1 Wakorintho
16 Sasa kuhusu mchango ulio kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoyapa maagizo makutaniko ya Galatia, nyinyi wenyewe pia fanyeni kwa njia hiyohiyo. 2 Kila siku ya kwanza ya juma acheni kila mmoja wenu kwenye nyumba yake mwenyewe aweke kando kitu fulani katika akiba kama aelekeavyo kuwa anafanikiwa, ili niwasilipo michango isitukie wakati huo. 3 Lakini nifikapo huko, watu wowote wale mwakubalio kwa barua, hao nitawatuma kupeleka zawadi yenu ya fadhili hadi Yerusalemu. 4 Hata hivyo, ikiwa yanifaa mimi kwenda huko pia, wao wataenda huko pamoja nami.
5 Lakini nitawajia nyinyi wakati nimekwisha kwenda kupitia Makedonia, kwa maana ninaenda kupitia Makedonia; 6 na labda nitakaa au hata nitapisha majira ya baridi kali nikiwa pamoja nanyi, ili mpate kuniongoza mahali ambapo huenda nikawa nikienda. 7 Kwa maana sitaki kuwaona nyinyi sasa tu wakati wa kupita kwangu, kwa maana natumaini kukaa wakati fulani pamoja nanyi, Yehova akiruhusu. 8 Lakini ninakaa katika Efeso mpaka msherehekeo wa Pentekoste; 9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa uongozao kwenye utendaji, lakini kuna wapingaji wengi.
10 Hata hivyo, Timotheo akiwasili, angalieni kwamba awa bila hofu miongoni mwenu, kwa maana anaifanya kazi ya Yehova, kama vile mimi. 11 Kwa hiyo, msiache mtu yeyote amdharau. Mwongozeni kwa amani, ili apate kunifikia hapa, kwa maana ninamngoja nikiwa pamoja na akina ndugu.
12 Sasa kuhusu Apolo ndugu yetu, nilimsihi sana kwa bidii awajie nyinyi akiwa na akina ndugu, na bado hayakuwa mapenzi yake hata kidogo aje sasa; lakini atakuja apatapo fursa.
13 Kaeni macho, simameni imara katika imani, endeleeni kama wanaume, kueni mwe wenye uweza. 14 Acheni mambo yenu yote yatendeke kwa upendo.
15 Sasa nawahimiza nyinyi kwa bidii, akina ndugu: Mwajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefanasi ndio matunda ya kwanza ya Akaya na kwamba walijitia katika kuwahudumia watakatifu. 16 Nyinyi pia mpate kufuliza kujinyenyekeza wenyewe kwa watu wa aina hiyo na kwa kila mtu anayeshirikiana na kufanya kazi ya jasho. 17 Lakini nashangilia kuwapo kwa Stefanasi na Fortunato na Akaiko, kwa sababu wao wamejazia kutokuwa kwenu hapa. 18 Kwa maana wameburudisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo watambueni watu wa namna hiyo.
19 Makutaniko ya Asia yawapelekea nyinyi salamu zao. Akila na Priska pamoja na kutaniko lililo katika nyumba yao wawasalimu nyinyi kwa ukunjufu wa moyo katika Bwana. 20 Ndugu wote wawasalimu nyinyi. Salimianeni kwa busu takatifu.
21 Hii ni salamu yangu, ya Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe.
22 Ikiwa yeyote hana shauku na Bwana, acheni awe mwenye kulaaniwa. Ee Bwana wetu, uje! 23 Fadhili isiyostahiliwa ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. 24 Upendo wangu na uwe pamoja na nyinyi nyote katika muungano pamoja na Kristo Yesu.