvaa. Hasa mahali pa kazi ambapo wanashughulika na umma, mara nyingi waajiri wanalazimika kuwatajia ni mavazi gani ambayo hawapaswi kuvaa. Uthibitisho mwingine unaoonyesha kwamba waajiriwa wapya hawatofautishi kazi na maisha yao ya kibinafsi unaonekana wakati marafiki wao wanapokuja kazini ili tu kuwatembelea.

Mzozo Kuhusu Mpaka “Wasuluhishwa”

Mzozo ambao umekuwepo kwa muda mrefu kati ya Bangladesh na India kuhusu kisiwa kimoja kidogo katika Ghuba ya Bengal sasa umesuluhishwa baada ya maji kuongezeka. Wahindi huliita eneo hilo lisilokaliwa Kisiwa cha New Moore, nao Wabangladeshi huliita Kisiwa cha South Talpatti. Eneo hilo halijawahi kuinuka zaidi ya mita 1.9 juu ya usawa wa bahari. Hata hivyo, picha za satelaiti zinaonyesha kwamba sasa eneo hilo limefunikwa na maji. Profesa Sugata Hazra wa Chuo Kikuu cha Elimu ya Bahari cha Jadavpur huko Calcutta anasema, “Jambo ambalo nchi hizi mbili zilishindwa kusuluhisha kwa kujadiliana kwa miaka mingi, limesuluhishwa na kuongezeka kwa joto duniani.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki