17 “‘Na mwanamume akimchukua dada yake, binti ya baba yake au binti ya mama yake, naye auone uchi wake, naye dada yake auone uchi wake, ni aibu.+ Kwa hiyo watakatiliwa mbali kutoka machoni pa wana wa watu wao. Ni uchi wa dada yake ambao ameufunua. Atajibu kwa kosa lake.