YEREMIA YALIYOMO 1 Yeremia awekwa kuwa nabii (1-10) Maono ya mti wa mlozi (11, 12) Maono ya chungu cha kupikia (13-16) Yeremia atiwa nguvu kwa ajili ya utume wake (17-19) 2 Waisraeli wamwacha Yehova na kuanza kuabudu miungu mingine (1-37) Israeli ni kama mzabibu wa kigeni (21) Pindo za nguo zake zina madoa ya damu (34) 3 Kina cha uasi imani wa Israeli (1-5) Israeli na Yuda wana hatia ya uzinzi (6-11) Mwito wa kutubu (12-25) 4 Kutubu kunaleta baraka (1-4) Msiba utakuja kutoka kaskazini (5-18) Uchungu wa Yeremia kuhusu msiba unaokuja (19-31) 5 Watu wakataa nidhamu ya Yehova (1-13) Wataharibiwa lakini hawataangamizwa kabisa (14-19) Yehova awaadhibu watu (20-31) 6 Kuzingirwa kwa Yerusalemu kunakaribia (1-9) Ghadhabu ya Yehova dhidi ya Yerusalemu (10-21) Wanasema “Kuna amani!” wakati hakuna amani (14) Watavamiwa kikatili kutoka kaskazini (22-26) Yeremia atakuwa mpimaji wa madini (27-30) 7 Tumaini la uwongo katika hekalu la Yehova (1-11) Hekalu litakuwa kama Shilo (12-15) Ibada ya kidesturi yashutumiwa (16-34) “Malkia wa Mbinguni” aabudiwa (18) Kutoa watoto dhabihu huko Hinomu (31) 8 Watu wachagua njia inayopendwa na wengi (1-7) Kuna hekima gani bila neno la Yehova? (8-17) Yeremia aomboleza kwa sababu ya kuvunjika kwa Yuda (18-22) “Je, hakuna zeri kule Gileadi?” (22) 9 Yeremia ahuzunika sana (1-3a) Yehova aiadhibu Yuda (3b-16) Nchi ya Yuda yaombolezewa (17-22) Jigambe kuhusu kumjua Yehova (23-26) 10 Mungu aliye hai atofautishwa na miungu ya mataifa (1-16) Uharibifu na uhamisho unaokuja (17, 18) Yeremia aomboleza (19-22) Sala ya nabii (23-25) Mwanadamu hawezi kuongoza hatua yake mwenyewe (23) 11 Yuda avunja agano lake pamoja na Mungu (1-17) Miungu mingi kama majiji (13) Yeremia afananishwa na mwanakondoo anayepelekwa machinjioni (18-20) Yeremia apingwa na watu wa mji wa nyumbani kwao (21-23) 12 Yeremia alalamika (1-4) Jibu la Yehova (5-17) 13 Mshipi wa kitani ulioharibika (1-11) Mitungi ya divai itavunjwavunjwa (12-14) Watu wa Yuda wasioweza kubadilika watapelekwa uhamishoni (15-27) “Je, Mkushi anaweza kuibadili ngozi yake?” (23) 14 Ukame, njaa kali, na upanga (1-12) Manabii wa uwongo washutumiwa (13-18) Yeremia akiri dhambi za watu (19-22) 15 Yehova hatabadili hukumu yake (1-9) Yeremia alalamika (10) Jibu la Yehova (11-14) Sala ya Yeremia (15-18) Apata furaha kwa kula maneno ya Mungu (16) Yehova amtia nguvu Yeremia (19-21) 16 Yeremia hapaswi kuoa, kuomboleza, wala kusherehekea (1-9) Adhabu, kisha kurudishwa (10-21) 17 Dhambi ya Yuda imetia mizizi (1-4) Baraka za kumtumaini Yehova (5-8) Moyo wenye hila (9-11) Yehova, tumaini la Israeli (12, 13) Sala ya Yeremia (14-18) Kuishika Sabato ikiwa siku takatifu (19-27) 18 Udongo mikononi mwa mfinyanzi (1-12) Yehova awageuzia Israeli mgongo (13-17) Njama dhidi ya Yeremia; ombi lake (18-23) 19 Yeremia aambiwa avunje chupa ya udongo (1-15) Kumtolea Baali dhabihu za watoto (5) 20 Pashuri ampiga Yeremia (1-6) Yeremia hawezi kuacha kuhubiri (7-13) Ujumbe wa Mungu ni kama moto unaowaka (9) Yehova ni kama shujaa anayetisha (11) Yeremia alalamika (14-18) 21 Yehova akataa ombi la Sedekia (1-7) Watu kuchagua uzima au kifo (8-14) 22 Ujumbe wa hukumu dhidi ya wafalme waovu (1-30) Kumhusu Shalumu (10-12) Kumhusu Yehoyakimu (13-23) Kumhusu Konia (24-30) 23 Wachungaji wazuri na wabaya (1-4) Usalama chini ya “chipukizi adilifu” (5-8) Manabii wa uwongo washutumiwa (9-32) “Mzigo” wa Yehova (33-40) 24 Tini nzuri na tini mbaya (1-10) 25 Kesi ya Yehova dhidi ya mataifa (1-38) Mataifa yatatumikia Babiloni kwa miaka 70 (11) Kikombe cha divai ya ghadhabu ya Mungu (15) Msiba kutoka taifa moja hadi lingine (32) Wale ambao Yehova atawaua (33) 26 Maadui watishia kumuua Yeremia (1-15) Yeremia aokolewa (16-19) Unabii wa Mika wanukuliwa (18) Nabii Uriya (20-24) 27 Nira ya Babiloni (1-11) Sedekia aambiwa ajitiishe kwa Babiloni (12-22) 28 Nabii wa uwongo Hanania ampinga nabii Yeremia (1-17) 29 Barua ya Yeremia kwa watu walio uhamishoni Babiloni (1-23) Waisraeli watarudi baada ya miaka 70 (10) Ujumbe kwa Shemaya (24-32) 30 Ahadi za kurudishwa na kuponywa (1-24) 31 Waisraeli waliobaki wataishi tena nchini (1-30) Raheli awaombolezea watoto wake (15) Agano jipya (31-40) 32 Yeremia anunua shamba (1-15) Sala ya Yeremia (16-25) Jibu la Yehova (26-44) 33 Ahadi ya kurudishwa (1-13) Usalama chini ya “chipukizi adilifu” (14-16) Agano pamoja na Daudi na makuhani (17-26) Agano kuhusu mchana na usiku (20) 34 Ujumbe wa hukumu kwa Sedekia (1-7) Agano la kuwaachilia huru watumwa lavunjwa (8-22) 35 Warekabu waonyesha utii wa pekee (1-19) 36 Yeremia asema mambo kisha yaandikwa katika kitabu cha kukunjwa (1-7)(1-7) Baruku asoma kwa sauti kitabu cha kukunjwa (8-19) Yehoyakimu akichoma moto kitabu hicho cha kukunjwa (20-26) Ujumbe waandikwa tena kwenye kitabu kipya cha kukunjwa (27-32) 37 Wakaldayo wataondoka kwa muda mfupi tu (1-10) Yeremia afungwa gerezani (11-16) Sedekia akutana na Yeremia (17-21) Yeremia apewa mkate (21) 38 Yeremia atupwa ndani ya tangi (1-6) Ebed-meleki amwokoa Yeremia (7-13) Yeremia amsihi Sedekia ajisalimishe (14-28) 39 Kuanguka kwa Yerusalemu (1-10) Sedekia akimbia kisha akamatwa (4-7) Yeremia atalindwa (11-14) Uhai wa Ebed-meleki utaokolewa (15-18) 40 Nebuzaradani amwachilia huru Yeremia (1-6) Gedalia awekwa kuwa msimamizi nchini (7-12) Njama dhidi ya Gedalia (13-16) 41 Ishmaeli amuua Gedalia (1-10) Yohanani amfanya Ishmaeli akimbie (11-18) 42 Watu wamwomba Yeremia asali ili wapate mwongozo (1-6) Yehova ajibu hivi: “Msiende Misri” (7-22) 43 Watu wakataa kutii kisha waenda Misri (1-7) Neno la Yehova kwa Yeremia nchini Misri (8-13) 44 Msiba watabiriwa dhidi ya Wayahudi walio Misri (1-14) Watu wakataa onyo la Mungu (15-30) “Malkia wa Mbinguni” aabudiwa (17-19) 45 Ujumbe wa Yehova kwa Baruku (1-5) 46 Unabii dhidi ya Misri (1-26) Misri itashindwa na Nebukadneza (13, 26) Ahadi kwa Israeli (27, 28) 47 Unabii dhidi ya Wafilisti (1-7) 48 Unabii dhidi ya Moabu (1-47) 49 Unabii dhidi ya Amoni (1-6) Unabii dhidi ya Edomu (7-22) Nchi ya Edomu haitakuwa taifa tena (17, 18) Unabii dhidi ya Damasko (23-27) Unabii dhidi ya Kedari na Hasori (28-33) Unabii dhidi ya Elamu (34-39) 50 Unabii dhidi ya Babiloni (1-46) Kimbieni kutoka Babiloni (8) Watu wa Israeli watarudishwa (17-19) Maji ya Babiloni yatakaushwa kabisa (38) Babiloni halitakaliwa tena (39, 40) 51 Unabii dhidi ya Babiloni (1-64) Babiloni litashindwa ghafla na Wamedi (8-12) Kitabu chatupwa ndani ya Mto Efrati (59-64) 52 Sedekia aasi Babiloni (1-3) Nebukadneza azingira Yerusalemu (4-11) Kuharibiwa kwa jiji na hekalu (12-23) Watu wapelekwa uhamishoni Babiloni (24-30) Yehoyakini aachiliwa huru kutoka gerezani (31-34)