11 Lakini mwaka wa saba utaliacha bila kulimwa nawe utaliacha lipumzike,+ nao maskini wa watu wako watakula kutokana nalo; nacho kile ambacho wataacha kitaliwa na wanyama wa mwituni.+ Hivyo ndivyo utakavyofanya na shamba lako la mizabibu na shamba lako la mizeituni.
4 Lakini katika mwaka wa saba kutakuwa na sabato ya pumziko kamili kwa ajili ya nchi hiyo,+ sabato kwa Yehova. Shamba lako hutalipanda mbegu, nalo shamba lako la mizabibu hutalikata matawi.