Waroma
14 Karibisheni mtu aliye na udhaifu katika imani yake, lakini si ili kufanya maamuzi juu ya maswali-maswali ya kindani. 2 Mtu mmoja ana imani ya kula kila kitu, lakini mtu aliye dhaifu hula mboga. 3 Acheni yeye anayekula asimdharau yeye asiyekula, na acheni yeye asiyekula asimhukumu yeye anayekula, kwa maana Mungu amemkaribisha huyo. 4 Wewe ni nani umhukumu mtumishi wa nyumbani wa mwingine? Kwa bwana-mkubwa wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Kwa kweli, atafanywa asimame, kwa maana Yehova aweza kumfanya asimame.
5 Mtu mmoja huhukumu siku moja kuwa juu ya nyingine; mtu mwingine huhukumu siku moja kuwa kama nyingine zote; acheni kila mtu awe amesadiki kikamili katika akili yake mwenyewe. 6 Yeye aiadhimishaye siku huiadhimisha kwa Yehova. Pia, yeye alaye, hula kwa Yehova, kwa maana yeye humshukuru Mungu; na yeye asiyekula hali kwa Yehova, na bado humshukuru Mungu. 7 Kwa kweli, hakuna hata mmoja kati yetu aishiye kwa habari yake mwenyewe tu, na hakuna yeyote afaye kwa habari yake mwenyewe tu; 8 kwa maana tukiishi, twaishi kwa Yehova, na tukifa, twafa kwa Yehova pia. Kwa hiyo tukiishi na tukifa pia, sisi ni wa Yehova. 9 Kwa maana kwa madhumuni haya Kristo alikufa na kuja kwenye uhai tena, ili apate kuwa Bwana juu ya wafu na walio hai pia.
10 Lakini kwa nini wewe wahukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe pia wadharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu; 11 kwa maana imeandikwa: “‘Kama niishivyo,’ asema Yehova, ‘kwangu kila goti litakunjwa, na kila ulimi utakiri waziwazi kwa Mungu.’” 12 Hivyo, basi kila mmoja wetu atatoa hesabu kwa Mungu kwa ajili yake mwenyewe.
13 Kwa hiyo acheni sisi tusiwe tukihukumiana tena, bali badala ya hivyo fanyeni hili kuwa uamuzi wenu, kutokuweka mbele ya ndugu kipingamizi chenye kukwaza au sababu ya kukwaza. 14 Najua nami nashawishwa katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu kilicho najisi katika chenyewe; ni pale tu ambapo mtu afikiria kitu fulani kuwa najisi, hicho huwa najisi kwake. 15 Kwa maana ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anatiwa kihoro, wewe hutembei tena kupatana na upendo. Kwa chakula chako usimwangamize yule ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa. 16 Kwa hiyo, nyinyi watu msiache jema mlifanyalo lisemwe kwa ubaya kwenu. 17 Kwa maana ufalme wa Mungu haumaanishi kula na kunywa, bali wamaanisha uadilifu na amani na shangwe pamoja na roho takatifu. 18 Kwa maana yeye ambaye kwa habari hii atumikia Kristo kama mtumwa ni mwenye kukubalika kwa Mungu na ana kibali cha wanadamu.
19 Hivyo, basi, acheni tufuatie mambo yafanyayo kuwe na amani na mambo yaliyo ya kujengana. 20 Komeni kuibomoa kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula tu. Ni kweli, vitu vyote ni safi, lakini ni jambo baya kwa mtu ambaye ala kukiwa na sababu ya kukwaza. 21 Ni vema kutokula nyama au kunywa divai au kufanya jambo lolote ambalo juu yalo ndugu yako akwazika. 22 Imani uliyo nayo, uwe nayo kupatana na wewe mwenyewe mbele ya macho ya Mungu. Mwenye furaha ni mtu asiyejiweka mwenyewe hukumuni kwa lile akubalilo. 23 Lakini ikiwa anazo shaka, tayari amehukumiwa kuwa mwenye hatia ikiwa yeye ala, kwa sababu hali kwa imani. Kwa kweli, kila kitu ambacho si kwa imani ni dhambi.