-
Hesabu 16:46, 47Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
46 Kisha Musa akamwambia Haruni, “Chukua chetezo uweke moto ndani yake kutoka katika madhabahu+ na uweke uvumba juu yake, nawe uende haraka kwao na kuufukiza ili dhambi yao ifunikwe,+ kwa sababu Yehova amekasirika. Pigo limeanza!” 47 Mara moja Haruni akachukua chetezo, kama Musa alivyomwambia, akakimbia katikati ya kusanyiko hilo, na pigo lilikuwa limeanza kuwaathiri watu. Basi akaweka uvumba juu ya chetezo, akaanza kuufukiza ili dhambi yao ifunikwe.
-