Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hesabu 28:11-15
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 11 “‘Mwanzoni mwa kila mwezi* mtamtolea Yehova dhabihu ya kuteketezwa ya ng’ombe dume wawili wachanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo dume saba wasio na kasoro wote wa umri wa mwaka mmoja,+ 12 na toleo la nafaka la sehemu tatu za kumi za vipimo vya unga laini uliochanganywa na mafuta+ kwa ajili ya kila ng’ombe dume na toleo la nafaka la sehemu mbili za kumi za vipimo vya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya kondoo dume mmoja,+ 13 na toleo la nafaka la sehemu moja ya kumi ya kipimo cha unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya kila mwanakondoo dume; mtavitoa vitu hivyo vikiwa dhabihu inayochomwa kwa moto yenye harufu inayompendeza*+ Yehova. 14 Na matoleo ya kinywaji ya dhabihu hiyo yanapaswa kuwa nusu ya hini ya divai kwa ajili ya ng’ombe dume+ na sehemu ya tatu ya hini kwa ajili ya kondoo dume+ na robo ya hini kwa ajili ya mwanakondoo dume.+ Hiyo ndiyo dhabihu ya kuteketezwa inayopaswa kutolewa kila mwezi kwa mwaka mzima. 15 Pia, mwanambuzi mmoja anapaswa kutolewa kwa Yehova ili kuwa dhabihu ya dhambi; atatolewa na dhabihu ya kuteketezwa inayotolewa kwa ukawaida pamoja na toleo lake la kinywaji.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki