26 Ndipo akamwambia: “Je, moyo wangu haukukufuata wakati yule mtu alipogeuka na kushuka kutoka katika gari lake ili kukupokea? Je, ni wakati wa kupokea fedha au kupokea mavazi au mashamba ya mizeituni au ya mizabibu au kondoo au ng’ombe au watumishi wa kiume na wajakazi?+