Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 23:9, 10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Aliyemfuata ni Eleazari+ mwana wa Dodo+ mwana wa Ahohi, naye alikuwa miongoni mwa mashujaa hao watatu hodari waliokuwa na Daudi walipowadhihaki Wafilisti. Walikuwa wamekusanyika huko kwa ajili ya vita, na wanaume wa Israeli walipokimbia, 10 alisimama imara na kuendelea kuwaua Wafilisti mpaka mkono wake ulipochoka na kuganda kwa sababu ya kuushika upanga.+ Basi Yehova akawapa ushindi* mkubwa siku hiyo;+ na watu wakamfuata Eleazari ili kuchukua nyara za watu waliouawa.

  • 2 Samweli 23:15-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 15 Kisha Daudi akasema alichotamani: “Laiti ningekunywa maji kutoka katika tangi lililo karibu na lango la Bethlehemu!” 16 Ndipo wale mashujaa watatu hodari wakaingia kwa nguvu katika kambi ya Wafilisti, wakateka maji kutoka katika tangi hilo lililo karibu na lango la Bethlehemu na kumletea Daudi; lakini akakataa kuyanywa, akayamwaga mbele za Yehova.+ 17 Akasema: “Ni jambo nisiloweza kamwe kuwazia, Ee Yehova, kufanya hivyo! Je, ninywe damu+ ya wanaume walioenda kuhatarisha uhai wao?”* Basi akakataa kuyanywa. Hayo ndiyo mambo waliyotenda mashujaa wake watatu hodari.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki