6 Ndipo roho ya Yehova ikaanza kutenda kazi juu yake,+ naye akampasua vipande viwili, kama vile mtu anavyompasua mwana-mbuzi vipande viwili, wala hapakuwa na kitu chochote mkononi mwake. Naye hakumwambia baba yake wala mama yake jambo alilokuwa amefanya.