3 Ndipo mfalme wa Israeli akawaambia watumishi wake: “Je, kweli hamjui kwamba Ramothi-gileadi+ ni jiji letu? Na bado tunasitasita kulichukua kutoka mkononi mwa mfalme wa Siria.”
14 Ndipo akaingia kwa mfalme, naye mfalme akamwambia: “Mikaya, je, twende kupiga vita juu ya Ramothi-gileadi, au nijiepushe?” Mara moja akasema: “Panda uende na kufanikiwa; nao watatiwa mkononi mwenu.”+