28 Watu wa jiji walipoamka asubuhi na mapema kama kawaida, tazama! madhabahu ya Baali ilikuwa imebomolewa na ule mti mtakatifu+ uliokuwa kando yake ulikuwa umekatwa, na yule ng’ombe-dume mchanga wa pili alikuwa ametolewa juu ya madhabahu ambayo ilikuwa imejengwa.