Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 25:9, 10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango la Makpela kwenye shamba la Efroni mwana wa Zohari Mhiti, lililo mbele ya Mamre,+ 10 shamba ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hethi. Abrahamu alizikwa huko pamoja na Sara mke wake.+

  • Mwanzo 49:29-33
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 29 Baada ya hayo aliwapa maagizo haya: “Nakaribia kufa.*+ Nizikeni pamoja na baba zangu katika pango lililo kwenye shamba la Efroni Mhiti,+ 30 pango lililo katika shamba la Makpela mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa Efroni Mhiti ili liwe mahali pa kuzikia. 31 Walimzika huko Abrahamu na Sara mke wake.+ Walimzika huko Isaka+ na Rebeka mke wake, na huko ndiko nilikomzika Lea. 32 Shamba hilo na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa wana wa Hethi.”+

      33 Basi Yakobo akamaliza kuwapa wanawe maagizo hayo. Kisha akairudisha miguu yake kitandani, akakata pumzi, naye akazikwa pamoja na watu wake.*+

  • Mwanzo 50:13, 14
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 13 Wanawe walimbeba na kumpeleka katika nchi ya Kanaani na kumzika katika pango lililo katika shamba la Makpela, shamba lililo mbele ya Mamre ambalo Abrahamu alikuwa amenunua kutoka kwa Efroni Mhiti ili awazike humo watu wake.+ 14 Baada ya kumzika baba yake, Yosefu akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wote walioenda naye kumzika baba yake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki