-
Mambo ya Walawi 14:53Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
53 Kisha atamwachilia ndege aliye hai aende zake mashambani nje ya jiji, naye ataitolea nyumba hiyo dhabihu ya kufunika dhambi, nayo itakuwa safi.
-
-
Mambo ya Walawi 16:21, 22Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi huyo aliye hai na kuungama juu yake makosa yote ya Waisraeli na maovu yao yote na dhambi zao zote, ataziweka juu ya kichwa cha mbuzi+ huyo na kumwagiza mtu aliyechaguliwa* ampeleke mbuzi huyo nyikani. 22 Mbuzi huyo atazibeba dhambi zao zote+ na kuzipeleka jangwani,+ mtu huyo atampeleka mbuzi huyo na kumwacha aende zake nyikani.+
-
-
Isaya 53:4Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
Lakini tulimwona kama mtu aliyepata mapigo, aliyepigwa na Mungu na kuteswa.
-