19 nawe utakaribia mbele ya wana wa Amoni. Usiwasumbue wala usigombane nao, kwa sababu sitakupa sehemu yoyote ya nchi ya wana wa Amoni iwe miliki yako, kwa maana nimewapa wana wa Loti iwe miliki yao.+
17 Na ni Yeye amewapigia kura, na mkono wake mwenyewe umewagawia mahali hapo kwa kamba ya kupimia.+ Wataimiliki mpaka wakati usio na kipimo; watakaa ndani yake kizazi baada ya kizazi.