-
Ayubu 20:26-29Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
26 Giza zito linasubiri hazina zake;
Moto ambao haukuwashwa na yeyote utamla;
Msiba unamsubiri yeyote atakayeokoka katika hema lake.
27 Mbingu zitafunua kosa lake;
Dunia itainuka dhidi yake.
28 Mafuriko yataifagilia mbali nyumba yake;
Yatakuwa mafuriko yenye nguvu katika siku ya hasira ya Mungu.
29 Hilo ndilo fungu ambalo Mungu atampa mwovu,
Urithi ambao Mungu amemtangazia.”
-