-
Kutoka 23:31-33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 “Nitaweka mpaka wenu kuanzia Bahari Nyekundu mpaka bahari ya Wafilisti na kuanzia nyikani mpaka kwenye Mto Efrati;+ kwa maana nitawatia wakaaji wa nchi hiyo mikononi mwenu, nanyi mtawafukuza kutoka mbele yenu.+ 32 Hampaswi kufanya agano pamoja nao wala na miungu yao.+ 33 Hawapaswi kuishi katika nchi yenu, wasije wakasababisha mnitendee dhambi. Mkiiabudu miungu yao, kwa hakika itakuwa mtego kwenu.”+
-
-
Yoshua 23:12, 13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 “Lakini mkimwacha na kushikamana na watu wa mataifa haya yaliyobaki+ na kuoana nao+ na kushirikiana nao, 13 mjue kwa hakika kwamba Yehova Mungu wenu hataendelea kuyafukuza* mataifa haya kwa ajili yenu.+ Yatakuwa mtego wa kuwanasa, nayo yatakuwa mjeledi wa kuwachapa mbavuni+ na miiba machoni mwenu mpaka mtakapoangamia kutoka katika nchi hii nzuri ambayo Yehova Mungu wenu amewapa.
-