22 Mara moja yule mwanamke akaenda kwa watu wote kwa hekima yake,+ nao wakakikata kichwa cha Sheba mwana wa Bikri, wakamtupia Yoabu. Basi akapiga baragumu,+ nao wakatawanyika kutoka kwenye jiji lile, kila mmoja akaenda nyumbani kwake; naye Yoabu akarudi Yerusalemu kwa mfalme.