35 ‘Hakuna mtu hata mmoja wa kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa kwamba nitawapa baba zenu,+ 36 isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na wanawe nchi hiyo aliyoikanyaga kwa miguu yake, kwa sababu amenifuata mimi Yehova kwa moyo wote.+