Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 12/15 uku. 3
  • Ni Nini Chanzo cha Ugomvi Katika Familia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nini Chanzo cha Ugomvi Katika Familia?
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Yakobo na Esau Wafanya Amani
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mwenendo Mwema Waunganisha Jamaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • ‘Tafuta Amani na Uifuatie’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Jinsi ya Kuchangia Amani Katika Familia
    Amkeni!—2015
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 12/15 uku. 3
Watoto wanahuzunishwa wanaposikia wazazi wakibishana

HABARI KUU | KUDUMISHA AMANI NYUMBANI

Ni Nini Chanzo cha Ugomvi Katika Familia?

“KAWAIDA sisi hugombana kuhusu pesa,” anasema Sarah,a anayeishi nchini Ghana, na ambaye aliolewa na Jacob miaka 17 iliyopita. Anaeleza hivi: “Kinachonikasirisha ni kwamba mimi hufanya mengi sana ili kuitunza familia yangu lakini Jacob hanihusishi anapofanya maamuzi kuhusu pesa. Majuma kadhaa yanaweza kupita bila sisi kuzungumza.”

Mume wake anayeitwa Jacob anasema hivi: “Ndiyo, kuna nyakati ambapo tunarushiana maneno makali. Hilo hutokea kwa sababu ya kutoelewana na kutowasiliana. Pia, mizozo hiyo hutokea kwa sababu ya kukasirika kupita kiasi hali fulani zinapotokea.”

Nathan, aliyefunga ndoa hivi karibuni nchini India, anaeleza jinsi hali ilivyokuwa baba-mkwe wake alipomfokea mama-mkwe. Nathan anasema hivi: “Mama-mkwe alikasirika sana akatoka nje. Nilipomwuliza kwa nini alimfokea, baba-mkwe alinigeukia akifikiri ninamtukana. Ghafla sisi sote tukaanza kufokewa.”

Huenda hata wewe umejionea jinsi maneno fulani yanayosemwa wakati usiofaa au ambayo hayajachaguliwa vizuri yanavyoweza kutokeza mzozo mkubwa nyumbani. Watu waliokuwa wakijadiliana kwa utulivu wanaweza ghafla kuanza kurushiana maneno. Kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuzungumza kwa njia inayofaa kila wakati, ni rahisi sana kuelewa vibaya maneno au nia ya mwenzako. Hata hivyo, inawezekana kuwa na amani na umoja.

Unaweza kufanya nini mabishano makali yanapotokea? Unaweza kuchukua hatua gani ili kudumisha amani na utulivu katika familia? Familia zinaweza kudumishaje amani nyumbani? Tafadhali endelea kusoma.

a Baadhi ya majina katika makala hii yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki