Waroma
13 Acheni kila nafsi iwe katika ujitiisho kwa mamlaka zilizo kubwa, kwa maana hakuna mamlaka ila kwa njia ya Mungu; mamlaka zilizopo zimesimama zikiwa zimewekwa na Mungu katika mahali pa vyeo vyazo vyenye kuhusu. 2 Kwa hiyo yeye aipingaye mamlaka amechukua msimamo dhidi ya mpango wa Mungu; wale ambao wamechukua msimamo dhidi ya huo watapokea hukumu juu yao wenyewe. 3 Kwa maana wale wanaotawala ni kitu cha hofu, si kwa kitendo kilicho chema, bali kwa kilicho kibaya. Basi, je, wataka usiwe na hofu yoyote kwa hiyo mamlaka? Fuliza kufanya lililo jema, nawe utakuwa na sifa kutoka kwayo; 4 kwa maana hiyo ni mhudumu wa Mungu kwako kwa faida yako. Lakini ikiwa unafanya lililo baya, uwe katika hofu: kwa maana haichukui upanga bila kusudi; kwa maana hiyo ni mhudumu wa Mungu, mlipiza-kisasi ili kuonyesha hasira ya kisasi juu ya yeye anayezoea kufanya lililo baya.
5 Kwa hiyo kuna sababu yenye kushurutisha nyinyi watu kuwa katika ujitiisho, si kwa sababu ya hasira hiyo ya kisasi tu, bali pia kwa sababu ya dhamiri yenu. 6 Kwa maana hiyo ndiyo sababu mnalipa kodi pia; kwa maana wao ni watumishi wa Mungu wa watu wote wakitumikia daima kwa kusudi hilihili. 7 Walipeni wote haki zao, kwa yeye atakaye kodi, kodi; kwa yeye atakaye ushuru, ushuru; kwa yeye atakaye hofu, hofu hiyo; kwa yeye atakaye heshima, heshima hiyo.
8 Nyinyi watu msiwe mkiwiwa na yeyote hata jambo moja, ila kupendana; kwa maana yeye apendaye binadamu-mwenziye ametimiza sheria. 9 Kwa maana mfumo wa sheria, “Lazima usifanye uzinzi, Lazima usiue kimakusudi, Lazima usiibe, Lazima usitamani,” na amri nyingine yoyote iliyoko, imejumlishwa katika neno hili, yaani, “Lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.” 10 Upendo haufanyi ovu kwa jirani ya mtu; kwa hiyo upendo ndio utimizo wa sheria.
11 Fanyeni hili, pia, kwa sababu nyinyi watu mwayajua majira, kwamba tayari ni saa ya nyinyi kuamka kutoka katika usingizi, kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu zaidi kuliko tulipopata kuwa waamini. 12 Usiku umesonga sana; mchana umekaribia. Kwa hiyo acheni tuondoe kazi za giza na acheni tuvae silaha za nuru. 13 Kama katika wakati wa mchana acheni tujiendeshe kwa adabu, si katika sherehe zenye makelele ya ulevi na vipindi vya kulewa, si katika ngono isiyo halali na mwenendo mlegevu, si katika zogo na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, na msiwe mkipanga kimbele kwa ajili ya tamaa za mwili.