Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/12 kur. 15-17
  • Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?
  • Amkeni!—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Umaarufu Mtandaoni Ni Muhimu Kadiri Gani?
    Vijana Huuliza
  • Nifanye Nini Ninapoonewa?
    Vijana Huuliza
  • Nifanye Nini Ninapoonewa Shuleni?
    Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Nifanye Nini Ikiwa Inaonekana Wengine Hawanipendi?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 3/12 kur. 15-17

Vijana Huuliza

Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?

Andika maneno yatakayokamilisha sentensi ifuatayo:

Ni vizuri ․․․․․ kuwa maarufu.

A. nyakati zote

B. nyakati fulani

C. usiwahi kamwe

JIBU sahihi ni “B.” Kwa nini? Kwa sababu kuwa maarufu humaanisha kwamba unapendwa na watu wengi—na hilo si jambo baya! Biblia ilitabiri kwamba Wakristo wangekuwa “nuru ya mataifa” na kwamba watu wangevutwa kwao. (Isaya 42:6; Matendo 13:47) Kwa njia hiyo, inaweza kusemwa kuwa Wakristo ni watu maarufu.

Je, wajua? Yesu alikuwa maarufu. Hata alipokuwa kijana, alipata “kibali kwa Mungu na wanadamu.” (Luka 2:52) Na Biblia inasema kwamba Yesu alipokuwa mtu mzima, “umati mkubwa ukamfuata kutoka Galilaya na Dekapoli na Yerusalemu na Yudea na kutoka upande ule mwingine wa Yordani.”—Mathayo 4:25.

Kwa nini jambo hilo lilifaa? Kwa sababu Yesu hakutaka utukufu au kujitafutia umaarufu, na hakuwa akiomba-omba kibali cha watu wengine. Yesu alifanya alichopaswa kufanya—jambo ambalo nyakati nyingine lilimfanya awe maarufu. (Yohana 8:29, 30) Wakati huohuo, Yesu alitambua kwamba, kibali alichopata kutoka kwa watu ambao hawakuwa na msimamo kilikuwa cha muda mfupi tu. Alisema wazi kwamba baadaye watu wangemuua!—Luka 9: 22.

Jambo Muhimu: Umaarufu ni kama utajiri. Si mara zote kuwa tajiri ni vibaya. Tatizo ni jinsi watu wanavyong’ang’ana kuupata—au kuudumisha.

Tahadhari! Vijana wengi hufanya juu chini ili wawe maarufu. Wengine wako tayari kufanya chochote ambacho watu wengi wanawashinikiza kufanya mradi tu wawe maarufu. Wengine ni waonevu wanaowalazimisha wengine wapendezwe nao—hata kama ni kwa sababu tu wanawaogopa.a

Katika kurasa zinazofuata, tutazungumzia njia hizo mbili mbaya za kujipatia umaarufu. Halafu tutachunguza njia bora ya kufanya hivyo.

Unaweza kupata makala zaidi za “Vijana Huuliza” katika Tovuti ya www.watchtower.org/ype

[Maelezo ya Chini]

a Biblia inawataja waonevu walioitwa “Wanefili,” ambao pia wanajulikana kama “wanaume wenye sifa.” Lengo lao kuu lilikuwa kujitafutia utukufu wao wenyewe.—Mwanzo 6:4.

[Sanduku/​Picha katika ukurasa wa 16, 17]

NJIA ZA KUJIPATIA UMAARUFU

KUJIPENDEKEZA KWA WATU

Nataka nikubaliwe na watu.

Ili nifaulu, lazima niige tabia zao.

“Nilijaribu kubadili tabia zangu ili nikubaliwe na wengine. Mwanzoni, ilionekana kama ninafaulu. Lakini baadaye nikagundua kwamba hupaswi kubadili utu wako ili tu ukubaliwe na watu.”—Nicole.

Kanuni ya Biblia: “Usiufuate umati kwa ajili ya makusudio maovu; wala . . . kugeuka kando pamoja na umati kwa kusudi la kupotosha haki.”—Kutoka 23:2.

UONEVU

Tayari watu wananipenda na nataka mambo yaendelee hivyo.

Nitafanya juu chini niendelee kuwa maarufu—hata kama itamaanisha kuwakandamiza wengine.

“Ni kawaida kwa vijana kuwadhulumu wenzao, na kwa kuwa wale ambao huwaonea wengine huwa maarufu sana, mtu mwenye haya ataamini chochote wanachosema.”—Raquel.

Kanuni ya Biblia: “Kama vile mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni wao vivyo hivyo.”—Luka 6:31.

NJIA INAYOFAA ZAIDI

1 Fahamu viwango vyako. Biblia inasema kwamba watu wakomavu ‘wamezoezwa kutofautisha yaliyo sawa na yaliyo makosa pia.’—Waebrania 5:14.

2 Shikilia mambo unayoamini. Uwe kama Yoshua ambaye alisema hivi kwa usadikisho: “Jichagulieni leo yule mtakayemtumikia . . . Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Yehova.”—Yoshua 24:15.

3 Uwe na uhakika kuhusu njia ya maisha uliyochagua. Mtume Paulo alimkumbusha Timotheo: “Mungu hakutupa sisi roho ya woga, bali ile ya nguvu.”—2 Timotheo 1:7.

Ukitumia njia hii ya tatu, huenda usiwe maarufu​—lakini utapendwa na watu wanaofaa!

[Sanduku/​Picha katika ukurasa 16, 17]

MAMBO AMBAYO VIJANA WENZAKO WANASEMA

Melissa​—Ni kweli kwamba unaweza kujaribu kuwa kama vijana wengine wote shuleni. Lakini hilo ni jambo linalochosha sana! Kuwa Mkristo kunakufanya uwe wa pekee kwa njia nzuri. Hakukufanyi uonekane kuwa mtu wa ajabu-ajabu. Kunafanya upendwe na watu.

Ashley​—Nikiwa shuleni, nilihisi kuwa sipendwi na watu, lakini ningehudhuria mkutano wa Kikristo na kukutana na marafiki walionipenda. Wakati huo, tamaa yoyote ya kutaka kupendwa na wanashule wenzangu ilififia.

Phillip​—Siri ya kukubaliwa na wengine ni kupendezwa nao kibinafsi. Hivi majuzi nimejaribu kuwafanyia rafiki zangu mambo madogo-madogo, na jambo hilo limenivuta karibu nao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki