Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 13:14, 15
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 14 Yehova akamwambia hivi Abramu baada ya Loti kujitenga naye: “Tafadhali, inua macho yako, na kutoka mahali ulipo tazama kaskazini na kusini, mashariki na magharibi, 15 kwa sababu nchi yote unayoona, nitakupa wewe na uzao wako* iwe miliki yenu ya kudumu.+

  • Mwanzo 26:3, 4
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 Kaa kama mgeni katika nchi hii,+ nami nitaendelea kuwa pamoja nawe na kukubariki kwa sababu nitakupa wewe na uzao wako* nchi zote hizi,+ nami nitatimiza kiapo hiki nilichomwapia Abrahamu baba yako:+ 4 ‘Nitaufanya uzao* wako uwe mwingi kama nyota za mbinguni;+ nami nitaupa uzao* wako nchi zote hizi;+ na kupitia uzao* wako mataifa yote ya dunia yatajipatia baraka,’+

  • Kumbukumbu la Torati 34:4
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Kisha Yehova akamwambia hivi: “Hii ndiyo nchi ambayo nilimwapia Abrahamu, Isaka, na Yakobo, niliposema, ‘Nitaupa uzao wako* nchi hii.’+ Nimekuruhusu uione kwa macho yako mwenyewe, lakini hutavuka kuingia humo.”+

  • Matendo 7:4, 5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Ndipo akaondoka katika nchi ya Wakaldayo, akaanza kuishi Harani. Na kutoka hapo, baada ya baba yake kufa,+ Mungu akamwagiza ahamie nchi hii ambayo mnaishi sasa.+ 5 Lakini hakumpa urithi wowote ndani yake, hapana, hata sehemu ya kutosha kukanyaga kwa mguu; bali aliahidi atampa aimiliki yeye na baada yake uzao wake,*+ ingawa bado hakuwa na mtoto.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki