-
Yeremia 37:1, 2Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
37 Na Mfalme Sedekia+ mwana wa Yosia akaanza kutawala baada ya Konia*+ mwana wa Yehoyakimu, kwa maana Mfalme Nebukadneza* wa Babiloni alikuwa amemweka kuwa mfalme katika nchi ya Yuda.+ 2 Lakini yeye na watumishi wake na watu wa nchi hawakuyasikiliza maneno ya Yehova yaliyosemwa kupitia nabii Yeremia.
-
-
Yeremia 38:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Mfalme Sedekia akajibu: “Tazama! Yuko mikononi mwenu, kwa maana mfalme hawezi kufanya jambo lolote ili kuwazuia.”
6 Basi wakamchukua Yeremia na kumtupa ndani ya tangi la maji la Malkiya mwana wa mfalme, lililokuwa katika Ua wa Walinzi.+ Wakamshusha Yeremia ndani kwa kamba. Basi hapakuwa na maji ndani ya tangi hilo, ila matope tu, naye Yeremia akaanza kuzama ndani ya matope.
-