-
2 Mambo ya Nyakati 35:20-25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Baada ya hayo yote, Yosia alipokuwa ametayarisha hekalu,* Mfalme Neko+ wa Misri alipanda kuja kupigana Karkemishi karibu na Mto Efrati. Kisha Yosia akaenda kukabiliana naye.+ 21 Kwa hiyo akamtumia Yosia wajumbe, akisema: “Vita hivi vinakuhusuje, Ee mfalme wa Yuda? Sijaja kupigana nawe leo, nimekuja kupigana na nyumba nyingine, na Mungu anasema kwamba ninapaswa kufanya haraka. Kwa faida yako mwenyewe, acha kumpinga Mungu, aliye pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.” 22 Hata hivyo, Yosia hakugeuka na kumwacha, lakini alibadili sura yake+ ili apigane naye, akakataa kabisa kusikiliza maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani mwa Mungu. Basi akaja kupigana naye katika Nchi Tambarare ya Megido.+
23 Na wapiga mishale wakampiga Mfalme Yosia, akawaambia watumishi wake: “Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana.” 24 Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa garini, wakamweka kwenye gari lake la pili la vita na kumpeleka Yerusalemu. Kwa hiyo akafa na kuzikwa katika kaburi la mababu zake,+ na watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia. 25 Na Yeremia+ akamwimbia Yosia wimbo wa maombolezo, na tangu siku hiyo waimbaji wote wa kiume na wa kike+ wanaendelea kuimba kumhusu Yosia katika nyimbo zao za huzuni;* na uamuzi ukafanywa kwamba nyimbo hizo zinapaswa kuimbwa katika nchi ya Israeli, nazo zimeandikwa katika nyimbo za huzuni.
-